Maswali muhimu kuhusu Lowassa

Maswali muhimu kuhusu Lowassa

Tembulukoje

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2014
Posts
397
Reaction score
143
Nimekaa nikatafakari sana, nikajiuliza sana, nikaamua na mimi kutoa maoni yangu juu ya mwenendo wa siasa hapa nchini Tanzania hasa kwa kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Nimejiuliza maswali muhimu mawili (2) magumu ambayo nimeshindwa kupata majibu kusuhu huyu mgombea wa uraisi kupitia umoja wa vyama vya UKAWA.

1. Kwa nini vijana wengi hasa wasiokuwa na ajira, walalahoi na mamalishe humshabikia sana Lowassa wakati wasomi, wazee makini na kiujumla watu "MAKINI" wakimpinga? Je ni kwa sababu Lowassa "ANAUCHUKIA" umasikini? Je Lowassa akiwa raisi ataoneshaje kuwa ni kwel unauchukia umasikini kwa hawa mamalishe na hawa vijana wasiokuwa na kazi? Atafanya nini hasa kwa haya makundi anayopenda "KUJIOSHEA" wakati wa hoja zake za kutafuta kura? Nachokijua mimi hizo ni kauli za kisiasa tu katika kutafuta kura. Nasema hivyo kwa sabubu zifuatazo:-

a) Kwanza mimi siamini kama kuna urafiki kati ya "TAJIRI" na "MASIKINI". Hakuna huo urafiki, haupo.

b) Nyuma ya Lowassa kuna watu kama Lostam, Kalamagi ambao wote ni matajiri. Lowassa anatumia umasiki wa haya makundi kuyalaghai akijua pia kuwa ni ‘MASIKINI WA KUFIKIRI' na wasiokuwa na uwezo wa kutafakari mambo.

c) Tatizo la ajira kwa vijana kwa sasa halitatuliki kwa njia yoyote, hata kama ni kujenga viwanda kila kata. Vijana wanaohitimu vyuo ni wengi sana kila mwaka. Uwiano wa kila kazi moja inayotangazwa kwa sasa ni 1:90. Na bado watu tunazaa kama hatuna akili nzuri. Tatizo la ajira kwa sasa sio tena kusema utajenga viwanda. Hebu kama kweli unataka kuwa raisi njoo na hoja tofauti ili watu "MAKINI" tukuelewe.

2. Kwa nini Lowassa ameng'ang'ania sana uraisi? Kuna biashara gani pale ikulu? Hadi kufikia hatua ya kukisaliti na kukihama chama? Ana ajenda gani? Na kama ameweza kukisaliti chama kilichomlea tangu mwaka 1977 takribani miaka 38 atashindwa kuisaliti nchi kweli kwa miaka 5?

Lowassa kiujumla yuko na uroho wa madaraka, uraisi kwake ni kufa na kupona. Na mbaya zaidi anatumia kundi la vijana hasa wasiokuwa na ajira (wasiokuwa na uwezo wa kufikiria na kudadavua mambo) ambao ndo wengi kuwalaghai na kauli ya "NACHUKIA UMASIKI" wakati hakuna urafiki kati yake yeye tajiri na umasikini.
 
yani magufuli anasahaulika,mda huu mngetumia kumnadi mgombea wenu badala ya kujitahidi kumchafua lowasa,kiufupi ni kwamba ccm imechokwa na wananchi wanaopenda maendeleo,wale wananchi wanaofurahia kusafirishwa twiga bila pasi ya kusafiria ndio wanaoishabikia ccm



Magufuli hasahauliki kisa fisadi lowasa ndo umusahau
We endelea kujisahaulisha sasa wakat ndo anaeumiA vichwa vyenu upawa
 
nimeshangaa! huyo muuliza swali alitaka kuuliza swali tu ili ajibiwe' au alitaka atupe wasifu wa lowasa? na mm nikusaidie hata wakati kikwete anaingia madarakan na akaungwa mkono cjui na ww kama ulimuunga mkono kwa lipi? sasa hao nao wanaomshabikia lowasa wana matarajio yao! kama ikitokea wakampa madaraka akaharibu ni wao watajilaumu! hata mwanaume huwa hatafutiwi mke!
 
Kwanza ata kuandika hujui rostam unaandka lostam karamagi unaandka kalamagi mi nimershia apo sijaendlea uko chin mana nshaona pumba tu
 
Jitu gonjwa
Halina nguvu
Fisadi
Tamaa
Saliti
Nafiki
King'ang'anizi

Kwnn anataka sana urais

Huyo atakuwa ana tamaaa

Visasi

Kurudisha gharama zake za uchaguzi

Hatuko tayr kuachilia jizi liende ikulu

Vp hawa waliopo sasa wanaoiba rasolimali zetu yan twiga na shngo yake ndefu bdo anafit ndan ya ndege
 
SOMA HII KWA MAKINI: Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zali". Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu. Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari.


Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'nyiro kwa kujaribu....
Sidhani kama Tanzania ni maabara ya kuendelea kufanya majaribio ya akina Kikwete...bila lengo mahususi, dira na muelekeo unaoeleweka zaidi ya utukufu wa kushika atamu....!!
 
napenda kutanguliza samahani kwa mtoa mada. kwa sababu nitapinga kwa ukali sana nikisema "namba c ni upumbavu kuliko upumbavu wowote uliopata kuandikwa na wapumbavu duniani... Ajira hutengenezwa kutokana na sera au mfumo wa nchi. kukosekana kwa ajira ni mfumo na sera mbovu za utawala" Aidha mtoa mada ameandika "wasomi ni watu makini" je vyama vyetu vya ushirika na viwanda walioviuwa hawakuwa wasomi? Je hao mamalishe wakati wa kutafuta uhuru si ndio waliokuwa mstari wa mbele mtoa mada amesahau?

Watu wamekata tamaa, wanaojiita wasomi wameifikisha nchi hii mahala pabaya... Wasomi wenye dhamana wanashindana kufilisi kama si kujimilikisha mali na rasilimali za umma huku tukiaminishwa TUENDELEE KUWAAMINI DAAAH!!!
 
SOMA HII KWA MAKINI: Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zali". Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu. Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari.


Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'nyiro kwa kujaribu....
Sidhani kama Tanzania ni maabara ya kuendelea kufanya majaribio ya akina Kikwete...bila lengo mahususi, dira na muelekeo unaoeleweka zaidi ya utukufu wa kushika atamu....!!


Kwa hio unataka tuwaamn hao vigeu geu wako wakina mbowe msigwa na mbatia?

Kama wanaweza hadi kuzgeuka kauli zao ?
Watashindwa kukugeuka ww mwananchi wa kawaida?

Tumuamn lowassa?
Khaaaaaa
Kwan mwaka 2008
Alipoiba akalazishwa ajiuzuru ulikuwa hujazaliwa?

Achen kujitia pamba masikion nyinyi

Hatuwez kuwaamn wanafiki kama wana ukawa
 
Jitu gonjwa
Halina nguvu
Fisadi
Tamaa
Saliti
Nafiki
King'ang'anizi

Kwnn anataka sana urais

Huyo atakuwa ana tamaaa

Visasi

Kurudisha gharama zake za uchaguzi

Hatuko tayr kuachilia jizi liende ikulu

wew umerogwa na tena ni mgonjwa hujitambui.
ikulu sio ya mamaako.

utavimba upasuke lakini kaa ukijua lowassa ndio rais wako.
 
Kwa hio unataka tuwaamn hao vigeu geu wako wakina mbowe msigwa na mbatia?

Kama wanaweza hadi kuzgeuka kauli zao ?
Watashindwa kukugeuka ww mwananchi wa kawaida?

Tumuamn lowassa?
Khaaaaaa
Kwan mwaka 2008
Alipoiba akalazishwa ajiuzuru ulikuwa hujazaliwa?

Achen kujitia pamba masikion nyinyi

Hatuwez kuwaamn wanafiki kama wana ukawa

kaaa mkao wa kuliwa tukupe dozi.labda utajitambua kenge kasoro mkia.
 
Lowasa
atawanyoosha mwaka huu

Siku zote nawaambia vijana wa UKAWA akili chache

Ona sasa huyu mchumia pesa anayoyaongea
Nonsense

Toen hoja kwa hoja


Jibu hoja zangu hapo
Nmesema lowasa mgonjwa
Mnafiki
Mwizi wa rasilimali ameiba ranchi ya taifa na kuwapa wamasai wenye ng'ombe zake had ndugu zetu wakulima na wafugaj wanauana

Mwz
Aliiba kwenye Richmond
Bunge zma likathbitisha hilo
Na akawajibishwa .


Njoon na hoja
Sio kama za huyo mchumia pesa
 
Lowasa
atawanyoosha mwaka huu

Hoja yako nn hapo?
Mbona mnakuwa hivo?


Nijib bas

Nmesema lowasa mwz
Mgonjwa
Ana tamaa
Visasi
Rafiki wa mafisad
Muongo anatudanganya atatufanya matajiri wakat monduli kwake watu n maskin had leo

Mbinafs lami amejenga inaishia kwake tu.
 
Nimekaa nikatafakari sana, nikajiuliza sana, nikaamua na mimi kutoa maoni yangu juu ya mwenendo wa siasa hapa nchini Tanzania hasa kwa kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Nimejiuliza maswali muhimu mawili (2) magumu ambayo nimeshindwa kupata majibu kusuhu huyu mgombea wa uraisi kupitia umoja wa vyama vya UKAWA.

