Maswali magumu kuhusu hotuba ya Mh Rais Magufuli UDSM

Mambo mengine ukiyafikiria yatakupa shida-senior minister for how many years? Ndo sasa anagundua na kuamini kuwa vyuo vinne vinatosha? Halafu mtu anasema Mzee kasema basi fungeni mjadala!!!!!!!!!! Matamko tata yanaendelea.
Mkuu wenzetu wa nchi jirani hua wanasema kua taifa letu tumejawa na vijana waoga,wanafki, wavivu, waongo na hawajiamini. Ukiona mtu anasema tufunge mjadala mtu flani keshasema inatosha muogope sana. Sasa msipolijadili jambo mtalitalipokeaje?
 
Wee umefikiri na kuja na Mawazo yaliyokwisha Muda wake ( expiry). Elimu pia inaendeshwa kwa Soko Huria vyuo visivyokidhi viwango vitakufa vyenyewe kutokana na ubora wa huduma zake haihitajiki Tangazo la Rais kuviua, huko tulishatoka kwny Urasimu huo wa ku admit Wanafunzi 25 tu kusomea MD Muhimbili au Computer science wakati Serikal inalipa Ma Prof Mamilion kwa Mwaka. Enzi hizo za urasimu na dhulma za kielimu hazirudi Watoto walifelishwa Muhimbili eti hawana akili lakin wanaenda India kuanza Upya kusoma na kurudi Muhimbili kuwa Madaktari Bingwa!

Tuache Vyuo vishindane pengine kwny ushindani huu vitakavyopotea ni hivyo vyuo vya Serikal.

Upuuzi wa kusomesha Wachache ili wawe na Elimu bora badala ya Wengi Wenye Elimu isiyobora alishajaribu Nyerere na ndio ilifikisha Taifa hapa. Acheni watu wapambane Kama imeshindikana kukopesha Wanafunzi isemwe wazi tu badala ya kupita Denge kwenda kufunga Vyuo!

Tukifunga Vyuo kukwepa Gharama tujiandae kwa gharama ya kudhibiti Vyuo vya Panya Road vitakavyoibuka kwa kasi kubwa sana!
Big up mkuu! Hivi ndivyo tunavyotakiwa kuvijadili.
 
Huwa mnasubiri Rais aongee mpate kufinyanga maneno
Usichoelewa hapo ni nini?
Rais kasema badala ya kua na utitiri wa vyuo vya hadhi ya chini ni bora tuwe na vyuo vinne vya hali ya juu,tatizo lipo wapi hapo?
Katafute cheti cha form four cha mbowe ukileta nakupa laki fasta

khaaa. sasa mbowe anahusika nini tena hapo?? i think hata usiku huwa unamuota eh
 
Jana Wanafunzi wa UDSM walimuelewa sana Mh. Kiongozi!Hakuna alieguna wala Kuzomea Kama Enzi zile za JK akiongea wanazomea 'Booooom'. Kweli awamu ya Tano nidhamu imetamalaki na kushika hatamu Kama Enzi za Baba w Taifa!
Hotuba ya Mh. Kiongozi illuwa ikipokelewa kwa Makofi toka kwa Wanafunzi
Kwanini unaandika kama vile ni wewe peke yako uliyekuwepo, au uliyeona kupitia tv? Wakati mwingine ni vizuri kukaa kimya tu!
 
Jana akiwa UDSM Mh Rais aligusia mambo mengi sana likiwemo suala mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na ukaguzi wa ubora wa vyuo vikuu nchini. je, juu ya haya ninyi mmemuekewa vipi wakuu?

1. Kwenye bajeti zimetengwa zaidi. billion 400, lakini zilizotoka ni billion 80 tu.Though hii ni kwa first batch, lakini tangu bajeti ipitishwe na mbaya zaidi vyuo vimeshafunguliwa na kuna wanafunzi wanaoendelea na masomo achilia mbali wadahiliwa wapya, hivi hatuoni kua mambo ni yale yale kama ilivyokya vya serikali za nyuma? Bajeti kubwa pesa inatoka kidogo.

2.Tunavyozungumza tu hapa wenzetu wa Kenya na Uganda na hata Afrika kusini wana vyuo vikuu zaidi ya 100, kielimu wanatuzidi,kimaarifa wanatuzidi na hata kiuchumi wanatuzidi pia. Sasa tunaposema tubaki angalao na vyuo vikuu 4 tu bora kuliko kua na utitiri wa vyuo ili tuwe na wakufunzi/walimu wa kutosha tuko sawa kweli? Hii sio kauli ya kisiasa hii? Kwani tukiwa na vyuo vikuu hata 100 Lakini vikawa bora tatizo nini? Kwani si kuna sheria ya kufuata ili mtu au taasisi inapotaka kuanzisha chuo kikuu? Je mtu akikidhi utamzuia kwa sababu hakuna lecturers wa kutosha?

