Maswali magumu kuhusu uchawi/ushirikina

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,954
Naamini mko poa wakuu,

Mi kuna maswali huwa najiulizaga na sijawahi kuyapatia majibu.

1.Nini tofauti ya mchawi na mwanga?

2.Nitamjuaje mchawi au mwanga (dalili na ishara zake)

3.Nini lengo la mchawi au mwanga?

4.Nasikia kuwa wachawi au wanga hawaibi pesa,sasa mbona nasikia uchawi na wanga unanunuliwa kwa pesa?

5.Je wachawi au wanga wakikutana mchana au usiku wasipokuwa katika hali ya kichawi/kiwanga huwa wanaongelea mambo yao ya kiwanga/kichawi?

6. Kipi hasa kinachoweza kumfanya mchawi akuloge au mwanga akuwangie?

7.Hivi unaweza kumuona mchawi au mwanga bila kufanyiwa mambo ya kiuganga?

8. Kwanini watu wanaohisiwa wanga au wachawi ni jamii ambazo ni "masikini, fukara"?

9.Je kuna wachawi/wanga matajiri?

10. Inakuwajekuwaje hadi wachawi/wanga wanafanya mambo yao bila kuonekana ktk hali ya kawaida hadi ufanyiwe uganga?

11.Kwanini magonjwa ya kulogwa wanasema hayaonekani katika vipimo vya hospitali?

12.Ufanye nini ili usilogwe/usiwangiwe katika maisha yako yote ?

13.Je ni kweli wachawi/wanga wanakula nyama za binadamu. Kama ndio, kwanini hawali zile za wanyama poli/wakufugwa?

14.Kipi kitakufanya ujue kwamba hiyo sehemu unayopita/uliyokaa wanapita/wamekaa wachawi?

15. Ushahidi gani utawaeleza watu kuwa fulani anakuloga na ukaleta maana kwa watu unaowaelezea?

16.Kuna tofauti gani kati ya ugonjwa wa Hospitali na ugonjwa wa kulogwa?

Hapo kwa leo, unaweza ukaongezea maswali au nitayaongezea kutegemea na majibu yenu wakuu.
 
1.Nini tofauti ya mchawi na mwanga ......??
MCHAWI NI MGANGA...MWANGA NDIO MCHAWI (YAANI HANA UWEZO WA KUKUCHAWIA 100%, ATAKUYUMBISHA TU...SAMPO HII NDO HUTIMULIWAKWA MAOMBI YA KIKRISTO...ILA SAMPO YA WAGANGA WALIOKO HATA IKULU, NI WALOWEZI AMBAO AKIJA KWETU ATAOMBA KUOMBEWA, ATAFANYIWA IBADA, ATASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII...LAKINI KUMBE NDIO MMILIKI WA ANGA AMBALO NYIE WOTE WAISLAMU KWA WAKRISTO MPO CHINI YAKE, NA KIONGOZI YEYOTE ANAYETEMBEA ENEO HILO LAZIMA WAGANGA WAKE WAPATE KIBALI KWAKE.)

2.Nitamjuaje mchawi au mwanga ........(dalili na ishara zake)
MCHAWI HUTAMJUA, LAZIMA NA WEWE UWE MCHAWI...CHUKULIA MFANO WA JINSI MFUMO WA USALAMA WA TAIFA UNAVYOFANYA KAZI...UNAYEWEZA KUMJUA NI MWANGA ANAYEJINASIBU KUWA MCHAWI...HAWA NDO WANAODONDOKA NA UNGO, N.K.

3.Nini lengo la mchawi au mwanga ???
LENGO LA MCHAWI HALINA TOFAUTI NA SHEHE WA UAMSHO AU MCHUNGAJI AMBAE KIU YAKE NI KUMILIKI EMPIRE/ESTATE...LENGO LA MWANGA NI KUKUKOMOA...HUYU NDO ANALOGA...MCHAWI HALOGI...MCHAWI YUKO KWENYE MISHION ZAKE...UKIJIPENDEKEZA ANGA ZAKE NDO HIVYO, UTAMUONA KAMA MWANGA.

