Maswali kuhusu kura ya mapema Zanzibar

Maswali kuhusu kura ya mapema Zanzibar

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,255
Reaction score
16,185
Zanzibar Wanapiga kura ya mapema kwa watu maalumu na kura ya watu wote siku ya pili.

Maswali kwa ZEC

1. Tume itabandika majina ya watu hao maalumu wanaotakiwa kupiga kura ya mapema kwenye vituo. Je, tume itayajuaje majina ya watu maalumu hadi iyabandike vituoni?

2. Kama tume inayafahamu majina yote ya watu maalumu je usiri katika kupiga kura utahakikishwa vipi? Maana Ni rahisi kufahamu watu maalumu wamepigaje kura zao Kama kura zao zitahesabiwa siku hiyohiyo.

3. Je, waliopiga kura ya mapema watazuiwaje kupiga kura Tena siku ya pili Zanzibar au Bara. Yaani kupiga Mara mbili kwenye uchaguzi.

4. Dhamira kuu ya kupiga kura siku mbili Ni Nini? Mbona Tanganyika ambayo Ina wapiga kura wengi inapiga kura siku moja tu watu wote
?

Hii inanikumbusha uchaguzi wa kura tatu za wakoloni
 
Nkikumbuka ule mwaka wazanzibar/pemba wanakimbilia uhamishoni Mombasaaa ilikuwa taaabu.

Tuombe haki, amani na maridhianooo,

Jambo lolote laweza athiri biashara ya utali
 
ZEC/NEC ndio wa kulaumiwa kwa kusababisha Vurugu na mauwaji ya Watu wasiokuwa na hatia.
 
Huu ni upuuzi mtupu na mbinu za kuiba kura,Zanzibar ni ndogo na inawatu wachache kuriko Dar,sasa kama Dar haipigi kura kwa siku mbili kwanini Zenj ipige kwa siku mbili,

Hata kama hao wanaopiga ni watu maalum na viongozi,TZ bara inawatu maalum na viongozi wengi kuliko Zenj,na haipigi kura kwa siku mbili.
Wizi mtupu
 
Ni mwendelezo wa dharau na hujuma dhidi ya koloni letu.
JK zama zile Maalim yupo serikalini ya umoja, wangetembeza dau kiasi kisha kura ya maoni Zbar ikawa sehemu mkoa wa Tz, tukaungana na ndugu zetu.
 
Huu ni upuuzi mtupu na mbinu za kuiba kura,Zanzibar ni ndogo na inawatu wachache kuriko Dar,sasa kama Dar haipigi kura kwa siku mbili kwanini Zenj ipige kwa siku mbili,
Hata kama hao wanaopiga ni watu maalum na viongozi,TZ bara inawatu maalum na viongozi wengi kuliko Zenj,na haipigi kura kwa siku mbili.
Wizi mtupu
Mbaya zaidi wanaopiga kura ya mapema wataenda tena siku ya pili kupiga kura ya wabunge na Rais wa muungano. Kwanini wasingepiga kura zote tarehe 28 badala ya kupoteza muda wao kwa siku mbili kupiga kura. Dhamira ni nini?
 
Je, watu hao ni wangapi
Je, wakifika wanaonyesha vitambulisho vya kazi zao, je, anonymity (usiri) kwa wapiga kura uko wapi? sio vizuri kujua watumishi wa serikali walipigaje kura zao. La sivyo kura zao zisihesabiwe peke yake zisubiri kuchanganywa na kura za siku ya pili.
 
Zanzibar Wanapiga kura ya mapema kwa watu maalumu na kura ya watu wote siku ya pili.

Maswali kwa ZEC
1. Tume itabandika majina ya watu hao maalumu wanaotakiwa kupiga kura ya mapema kwenye vituo. Je, tume itayajuaje majina ya watu maalumu hadi iyabandike vituoni?

2. Kama tume inayafahamu majina yote ya watu maalumu je usiri katika kupiga kura utahakikishwa vipi? Maana Ni rahisi kufahamu watu maalumu wamepigaje kura zao Kama kura zao zitahesabiwa siku hiyohiyo.

3. Je, waliopiga kura ya mapema watazuiwaje kupiga kura Tena siku ya pili Zanzibar au Bara. Yaani kupiga Mara mbili kwenye uchaguzi.

4. Dhamira kuu ya kupiga kura siku mbili Ni Nini? Mbona Tanganyika ambayo Ina wapiga kura wengi inapiga kura siku moja tu watu wote
?

Hii inanikumbusha uchaguzi wa kura tatu za wakoloni
Namba tatu ndio mpango mzima uliobeba dhamira ya kupiga kura siku mbili
 
Back
Top Bottom