Kabla cjawajibu maswali yenu naomba niwaulize kwanza-
....Tukiunda serikali ya 3 ya Muungano haitakuwa na gharama zake? Hizo ghrama zake ni nani atazihudumia? Na Je, bunge la serikali hii litakuwa na wajumbe wangapi, kutoka wapi na majimbo gani? Mishahara na posho zao zitagharamiwa na nani, watumishi wake watakuwa sehemu zote za Jamhuri au makao makuu tu na kadhalika… Hizi gharama za misafara ya rais ktk mialiko ya Kimataifa, mawaziri wake, mamlaka yake katika mipango ya maendeleo na kadhalika ndiyo maswala muhimu ya kujadili kuliko kuendelea kuidai Tanganyika ambayo ipo.
Je, nchi za wenzetu walokuwa na mfumo kama huu mamlaka ya uendeshaji wa shughuli za serikali zake umejengwa vipi na nini nafasi ya serikali kuu ktk ujenzi wa Mataifa hayo. Nini ukomo wa mamlaka ya serikali za nchi kuendea mamlaka ya serikali kuu juu ya jambo hilo hilo. Ikiwa Nchi inahitaji uwekezaji katika Kilimo, serikali kuu itahusika vipi tofauti na hizo za kila nchi.?