Maswali ya hovyo yanayoulizwa na wabunge wa Chadema bungeni!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Waziri Mkuu wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefunguka na kuwapa ushauri Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu tetesi za kuporwa ushindi wa Kata kadhaa ambazo wao wanaona walishinda na kuwataka kukata rufaa.

Majaliwa.jpg

Kassim Majaliwa amesema hayo leo Februari 8, 2018 akiwa anajibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge mbalimbali, ambapo Mbunge wa viti maalum CHADEMA Devotha Minja alitaka kufahamu kama ni sera ya Serikali ya awamu ya tano kupora ushindi kwa watu ambao wameshinda kihalali.

Devotha Minja alihoji suala hilo na kudai kuwa katika baadho ya Kata zikiwepo Kata ya Sofi Malinyi CHADEMA ilipata kura 1,908 wakati CCM ilipata kura 1,878, Kata ya Siuyi Singida CHADEMA ilipata kura 1,358 huku CCM ikipata kura 1,304 lakini katika Kata hizo CCM ilitangazwa kushindi dhidi ya CHADEMA, ndipo hapa Waziri Mkuu aliposema kuwa anaamini Tume ya Uchaguzi haiwezi kutangaza matokeo ndivyo sivyo.

"Sitarajii kama Tume ya Uchaguzi (NEC) inafanya kazi ya kutangaza walioshindwa na kuwaacha walioshinda na masuala haya ya tume serikali imeweka utaratibu na tumeunda chombo kinachoshughulikia chaguzi zote nchini Tume ya Uchaguzi (NEC) lakini chombo kingine ni ile kwenye Mamlaka ya Serikali za mitaa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na vyombo hivyo lakini tunazo sheria zinazosimamia simamia uchaguzi na zote hizi zinasimamiwa na Tume" alisema Majaliwa

Majaliwa aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa kwa mujibu wa Sheria hizo zinatoa nafasi kukutana na vyama mbalimbali ambavyo havijaridhika juu na matokeo ya uchaguzi hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashauri CHADEMA kufanya hivyo ili kutafuta haki yao kama wanaona kuna haki imeporwa.

"Ipo Sheria inatoa miezi mitatu ya kukata rufaa juu ya hizo namba ulizosisoma mimi sina uhakika nazo, sasa Mhe Mbunge kama una uhakika na takwimu ulizosisoma kwamba hao wenye namba nyingi ndiyo walishinda lakini ametangazwa mwingine bado unayo fursa ya kukata rufaa kwa mujibu ya Sheria ya uchaguzi, kwa hiyo nikushauri kufuata chombo chetu na kwa kuwa sheria zipo na wewe una fursa ya kufuata sheria ile ili kupata haki yako ya msingi"

My take:
Hivi hili swali alilouliza Devotha lilitakiwa kuulizwa bungeni kweli?
Kwa nini wabunge wanatumia rasilimali zetu kuulizia mambo yanayojulikana kiutaratibu?
Source:EATV
 
Swali la Devotha, mtu anasema "wabunge wa chadema"
Sasa, unajiuliza ndani ya Devotha Minja kuna wabunge wangapi???
 
Umesema WABUNGE maana wengi lkn unataja mmoja. Uchama utaliua hili taifa
 
Hao cdm unataka wakaulize kwenye hizi mahakama zinazowanyima wabunge wa upinzani dhamana hata kama sheria inaruhusu? Alichofanya huyo mbunge ni kujiongeza maana sasa hivi mahakama inafanya kazi kwa kufuata nini magogoni inataka.
Kajiongeza kizembe!
mnaogopaje mahakama wakati mna mawakili wasomi?
 
Akichangia bungeni Goodluck Mlinga mbunge wa jimbo la Ulanga (CCM) alisema,

"Mh.m/kiti swala langu la kwanza ni ushukaji wa elimu ya Tanzania, kwa muda wa miaka 2 sasa waziri wa elimu amedumu ktk wizara hii lakini tumeshuhudia kwa uangukaji mkubwa wa elimu wa shule za serikali".

"Mimi sielewi hawa maprofesa wa Tanzania wana matatizo gani?, Ningekuwa mshauri wa raisi ningemshauri awachague watu kama wakina Msukuma au Lusinde ambao wameishia la saba wawe mawaziri wa elimu sababu wanajua matatizo yaliyowafanya wasiweze kusoma".
 
Kajiongeza kizembe!
mnaogopaje mahakama wakati mna mawakili wasomi?

Mawakili wasomi wapo tena wa kutosha, ila mahakimu wanamuogopa jamaa ile mbaya. Wote sasa hivi wanafanya kumfurahisha jamaa japo wanaona aibu kwa upuuzi wanaofanya.
 
Kuwamfuasi wa CHADEMA ni lazima akili zako ziwe na matege.
Kwa hiyo huoni jinsi alivo jibiwa vizuri kabisa?
We ulijua una miezi mitatu ya kukata rufaa? Au ndio nyie wavivu wa kufikiri,mnataka watu wafikirie kwa niaba yenu.
 
Back
Top Bottom