Maswali na Majibu Bungeni 14 Juni 2011

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Spika Ana Makinda yupo katika kiti chake tayari kuendesha mjadala wa maswali na majibu kabla ya kuendelea na hoja iliyoahirishwa jana ya kuchangia Mpango wa maendeleo 2011/12 - 2015/16
 
Mrema nauliza kuhusu mgogoro wa Ardhi wa Mwaka 2000 unaomhusu Bw. Lekule

Naibu waziri anasema serikali ina wajibu wa kulipa fidia kufuatia kubadilishwa matumizi ya Ardhi hiyo na kwamba tume imeundwa ili kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa nje ya mahakama kwa maridhiano

Hivyo mazungumzo yako wazi kwa fidia yoyote

Na spika anamtaka mh mrema kuwa kiunganishi kwa kufikia muafaka huo

maswali yanaendelea

Wizara ya Elimu
 
Serikali kuongeza udahili wa walimu wa Kata 19031, shahada zaidi ya 12 elfu na stashahada zaidi ya elfu saba wanatarajiwa kuhitimu na kukamilisha nyongeza hiyo

Maslahi na stahili za walimu kuboreshwa kwa kadiri ya uwezo wa serikali

swali la nyongeza

VIPI KUHUSU WALE AMBAO WAPO NYUMBANI NA HAWAJAAJIRIWA NA HAPA UNAELEZA KUONGEZA UDAHILI
 
Naibu waziri: hana hakika kama kweli kama wapo walimu wa aina hiyo kwani serikali ilitoa nafasi na waliajiriwa walimu zaidi ya elfu 9 wale wote walioomba ndio walioajiriwa na wizara imebaini kuwa wengi waliopo mitaani ni wale ambao hawajakamilisha viporo katika mitihani yao ili wahitimu (SUPS)
 
Swali la nyongeza

Serikali ina mpango gani wa kuwapunguzi kodi ya vifaa vya ujenzi walimu ili nao waweze kumudu kupata makazi kulingana na uwezo wa kipato chao
 
Spika amelitaja kama swali jipya na halistahili kuwa la nyongeza

kapotezewa

Wizara ya Nishati na Madini sasa
 
Ngeleja: Vijiji vinavyopitiwa na nyaya za umeme wakati wao hawana umeme

Wizara imeigiza TANESCO kupitia wakala wa Nishati vijijini kureview mpango huo na kupata transforma zitakazowezesha kusambaa umeme katika vijiji ambavyo nyaya za gidi ya Taifa zinapita

Swali la nyongeza
 
Fedha zitatoka wapi?

Waziri Ngeleja anasema fedha zishatengwa katika bajeti katika fungu ala wakala wa Nishati Vijijini
 
Lini serikali itatoa hati za kimila za ardhi?

Naibu Waziri: Kwa kushirikiana na MKURABITA serikali imefanikisha zoezi hilo na wilaya kadhaa zaoezi hilo linaendelea na linatarajiwa kukamilika mapema mwaka huu katika wilaya nyingine saba, na zaidi ya hati miliki za kimila 4000 zisahatolewa

Vijiji vimehimizwa kutimiza masharti husika ili kukamilisha zoezi hilo.
 
Ngeleja: Vijiji vinavyopitiwa na nyaya za umeme wakati wao hawana umemeWizara imeigiza TANESCO kupitia wakala wa Nishati vijijini kureview mpango huo na kupata transforma zitakazowezesha kusambaa umeme katika vijiji ambavyo nyaya za gidi ya Taifa zinapitaSwali la nyongeza
Asante kwa updates,lkn hilo la rural electrification naona kama linaota mbawa coz lipo tangu longi!
 
Swali la Nyongeza

Wilaya ya mpanda imekamilisha taratibu zote na kwa nini mpaka sasa mpango huo umecheleweshwa kwa makusudi?

Jibu: Naibu waziri anasema ikiwa kama wamekamilisha taratibu zote hizo Wizara itawaunga mkono kwa kupeleka maafisa wa fani husika ili kikamilisha zoezi hilo.

Duuh kapangua skadi kiaina
 
ataje kiasi sio kusema tuu ooh zimetengwa!

Hawezi kusema si unakumbuka ndio ile wizara ambayo fedha za karanga na soda kwa wageni kwa mwaka wametengewa milioni 350. sijui karanga za aina gani hizi yarabi!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lini serikali itatoa hati za kimila za ardhi?Naibu Waziri: Kwa kushirikiana na MKURABITA serikali imefanikisha zoezi hilo na wilaya kadhaa zaoezi hilo linaendelea na linatarajiwa kukamilika mapema mwaka huu katika wilaya nyingine saba, na zaidi ya hati miliki za kimila 4000 zisahatolewaVijiji vimehimizwa kutimiza masharti husika ili kukamilisha zoezi hilo.
hati za kimila, hapo sasa...! mkazo vijijini tu,vp wa mjini ambao humiliki ardhi kimila?
 
Back
Top Bottom