1. Kwa nini vijana wengi hasa wasiokuwa na ajira, walalahoi na mamalishe humshabikia sana Lowassa wakati wasomi, wazee makini na kiujumla watu “MAKINI” wakimpinga? Je ni kwa sababu Lowassa “ANAUCHUKIA” umasikini? Je Lowassa akiwa raisi ataoneshaje kuwa ni kwel unauchukia umasikini kwa hawa mamalishe na hawa vijana wasiokuwa na kazi? Atafanya nini hasa kwa haya makundi anayopenda “KUJIOSHEA” wakati wa hoja zake za kutafuta kura? Nachokijua mimi hizo ni kauli za kisiasa tu katika kutafuta kura. Nasema hivyo kwa sabubu zifuatazo:-

a) Kwanza mimi siamini kama kuna urafiki kati ya “TAJIRI” na “MASIKINI”. Hakuna huo urafiki, haupo.

b) Nyuma ya Lowassa kuna watu kama Lostam, Kalamagi ambao wote ni matajiri. Lowassa anatumia umasiki wa haya makundi kuyalaghai akijua pia kuwa ni ‘MASIKINI WA KUFIKIRI’ na wasiokuwa na uwezo wa kutafakari mambo.

c) Tatizo la ajira kwa vijana kwa sasa halitatuliki kwa njia yoyote, hata kama ni kujenga viwanda kila kata. Vijana wanaohitimu vyuo ni wengi sana kila mwaka. Uwiano wa kila kazi moja inayotangazwa kwa sasa ni 1:90. Na bado watu tunazaa kama hatuna akili nzuri. Tatizo la ajira kwa sasa sio tena kusema utajenga viwanda. Hebu kama kweli unataka kuwa raisi njoo na hoja tofauti ili watu “MAKINI” tukuelewe.

2. Kwa nini Lowassa ameng’ang’ania sana uraisi? Kuna biashara gani pale ikulu? Hadi kufikia hatua ya kukisaliti na kukihama chama? Ana ajenda gani? Na kama ameweza kukisaliti chama kilichomlea tangu mwaka 1977 takribani miaka 38 atashindwa kuisaliti nchi kweli kwa miaka 5?

Lowassa kiujumla yuko na uroho wa madaraka, uraisi kwake ni kufa na kupona. Na mbaya zaidi anatumia kundi la vijana hasa wasiokuwa na ajira (wasiokuwa na uwezo wa kufikiria na kudadavua mambo) ambao ndo wengi kuwalaghai na kauli ya “NACHUKIA UMASIKI” wakati hakuna urafiki kati yake yeye tajiri na umasikini.

Mkuu usijisumbue, watanzania tunaojitambua hatuwezi kumshabikia fisadi papa aliyepora ardhi ya watanzania na kutumia madaraka kujilimbikizia mali na ambaye ni zao la CCM maslahi. Huyu katumia ujuha wa Mbowe na wafuasi wasiojitambua.
Hata hao unaosema mama lishe nk wana akili zao na wameshashtuka baada ya kuona kakosa sapoti ya watu makini na baada ya wafuasi wa Chadema kukosa hoja na kuwatukana akina Mzee Butiku. Nasubiri Mzee Warioba atakapoongea ndo mwisho wa Ukawa!
Hawana tena agenda ya kupinga ufisadi ni kuingia madarakani tu! Haiwezi kuwafikisha mbali.
Yuko wapi John Mnyika? Sijamsikia na tunamsubiri aje ale matapishi yake. Asipomnadi Lowassa na akigombea jimbo kama alivyopangiwa basi tutajua kidogo ana akili - anatafuta ubunge lakini kagoma kushiriki upuuzi wa kumsafisha fisadi. Wasiojitambua kama Msigwa na Mtatiro ndo wanajipoteza kisiasa.
 
Jitu gonjwa
Halina nguvu
Fisadi
Tamaa
Saliti
Nafiki
King'ang'anizi

Kwnn anataka sana urais

Huyo atakuwa ana tamaaa

Visasi

Kurudisha gharama zake za uchaguzi

Hatuko tayr kuachilia jizi liende ikulu

Utapata jibu October 25. Tuliza Boli
 
Siku zote nawaambia vijana wa UKAWA akili chache

Ona sasa huyu mchumia pesa anayoyaongea
Nonsense

Toen hoja kwa hoja


Jibu hoja zangu hapo
Nmesema lowasa mgonjwa
Mnafiki
Mwizi wa rasilimali ameiba ranchi ya taifa na kuwapa wamasai wenye ng'ombe zake had ndugu zetu wakulima na wafugaj wanauana

Mwz
Aliiba kwenye Richmond
Bunge zma likathbitisha hilo
Na akawajibishwa .


Njoon na hoja
Sio kama za huyo mchumia pesa

huo ufisadi aliufanya akiwa chama gani?. na walichukua hatua gani juu yake?. UkAWA hakuna fisadi mafisadi wamejificha ugambani maana fisadi hawezi kuwa salama nje ya ccm. swala la ugonjwa usilisemee mwenyekiti wenu anatezi........ mbona hajamfukuza uenyekiti?. ilikuwa lazima awape wamasai maana ndio aliokuwa anawatumikia ka mbuge wao ulitaka awape wagogo?. Si msaliti nyinyi ndio wasaliti. katiba yenu inasema anayekubalika ndio achaguliwe nyie mkamukata mlitaka aende wapi na mafuriko ya watu waliokuwa nyuma yake?. Kamanda mmoja UKAWA ni sawa na magamba buku. LOWASA atawanyosha mwaka huu mtajuuuuta kumkata. lete hojaa na sio vioja.
 
Back
Top Bottom