Kijukuu cha ngoyayi
JF-Expert Member
- Oct 27, 2018
- 2,918
- 5,523
KUNA MWANACHAMA WA CCM AMEANDIKA KUWAAULIZA WANA CCM WENZAKE MSOME👇
Hivi Tatizo letu ni Chadema Kweli?
Wana CCM wenzangu naomba tujiulize, hivi wanaotusumbua ni Chadema kweli au ni Wananchi?
Waliotukataa ni Chadema au ni Wananchi?
Chadema ni nani Hawa? Wako wangapi? Mbona takwimu zetu mara zote huonesha ni wachache wasio na madhara?
Mbona hawana Jeshi hawa, wanao-ongea kwenye majukwaa wako watatu tu yuko Lisu Heche na Lema? Sisi tuna wengi sana, tuna Kila aina ya raslimali Hii hofu yetu inatoakana na nini?
Mbona sisi tunawanachama wengi zaidi? Wanamuziki wote wanatuunga Mkono sisi? Comedians wote, waaigizaji wote, vyomba vyote viko kwetu!! Wao pesa hawana wanategemea tone tone sisi tuna Kila kitu!!
Nauliza Ndugu zangu wapi Chadema? Je ni hoja zao? Je wametuzidi lini wanachama?
Nani ametukataa sisi Wana CCM? Ni Chadema au ni Wananchi?
Wana CCM tujiulize vizuri, nahisi tunatafuta majawabu katika maswali yasiyo sahihi!!
Tumekataliwa na nani?
Kama wananchi wangekuwa upande wetu kweli Chadema ingekuwa ni tatizo kwetu? Hofu yetu inatoka wapi kama Chadema haina wanachama na haiungwi Mkono na Wananchi?
Mbona ni kama tumeacha tatizo tunashughulika na matokeo?
Hivi tukifanikiwa kuiondosha Chadema kwenye Ramani ya nchi yetu hivi tunaamini tutakuwa na amani? Au ndio tunaamini imani ya Wananchi itarudi kwetu?
Na hapa tunahitaji kuifuta Chadema au kuwafuta wenye imani ya Ki-Chadema? Tukiamua Hilo tuna hakika hatutawafuta na wanaovaa kijani kama sisi?
Tuanze kutafuta kipimo Cha kupima tunaovaa kijani imani yetu Iko wapi
Mbona matendo haya yanazidi kuumiza walio wetu kuliko hao Chadema?
Hii chuki mnafikiri inamipaka? Baada ya kuwaumiza na kuwatweza huwa tunakaa kufanya tathmini ya namna tulivyowavutia wananchi? Au tukimaliza tunaishia kusema tumewakomesha?
Hivi wako watu makini wanaopita na kufanya tathmini ya faida na madhara ya matendo yetu kweli? Au tunaishia kupongezana na kusema watatutambua sisi nani?
Nauliza na naomba mtu anijibu, Je tatizo letu ni Chadema Kweli au ni Wananchi waliotukataa? Na haya yanayoendelea tuna amini yatasaidia kurejesha imani kwa wananchi?