4.Nasikia kuwa wachawi au wanga hawaibi pesa,sasa mbona nasikia uchawi na wanga unanunuliwa kwa pesa ??
WACHAWI WANAIBA..MFANO HAI NI KAMPUNI ZA MABASI KADHAA UBUNGO - SITAYATAJA, ILA KUNA MMOJA ALIPEWA MTAJI NA MAMA YAKE ALIYEIBA BENKI...HUYU MAMA ALIWACONTACT WACHAWI WENZIE...WALIOWIN TENDA WAKAPEWA MBINU NA KUHAMISHA LOCKER ZA BENKI (BULK)..SITITAJA BENKI...THEN AKAWAPA MALIPO YAO WAKASEPA, YEYE AKAMPA MTAJI WA MABASI MWANAE. YAANI UCHAWI NI KAZI AMBAYO PIA BOSI ANA BOSI WAKE NA WANAKUBALIANA MSHAHARA. MFANO MWINGINE NI AJALI YA LUCKY VICENT...DAMU ILIYOKUWA INAHITAJIKA ILIZIDI, WALE MADOGO 3 WAKASALIMIKA, MKUU KWA HAYA AKAONA AWARUDISHE TU...MAISHA YAKASONGA.

5.Je wachawi au wanga wakikutana mchana au usiku wasipokuwa katika hali ya kichawi/kiwanga huwa wanaongelea mambo yao ya kiwanga/kichawi ???
HAWA WATU HAWAKUTANAGI...NI SAWA NA MWANAJESHI AKUTANE NA MGAMBO KUJADILI USALAMA WA NCHI.

6. Kipi hasa kinachoweza kumfanya mchawi akuloge au mwanga akuwangie ??
MWANGA ANAWANGA KULIPA KISASI...NA HAWEZI KUFANYA HAYO KAMA HAKUJUI NDIO MAANA MOSTLY UNAKUTA NI NDUGU AU RAFIKI WA KARIBU, WAAGUZI WANAKULA HELA ZENU MAANA WANALIJUA HILO. MCHAWI NI MWAJIRIWA WA MTU (TAJIRI, KIONGOZI ETC), NA ANAWEZA KUACCESS MAISHA YAKO KWA COMMAND YA BOSI.

7.Hivi unaweza kumuona mchawi au mwanga bila kufanyiwa mambo ya kiuganga ...??
MWANGA UNAWEZA KUMUONA HATA KWA MAOMBI, ACHILIA MBALI UGANGA...MCHAWI SAHAU HABARI ZAKE.

8. Kwanini watu wanaohisiwa wanga au wachawi ni jamii ambazo ni "masikini,fukara" ??
HAKUNA MCHAWI FUKARA...NENDA MASAKI, KIGAMBONI NA BUNJU UONE WALIVYOPOROMOSHA MAHEKALU. WANGA NDIO MASKINI.

9.Je kuna wachawi/wanga matajiri ???
WAPO..NENDA KIGAMBONI, BUNJU NA BAGAMOYO

10. Inakuwajekuwaje hadi wachawi/wanga wanafanya mambo yao bila kuonekana ktk hali ya kawaida hadi ufanyiwe uganga ???
WANAONEKANA. NI KAMA VILE HUWEZI KUMUONA YESU MOYONI MWAKO KAMA HUJAAMUA KUMUONA AU KUMKIRI.

11.Kwanini magonjwa ya kulogwa wanasema hayaonekani ktk vipimo vya hospitali ??
ELIMU DUNIA NA ELIMU YA KIROHO NI MBALIMBALI.

12.Ufanye nini ili usilogwe/usiwangiwe ktk maisha yako yote .......... ??
USIWE MCHEPUKO..BAKI NIA KUU...KAMA NI MUNGU IWE KWA MUNGU KWELI...KAMA NI UDHALIMU IWE UDHARIMU KWELI. UKIWA KATIKATI NDIO HATA BIBLIA IKASEMA UNAWEZA KUKAPIKWA/KUKATALIWA NA MUNGU NA SHETANI...