Kufanya kitui bora ni process. Yapasa kuwa na raslimali za kutosha ili kuweka ubora. Unajua waliosoma hapo chuoni miaka ya 1990's na mwanzoni elimu ilikuwaje? hii ya kufungua vyuo bila kuwa na rasilimali watu na mali ndio imefikisha kuzaraulika kwa elimu yetu. wangapi wanasoma sasa na wanatoka watupu? Idea yake yaweza kuwa nzuri kwa maendeleo ya elimu yetu. waingie wachache wapewe elimu na mahitaji ya kutosha. wasioweza kucompete wawahi sehemu zingine
 
Jana akiwa UDSM Mh Rais aligusia mambo mengi sana likiwemo suala mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na ukaguzi wa ubora wa vyuo vikuu nchini. je, juu ya haya ninyi mmemuekewa vipi wakuu?

1. Kwenye bajeti zimetengwa zaidi. billion 400, lakini zilizotoka ni billion 80 tu.Though hii ni kwa first batch, lakini tangu bajeti ipitishwe na mbaya zaidi vyuo vimeshafunguliwa na kuna wanafunzi wanaoendelea na masomo achilia mbali wadahiliwa wapya, hivi hatuoni kua mambo ni yale yale kama ilivyokya vya serikali za nyuma? Bajeti kubwa pesa inatoka kidogo.

2.Tunavyozungumza tu hapa wenzetu wa Kenya na Uganda na hata Afrika kusini wana vyuo vikuu zaidi ya 100, kielimu wanatuzidi,kimaarifa wanatuzidi na hata kiuchumi wanatuzidi pia. Sasa tunaposema tubaki angalao na vyuo vikuu 4 tu bora kuliko kua na utitiri wa vyuo ili tuwe na wakufunzi/walimu wa kutosha tuko sawa kweli? Hii sio kauli ya kisiasa hii? Kwani tukiwa na vyuo vikuu hata 100 Lakini vikawa bora tatizo nini? Kwani si kuna sheria ya kufuata ili mtu au taasisi inapotaka kuanzisha chuo kikuu? Je mtu akikidhi utamzuia kwa sababu hakuna lecturers wa kutosha?

Mambo madogo unashindwa kuelewa,pole sna nyie ndo mnarudisha nyuma tanzania...boea ukae na ujinga wako..kukuelezea wewe ni kupoteza muda
 
Ukweli nakubaliana na swala la kukagua ubora wa vyuo. Natambua huwezi elewa maumivu anayopata mtu na familia yake pale anaposoma kwenye chuo cha kisicho na hadhi then anaenda kuomba kazi anakosa kwa sababu tu ya chuo alichotoka. Kuna vyuo vinatoa degrees ila wanao-graduate hawa-qualify kuitwa degree holders. Bora akague ili vyuo vyetu viweze kupambana na vyuo vingine katika soko la ajira.
Kwanini nia hiyo nzuri isingeanzia kwa kuangalia wale ambao rais amewateua wamesoma katika vyuo gani? Kuna haja ya kutafakari kwa upana zaidi masuala yanayoibuka kwenye majukwaa ambayo yanatumika kwa mambo yote, ikiwemo kisiasa!
 
Ukipunguza idadi ya vyuo vikuuu ni lazima utapunguza udahili wa wanafunzi kuingia Vyuo vikuu. Na ukipunguza udahili utakua umepunguza gharama kama za mikopo.
Kwahiyo Rais anataka kupunguza vyuo ili wanafunzi watakao pata mikopo wawe wachache.
Mmejiuliza ni kwanini waliongeza vigezo vya kuingia chuo kikuu? Anataka kuwe na wanafunzi wachache.
 
Badala ya kujenga msingi bora kwenye elimu ya Msingi na Sekondari anahangaika na vyuo vikuu ambavyo vioo kisheria na vinakaguliwa mara kwa mara.

Atatue swala la watoto kumaliza darasa la saba bila kujua KKK - Kusoma Kuandika na Kuhesabu.
 
Jana Wanafunzi wa UDSM walimuelewa sana Mh. Kiongozi!Hakuna alieguna wala Kuzomea Kama Enzi zile za JK akiongea wanazomea 'Booooom'. Kweli awamu ya Tano nidhamu imetamalaki na kushika hatamu Kama Enzi za Baba w Taifa!
Hotuba ya Mh. Kiongozi illuwa ikipokelewa kwa Makofi toka kwa Wanafunzi
Wanafunzi wangapi walihudhuria....wewe ulikuwepo jana acha kuandika tu ilimradi tu
 
Jana akiwa UDSM Mh Rais aligusia mambo mengi sana likiwemo suala mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na ukaguzi wa ubora wa vyuo vikuu nchini. je, juu ya haya ninyi mmemuekewa vipi wakuu?

1. Kwenye bajeti zimetengwa zaidi. billion 400, lakini zilizotoka ni billion 80 tu.Though hii ni kwa first batch, lakini tangu bajeti ipitishwe na mbaya zaidi vyuo vimeshafunguliwa na kuna wanafunzi wanaoendelea na masomo achilia mbali wadahiliwa wapya, hivi hatuoni kua mambo ni yale yale kama ilivyokya vya serikali za nyuma? Bajeti kubwa pesa inatoka kidogo.

2.Tunavyozungumza tu hapa wenzetu wa Kenya na Uganda na hata Afrika kusini wana vyuo vikuu zaidi ya 100, kielimu wanatuzidi,kimaarifa wanatuzidi na hata kiuchumi wanatuzidi pia. Sasa tunaposema tubaki angalao na vyuo vikuu 4 tu bora kuliko kua na utitiri wa vyuo ili tuwe na wakufunzi/walimu wa kutosha tuko sawa kweli? Hii sio kauli ya kisiasa hii? Kwani tukiwa na vyuo vikuu hata 100 Lakini vikawa bora tatizo nini? Kwani si kuna sheria ya kufuata ili mtu au taasisi inapotaka kuanzisha chuo kikuu? Je mtu akikidhi utamzuia kwa sababu hakuna lecturers wa kutosha?
Hahahaa eti Uganda kiuchumi wanatuzidi. Hata Kenya sio tishio kwetu. Uchumi wetu unakuwa vizuri na takwimu zinaonesha tuko 2 kwa uchumi kukua vizuri barani Afrika.
 
Ukipunguza idadi ya vyuo vikuuu ni lazima utapunguza udahili wa wanafunzi kuingia Vyuo vikuu. Na ukipunguza udahili utakua umepunguza gharama kama za mikopo.
Kwahiyo Rais anataka kupunguza vyuo ili wanafunzi watakao pata mikopo wawe wachache.
Mmejiuliza ni kwanini waliongeza vigezo vya kuingia chuo kikuu? Anataka kuwe na wanafunzi wachache.
Kaka sikiliza hotuba vizuri uelewe. Ni bora kuwa na vyuo vinne vinavyotoa elimu bora kuliko kuwa na utitiri wa vyuo ambavyo ubora wake ni shida. Halafu piga mahesabu tuna jumla ya wanafunzi wangapi vyuoni na hivyo vyuo viko full utilized ama underutilized. Implication ya underutilization ni nini halafu uonaongeza vyuo vikuu ambavyo wanafunzi waliopo hawatoshelezi.
 
Mambo madogo unashindwa kuelewa,pole sna nyie ndo mnarudisha nyuma tanzania...boea ukae na ujinga wako..kukuelezea wewe ni kupoteza muda
Mm na wewe na mjinga zaidi?badala kujibu swali wewe unaonesha UPu.m.bavu wako.siwezi kujibishana.
 
Hahahaa eti Uganda kiuchumi wanatuzidi. Hata Kenya sio tishio kwetu. Uchumi wetu unakuwa vizuri na takwimu zinaonesha tuko 2 kwa uchumi kukua vizuri barani Afrika.
Kwa mujibu wa takwimu za TWAWEZA ni sawa.
 
Kama hakuna lectures wa kutosha unategemea nini kwenye chuo kikuu,wanafunzi wameenda pale kutalii au kujifunza na kufunzwa?
Hivi mko serious na mnachokomenti au mnatania... yani projection zenu zipo anti-clockwise... Hivi 2025 tutakua na idadi gani ya wahitaji wa Elimu ya juu.. yani vyuo vipungue tena???

this is ONLY IN TANZANIA..
 
Kaka sikiliza hotuba vizuri uelewe. Ni bora kuwa na vyuo vinne vinavyotoa elimu bora kuliko kuwa na utitiri wa vyuo ambavyo ubora wake ni shida. Halafu piga mahesabu tuna jumla ya wanafunzi wangapi vyuoni na hivyo vyuo viko full utilized ama underutilized. Implication ya underutilization ni nini halafu uonaongeza vyuo vikuu ambavyo wanafunzi waliopo hawatoshelezi.

Kwani amna sheria ya kuvibana hivyo vyuo kutoa elimu bora? Serikali wenyewe ndio wamewaendekeza kwa kupokea rushwa.
Idadi ya wanafunzi ni kubwa sana,mwaka huu wanafunzi wengi wamekosa vyuo ata kama una vigezo. Mpaka sasa wako wengine awajui wafanye nini kwasababu amna nafasi ya kuingia chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom