Makonyeza
Member
- Feb 2, 2020
- 69
- 252
*Hivi umeshawahi kushuhudia CAF wakijishughulisha na mashindano ya Kagame Cup, jibu ni hapana, na sababu ni moja tu, kwamba CAF kama baba wa Mpira Afrika hawayatambui mashindano hayo.
*Hivi kwani matamasha ya Simba Day na Mwananchi Day yanatambulika na Tff?, jibu ni hapana, na sababu ni kwamba ni matamasha yasiyo rasmi(bonanza) na hayapo katika Kalenda ya Tff. Na zaidi hayahusiki wala kuwajibika kwa kanuni wala katiba ya Tff.
*Hivi, hukumu ya Tff kwa Manara haina ukomo, jibu ni inao ukomo na ndio sababu hata mwenyekiti wa hiyo kamati ya maadili alisikika akieleza kwamba kifunho cha Manara hakitohusisha mitandao yake ya kijamii(kwa sababu ni mambo yake binafsi).
*Kwani kuuzungumza na kuujadili Mpira kwa kutumia mitandao ya kijamii sio kujishughulisha na Mpira?? Jibu ni hapana, huko pia ni kujishughulisha tena kwenye athari zaidi kwa sababu jambo lolote kupitia mitandao hufika mbali na kwa haraka zaidi. Hata taarifa za Tff wenyewe asilimia tisini tunazipata kupitia mitandao ya kijamii.
Sasa Kumfungia Manara kutojishuguulisha na soka isipokuwa kwa mitandao yake ya kijamii hii ni FUTUHI kama futuhi zingine tu.
Kama ni vile kusema eti hatakiwi kujishughulisha na shughuli yoyote inayohusiana na Soka, swali Je, hivi Tff wangemshtaki Manara hata kama wangemkuta anapiga Dana Dana au akicheza au kushiriki Ndondo Cup kwa namna yoyote, jibu ni kwamba wasingeshughulika naye kwa sababu Tff huko mkono wao kimamlaka haufiki kwa maana hawatambui shughuli hizo kisheria wala kikanuni.
SASA Basi, kwa Tff kuendelea kuendelea kujishughulisha na mambo ambayo kikanuni, kisheria na kimamlaka hakiwahusu ni kuthibitisha kwamba inawezekana tafsiri za kanuni zao wenyewe inawashinda na Sasa wanalazimika kutumia mabavu tu, na ushahidi wa hili ni ile tamko lililotolewa na yule mwenyekiti wa kamati ya maadili kwamba eti Manara haruhusiwi kujishughulisha na Mpira ndani na hata NJE YA NCHI.
Kwangu hii ilimaanisha TFF wanahukumu kwa kutumia sheria na kanuni wasizozijua.
Kwa hili sicheki bali ninasikitika!
Jadili changa, matusi sitaki!