13.Je ni kweli wachawi/wanga wanakula nyama za binadamu ........Kama ndio, kwanini hawali zile za wanyama poli/wakufugwa ??
WANGA NDIO WANA HIVYO VIMBWANGA...WACHAWI WANAKULA KUKU KWA MRIJA KULE BUNJU, BAGAMOYO NA KIGAMBINI

14.Kipi kitakufanya ujue kwamba hiyo sehemu unayopita/uliyokaa wanapita/wamekaa wachawi ??
UNLESS YOU ARE IN BUSINESS, NDIO UTAJUA. HIVI WEWE UKINIKUTA NAONGEA NA MTU UTAJUA BILA SISI KUKUSHIRIKISHA?

15. Ushahidi gani utawaeleza watu kuwa fulani anakuloga na ukaleta maana kwa watu unaowaelezea ??
KATIBA HAITAMBUI UCHAWI. MEANING HAKUNA USHAHIDI.

16.Kuna tofauti gani kati ya ugonjwa wa Hospitali na ugonjwa wa kulogwa ??
MATIBABU.
 
1.Nini tofauti ya mchawi na mwanga?

MCHAWI ANA DHURU, AMA HATA K MWANGA YEYE NI MSUMBUFU ANA SUMBUA KAMA KUKUCHOSHA NA MENGINE KAMA HAYO

2.Nitamjuaje mchawi au mwanga (dalili na ishara zake)

HAWA WAPO KIROHO , HADI HUWE NA MACHO YA ROHONI AU SENSE ZA ROHONI KUWEZA KUWAHISI AU KUWATAMBUA. OTHERWISE UNAWEZA TUMIA NJIA ZA KUSIKIA SIKIA ILA SIO MAKINI SANA HAILETI MAJIBU SAHIHI.

UKIKAAAA VZURI NA MUNGU ATAKUJUZA MENGI NA KUKUFUNULIA PIA.

3.Nini lengo la mchawi au mwanga?

Labda nijibu hivi. Kila mmoja ana lengo lake katika uchawi hadi kujiunga.
1.kujilinda maana atakuwa miongon mwa pack yao so anahisi atapata sapoti kwao
2.haki, kisasi wengine hujiunga na kuwa mwanga kwa ajili ya kupata nguvu kutetekeleza hayo.
3. Kudhuru tu au kusumbua bila sababu wengine wana nature ya kuwa wasumbufu tu
N.k

4.Nasikia kuwa wachawi au wanga hawaibi pesa,sasa mbona nasikia uchawi na wanga unanunuliwa kwa pesa?
Kama nilivyo sema mwanzo starehe ghalama kuna wengine hizi ni starehe zao kun ambao wanapenda power tu.
Sio kila jambo linalo nunuliwa huwa linarudisha fedha mfano watu wananunua picha na kuziweka ndani kama pambo tu , au watu wananunua bia kama burudani haileti fedha walanini.

Ila kukujuza tu kila uchawi fulani una miko yake kuna mingine inakupa kuruhusu unaweza kujitajirisha kupitia kuroga watu na kuwatibu wakakulipa, chuma ulete n.k hayo yanaleta fedha pia

5.Je wachawi au wanga wakikutana mchana au usiku wasipokuwa katika hali ya kichawi/kiwanga huwa wanaongelea mambo yao ya kiwanga/kichawi?

Hapa wao wanaweza jibu ila kwa kawaida sio kwamba wao muda wote wapo kikazi zaidi kuna muda wana socialize kwa mambo yao kawaida tu , ndiio maan unaweza kaaa au kuishi na wachawi lakini usiwajue.

6. Kipi hasa kinachoweza kumfanya mchawi akuloge au mwanga akuwangie?
1.Hapa inaweza kuwa husda au sababu yeyote tu
2.kutesta zana zake hapa anafanya majaribio ya silaha mpya au nguvu zake kuona kama zimekomaa au not.

7.Hivi unaweza kumuona mchawi au mwanga bila kufanyiwa mambo ya kiuganga?

Yeah, inawezekana. Endapo utakuwa deep kwa MUNGU macho ya rohon YANAFUNGUKA TU.

Pia endapo mchawi aka kiuka miko au dawa zake kuisha au akasahau kupaka dawa za kutoonekana au akanaswa yote haya huweza kukufanya kuona.

8. Kwanini watu wanaohisiwa wanga au wachawi ni jamii ambazo ni "masikini, fukara"?
Hiii ni myth na mazoea ya siku nyingi kuwa wazee , wenye macho mekundu au masikini ndio huwa wachawi.
.lakini kuna matajiri wengi vijana na hata watoto wamekubuh humu

9.Je kuna wachawi/wanga matajiri?
Yeah wapo wengi tu. Tena hata wataaalamu na wasomi kibao wapo humu, viongozi n.k

10. Inakuwajekuwaje hadi wachawi/wanga wanafanya mambo yao bila kuonekana ktk hali ya kawaida hadi ufanyiwe uganga?
Hawa wanatumia dawa za kufunga machi ya kawaida
Uchawi ni vitu vya rohoni so inahitaji huwe na nguvu za rohoni kuwa gundua na kuwaona pia.

11.Kwanini magonjwa ya kulogwa wanasema hayaonekani katika vipimo vya hospitali?

Kwa sababu ni mambo ya kiimani.
Hayana scientific proof, haya pimwi katika vipimo vya mwili bali vya mambo ya imani. Ingawa matokeo yake huonkana mwilini

12.Ufanye nini ili usilogwe/usiwangiwe katika maisha yako yote ?
Zipo njia nyingi za kichawi kiganga na za giza zenye masharti na utumwa mwingi.

Lakini the best of the best GOD kaa vzuri n mshike MUNGU ALIYE HAI, BWANA MKUBWA, JINA LILILO KUU KUPITA YOTE , NIKO AMBAYE NIKO, ALFA NA OMEGA hizi zote ni codes zake ukikiaa vema naye hakun nguvu ingine itayojinyanyua agaist you ikashinda

13.Je ni kweli wachawi/wanga wanakula nyama za binadamu. Kama ndio, kwanini hawali zile za wanyama poli/wakufugwa?
1.Kila kitu kina sadaka, sadaka kubwa ni uhai wa bindamu.
2.Uhai wa binadamu unaongeza power kwa ambaye anatumia, ndio maan wao husema wazi kuwa wanajisikia weak kama wasipo tumia
3.ukiona mtu analiwa nyama jua hana mahusian vema na MUNGU so ibilisi ana rahisisha umauti wa watu.
4.prove ukuuu wenu kwa kula jamiii ya aina yako
5. Roho wanazo husika nazo katika uchawi zina demand hvyo
6. Nyama ya mtu ni tamu sana kulingana na maneno yao

14.Kipi kitakufanya ujue kwamba hiyo sehemu unayopita/uliyokaa wanapita/wamekaa wachawi?

Hapa kuna meng kuna sensi nyingi za rohoni.
1. Huwe vzuri na Mungu .
2. Huwe na madawa
3. Tumia wazoef wakupe huzoefu na kuhusianisha sehem zingine mfan kusikia nywele zina sisimka gafla, joto la gafla kuwepo, ukimya uliyo tokea gafla , kupata hofu gafla & kukosa amani , usingizi kukata gafla.
4.kuna wengine wata taka kujionyesha wapo hapo so utasikia makelele na ishara n.k

15. Ushahidi gani utawaeleza watu kuwa fulani anakuloga na ukaleta maana kwa watu unaowaelezea?
Hakuna ushahid utaothibitsha labda nguvu za kiimani zitumike ama umkate mtu katik mazingira tatanishi nyakati tatanishi n.k
16.Kuna tofauti gani kati ya ugonjwa wa Hospitali na ugonjwa wa kulogwa?

Hapo kwa leo, unaweza ukaongezea maswali au nitayaongezea kutegemea na majibu yenu wakuu.

17. Tofaut ya mchawi na mshirikina.
Mchawi anafanya mambo mwenyewe na miongoni mwa jamiii ya kilinge
.mshirikina ni mdau wa kwenda kwa waganga analipa watu wamfanyie sio memba huyu
 
Wapi mshana jr kuna jamaa anakuchokoza huku ktk elimu dunia njoo (utu-google-she) maana mwenzetu huko vzr ktk tasnia hii
 
1.Nini tofauti ya mchawi na mwanga ......??
MCHAWI NI MGANGA...MWANGA NDIO MCHAWI (YAANI HANA UWEZO WA KUKUCHAWIA 100%, ATAKUYUMBISHA TU...SAMPO HII NDO HUTIMULIWAKWA MAOMBI YA KIKRISTO...ILA SAMPO YA WAGANGA WALIOKO HATA IKULU, NI WALOWEZI AMBAO AKIJA KWETU ATAOMBA KUOMBEWA, ATAFANYIWA IBADA, ATASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII...LAKINI KUMBE NDIO MMILIKI WA ANGA AMBALO NYIE WOTE WAISLAMU KWA WAKRISTO MPO CHINI YAKE, NA KIONGOZI YEYOTE ANAYETEMBEA ENEO HILO LAZIMA WAGANGA WAKE WAPATE KIBALI KWAKE.)

2.Nitamjuaje mchawi au mwanga ........(dalili na ishara zake)
MCHAWI HUTAMJUA, LAZIMA NA WEWE UWE MCHAWI...CHUKULIA MFANO WA JINSI MFUMO WA USALAMA WA TAIFA UNAVYOFANYA KAZI...UNAYEWEZA KUMJUA NI MWANGA ANAYEJINASIBU KUWA MCHAWI...HAWA NDO WANAODONDOKA NA UNGO, N.K.

3.Nini lengo la mchawi au mwanga ???
LENGO LA MCHAWI HALINA TOFAUTI NA SHEHE WA UAMSHO AU MCHUNGAJI AMBAE KIU YAKE NI KUMILIKI EMPIRE/ESTATE...LENGO LA MWANGA NI KUKUKOMOA...HUYU NDO ANALOGA...MCHAWI HALOGI...MCHAWI YUKO KWENYE MISHION ZAKE...UKIJIPENDEKEZA ANGA ZAKE NDO HIVYO, UTAMUONA KAMA MWANGA.

4.Nasikia kuwa wachawi au wanga hawaibi pesa,sasa mbona nasikia uchawi na wanga unanunuliwa kwa pesa ??
WACHAWI WANAIBA..MFANO HAI NI KAMPUNI ZA MABASI KADHAA UBUNGO - SITAYATAJA, ILA KUNA MMOJA ALIPEWA MTAJI NA MAMA YAKE ALIYEIBA BENKI...HUYU MAMA ALIWACONTACT WACHAWI WENZIE...WALIOWIN TENDA WAKAPEWA MBINU NA KUHAMISHA LOCKER ZA BENKI (BULK)..SITITAJA BENKI...THEN AKAWAPA MALIPO YAO WAKASEPA, YEYE AKAMPA MTAJI WA MABASI MWANAE. YAANI UCHAWI NI KAZI AMBAYO PIA BOSI ANA BOSI WAKE NA WANAKUBALIANA MSHAHARA. MFANO MWINGINE NI AJALI YA LUCKY VICENT...DAMU ILIYOKUWA INAHITAJIKA ILIZIDI, WALE MADOGO 3 WAKASALIMIKA, MKUU KWA HAYA AKAONA AWARUDISHE TU...MAISHA YAKASONGA.

5.Je wachawi au wanga wakikutana mchana au usiku wasipokuwa katika hali ya kichawi/kiwanga huwa wanaongelea mambo yao ya kiwanga/kichawi ???
HAWA WATU HAWAKUTANAGI...NI SAWA NA MWANAJESHI AKUTANE NA MGAMBO KUJADILI USALAMA WA NCHI.

