Maswali magumu kuhusu dowans

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Nashukuru nimesoma nakala ya hukumu ya mahakama ya kimataifa kuhusu suala la DOWANS vs TANESCO.
Hadi sasa nipo katika kipengere cha 337 lakini nimeshangazwa namna nchi yetu ilivyoharibika halafu kwa ujasiri wa ajabu Rais Kikwete anasema hawajui wamiliki wa Dowans.
Kuna mambo wakati mwingine unatakiwa kuwa na kiburi cha uhalisi siyo kiburi cha kuigiza.
Na majuzi Rais Kikwete aliwahutubia wanachama wa CCM pale Dodoma akikana kuhusika na DOWANS. Kivipi? Nani ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri linaloidhinisha mikataba ya serikali?
Ni kwanini kikwete akiwa mwenyekiti wa baraza hilo aliruhusu tenda iliyotolewa na tanesco izidi siku 45 kama inavyoagiza sheria za manunuzi? Hakujua kuna ukiukwaji hapo? Sasa hahusiki kivipi? Au anadhani kuhusika mpaka upate kigawo cha kujichana,kujirusha,kuchizika,kuwa mjanja na kunywa bambucha?
Kwanini Kikwete aliwaambia wanachama wa CCM kwamba hahusiki wakati anajua wazi kuwa hilo siyo suala la chama chake bali suala la nchi. Hapa sitaki kujua kama anahusika kama mtu binafsi au la.
Nataka kujua upevu wake wa akili kujua kuwa hili ni suala la chama na hili siyo la chama. Ni kwanini aliwaambia watu kuwa hajui wamiliki wa Dowans wakati waziri wake aliyemteua alitutajia wamiliki (ambao ni wakurugenzi, lakini siyo lazima wawe wamiliki), ina maana taarifa za waziri Ngeleja zilikuwa ni uwongo?
Na kama hahusiki akiwa rais inamaana Kikwete siyo kiongozi wa Tanzania? Anawajibika vipi kutetea maslahi ya nchi katika muktadha huu? Au hajui yeye ni nani?
Na kama haitoshi tumeligeuza suala la Dowans kuwa siasa badala ya kuangalia maangamizi ya wananchi wanaoteseka kila siku.
Nafikiri kuna haja ya kuamini kuwa Edward lowassa hakustahikl kujiuzulu ili tungelijua kinachoendelea, kwani alieleza siku ile “tukianza hivi hakuna atakayepona hapa bungeni”. Nini kipo nyuma ya kauli?
MASWALI MAGUMU KUHUSU DOWANS.
1.Katika kipengere cha 157 majaji wanamtaja Rostam Aziz kuwa mtu anayehusika na suala zima. Na hakuna mahali ambapo imeshangaza kuliona suala la mtu binafsi kuhusu mkataba na serikali halafu serikali hiyo ikashinikiza wataalamu wanaokagua mkataba huo waupitishe, kwanini? Kwanini RA mwanzoni alikataa na sasa anakubali?
2.Dowans Holdint SA iliiandikia Tanesco kwamba ili kurahisisha utendaji kazi wa kampuni hiyo katika mkataba wake na tanesco wanalazimika kuanzisha kampuni tanzu Tanzania.
Hii inamaana baada ya kuona kuna umuhimu wa kuendesha ufuaji wa umeme ukiwa na utendaji wa kila siku.
Ni kwanini kampuni hiyo tanzu(dowans Tanzania Limited) iliuziwa vifaa na kampuni mama ya Dowans Holding SA? Inawezekanaje kampuni mama kuiuzia kampuni yake tanzu vifaa ili ifanye kazi ya ufuaji wa umeme?
3. ilikuwaje Dowans Tanzania kupewa mamlka ya kuendesha mkataba wakati haikuingia mkataba na tanesco? Na kama haitoshi ilikuwaje sito bwana Surtees alisaini nyaraka za mkataba bila upande wa tanesco kuwepo?
4. nini kilichojificha kwa balozi Kazaura? Ni kwanini wizara ya nishati na madini ilikuwa ikishinikiza sana tanesco kuingia mkataba na dowans ambayo imerithi kutoka Richmond?
Kulikuwa na ulazima gani kwa wataalamu wa tanesco kushikizwa kuingia mkataba wakati wao walikuwa na mamlka kisheria kuichagua kampuni inayofaa?
5. kama kikwete anakataa hahusiki na dowans, ni kwanini wizara yake aliyoteua yeye mwenywe, na kwa mamlaka kisheria iliamua kuingilia mamlaka ya tanesco? Sasa atasema hahusiki kivipi wakati utawala wake ndiyo umeiingiza dowans?
6.Rex attorney walikula rushwa?
7.ilikuwaje wakaishauri tanesco mkataba ulikuwa batili halafu mua huohuo wakaiambia tanesco hiyohiyo ilipe deni la dowans kwamba hakuna jinsi?
8. elimu waliyopata Rex attorney ilikuwa ni kuwatapeli watanzania? Kama siyo matapeli hawaoni kuwa ushauri wao butu, na wakijinga, tena usiozingiatia weledi wa kisheria ndiyo umeiingiza tanesco katika janga?
9.pesa walizolipwa Rex attorney kwa kazi ya kuishauri tanesco zilifanya kazi gani ikiwa wameiingiza tanesco katika janga ambalo, na ambalo pengine tunaweza kusema walipanga njama?
10. nani anajua mikakati ya kundi la Kikwete walipojiandaa kuitwaa Tanzania tangu mwaka 1995? Walitumia pesa kiasi gani kujipanga toka mwaka 1995 hadi 2005? Nani alikuwa mtoa pesa, na alizitoa wapi? Na kwanini aliamua kuzitoa kuhakikisha wanaitawala Tanzania?
11.gharama zao za kujipanga tangu mkwaka 1995 hadi 2005 watazirudisha lini? Je kwa kuingia mkataba na tanesco kupitia dowans? Je tutakosea ukusema sasa wanarejesha gharama za maandalizi tangu mwaka 1995?
Naishia hapo ingawa nina usongo wa kuuliza maswali zaidi ya mia moja. Ukisoma hukumu ya ICC kuna maswali zaidi ya elfu moja yatokanayo na mkataba wa kipumbavu,ujinga,upuuzi,watawala wabovu wasio na maono.
Hukumu inadhihirisha Tanzania imeoza na imekumbatia uozo kila ngazi. Hukumu inaonyesha wazi kuwa Tanzania tumejaa wajinga(nikiwemo mimi mwenywe kwa pengine nimeuliza ujinga).
Rushwa inanuka, vitisho vimeshamiri na wataalamu wetu wanaroho za plastiki, hawajiamini na hawaamini lolote katika utaalamu wao. unaambiwa kama umeingiliwa katika kazi yako kitaalamu basi ng’atuka(ikiwemo udhaifu wa Mama Wandiba katika suala la dowans).
Nchi inanuka, tumewapa mwanya wapumbavu kuonekana werevu? Steve Bantu Bicco, alisema, “I write what I like”. Watakaokerwa wanisamehe tu kwani nchi inapasuka msamba kutokana na ujinga wetu wenyewe.

 
jibu moja kwa maswali magumu yote hapo juu'; the dowans deal wasn't there to serve any one but the greedy corporates and corrupt politicians! Ni ka kundi kadogo cha watu waliojipangia deal tamu
 
Back
Top Bottom