6. Kipi hasa kinachoweza kumfanya mchawi akuloge au mwanga akuwangie ??
MWANGA ANAWANGA KULIPA KISASI...NA HAWEZI KUFANYA HAYO KAMA HAKUJUI NDIO MAANA MOSTLY UNAKUTA NI NDUGU AU RAFIKI WA KARIBU, WAAGUZI WANAKULA HELA ZENU MAANA WANALIJUA HILO. MCHAWI NI MWAJIRIWA WA MTU (TAJIRI, KIONGOZI ETC), NA ANAWEZA KUACCESS MAISHA YAKO KWA COMMAND YA BOSI.

7.Hivi unaweza kumuona mchawi au mwanga bila kufanyiwa mambo ya kiuganga ...??
MWANGA UNAWEZA KUMUONA HATA KWA MAOMBI, ACHILIA MBALI UGANGA...MCHAWI SAHAU HABARI ZAKE.

8. Kwanini watu wanaohisiwa wanga au wachawi ni jamii ambazo ni "masikini,fukara" ??
HAKUNA MCHAWI FUKARA...NENDA MASAKI, KIGAMBONI NA BUNJU UONE WALIVYOPOROMOSHA MAHEKALU. WANGA NDIO MASKINI.

9.Je kuna wachawi/wanga matajiri ???
WAPO..NENDA KIGAMBONI, BUNJU NA BAGAMOYO

10. Inakuwajekuwaje hadi wachawi/wanga wanafanya mambo yao bila kuonekana ktk hali ya kawaida hadi ufanyiwe uganga ???
WANAONEKANA. NI KAMA VILE HUWEZI KUMUONA YESU MOYONI MWAKO KAMA HUJAAMUA KUMUONA AU KUMKIRI.

11.Kwanini magonjwa ya kulogwa wanasema hayaonekani ktk vipimo vya hospitali ??
ELIMU DUNIA NA ELIMU YA KIROHO NI MBALIMBALI.

12.Ufanye nini ili usilogwe/usiwangiwe ktk maisha yako yote .......... ??
USIWE MCHEPUKO..BAKI NIA KUU...KAMA NI MUNGU IWE KWA MUNGU KWELI...KAMA NI UDHALIMU IWE UDHARIMU KWELI. UKIWA KATIKATI NDIO HATA BIBLIA IKASEMA UNAWEZA KUKAPIKWA/KUKATALIWA NA MUNGU NA SHETANI...

13.Je ni kweli wachawi/wanga wanakula nyama za binadamu ........Kama ndio, kwanini hawali zile za wanyama poli/wakufugwa ??
WANGA NDIO WANA HIVYO VIMBWANGA...WACHAWI WANAKULA KUKU KWA MRIJA KULE BUNJU, BAGAMOYO NA KIGAMBINI

14.Kipi kitakufanya ujue kwamba hiyo sehemu unayopita/uliyokaa wanapita/wamekaa wachawi ??
UNLESS YOU ARE IN BUSINESS, NDIO UTAJUA. HIVI WEWE UKINIKUTA NAONGEA NA MTU UTAJUA BILA SISI KUKUSHIRIKISHA?

15. Ushahidi gani utawaeleza watu kuwa fulani anakuloga na ukaleta maana kwa watu unaowaelezea ??
KATIBA HAITAMBUI UCHAWI. MEANING HAKUNA USHAHIDI.

16.Kuna tofauti gani kati ya ugonjwa wa Hospitali na ugonjwa wa kulogwa ??
MATIBABU.
Hapo namba kuhusu Lucky Vincent ukiambiwa ulete uthibitisho utaweza?
 
Je mchawi/mwanga aliye mroga Mtu Yule mchawi/mwanga akifa itakuwaje Kwa aliyekuwa amerogwa na Marehemu mchawi/mwanga?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom