Maswali 21 kwa Zitto Kabwe

Niliwahi kusema miaka kama 7 hivi nyuma...kuwa Zitto sijawahi kumuona mtu wa maana!!
 
Huwezi kupata majibu sahihi juu ya maswali yako. cha msing uwe mstahimilivu wa matusi na utegemee majibu mepesi au maswali zaidi. Ni jicho la tatu tu linaweza kuona na wengi wa watanzania jicho la tatu halifanyi kazi tena.
 
Na ninyi muulizeni babu Slaa kwa nini mpaka sasa miaka 90 ana girfriend badala ya mke?
 

Maswali ya kitoto sana.Ingawa yameshajibiwa mara nyingi tu hapa hapa JF. Leteni mijadala mingine sasa tuneshachoka na thread zenu za kumlilia Zitto.
 
ZZK alisema hiyo pesa ya kiinua mgongo haitaki, pia katika hao MP 50 watakao kuja kujiunga ACT kutoka CDM na CCM ndio wanaomfadhili ACT, kama in kweli je haoni hao hoa wabunge hizo pesa ni sehemu ya zile alizozikataa?, sasa wewe umekata a posho wenzako wanapokea na ndio michango hapo ACT, does it make sense?
 
Maswali yako ni mazuri sana na ya msingi kabisa.

Mimi ni miongoni mwa neutral katika siasa za kitanzania haswa kwa sababu ni za kizandiki na sio "open politics". Na sasa naweza kusema, kama zitto ni kibaraka wa ccm, basi chadema pia yweza kuwa ni kibaraka.

1. Iliundwa na mtei na bado ni mlezi, aliyekuwa katika serikali ya ccm hadi uwaziri wa wizara nyeti kama fedha
2. Unaongozwa na mbowe, ambaye hata baba yake sijukama bado ni ccm, lakini ni miongoni walio kuwa wafadhili wazuri wa chama hicho.
3. Kwa taarifa nilio isoma jana mtandaoni hapa, chadema walijua mipango yote ya zitto, ikiwa ni pamoja na kuundwa act, kama plan b baada ya awali kushindwa. Jibu lilikuwa ni kumnyanganya zitto uongozi na kutomfukuza uanachama na kuona kama bado angeondoka. Chadema imefanya hivyo ikijua alisha unda chama kwa ufadhili wa ccm ili kudhoofisha upinzani na haswa ukawa.lakini cha kushangaza bado wamemfukuza zitto ili kutimiza azma hiyo!!

Pamoja na haya yote maswali ya hapo juu ni ya msingi sana tuyajibu na yakijibika pasipo na shaka, hata mimi kwa maa ya kwanza kabisa nitaanza siasa na kujiunga na act na hasa nikijiaminisha haina mahusiano na ccm
 
Zitto kawashika pabaya Chadema, Habari za Chadema watanzania hawazitaki tena, Macho na masikio ya watanzania ni kwa Zitto na ACT
Naam Sheikh naona ushafika tayari eneo la tukio, karibu sana hatutegemei jibu jioya toka kwako.
MANI
 
Last edited by a moderator:
Kama siasa ni kipaji basi Zitto ana kipaji cha ajabu sana...huyu jamaa hatari sana asee..anajua hatashinda uraisi kwa sasa...CCM ndo wana shida na uraisi wanampa msaada ili kudhoofisha ukawa but yeye anajua anachofanya baada ya uchaguzi ACT itakuwa imesikika Tanzania nzima..af atawageuzia kbao CCM kuelekea 2020...!!! Zitto ni mwanasiasa pekee Tanzania anayejua kujenga hoja,kuitetea na kuwashawishi watu wa tabaka lolote....hata kama unamchukia huyu jamaa ukikutana na hoja zake utashawishika kumsikiliza....
 


Taifa likiwa na wajinga wengi utaona mengi ndo kama hayo unayoyaona sasa kaka
 
Huu ni udhaifu sana wa kisiasa

Toka Zitto ahame chadema amekuwa mtu wa kuandamwa kila kukicha na kusemwa kwa ubaya mno.
Inaonyesha huyu mtu alikuwa ni muhimu sana katika chama na kama hakuwa muhimu kwanini anasakamwa sana na wanachama wa chadema!

Zitto usirudi nyuma katika kuleta Mabadiliko ya kweli....
 
MAJIBU
1.kwa sababu nabii hakubaliki nyumbani ambako ni chadema.
2.kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiipenda CCM muda mrefu kutokana na kutokuwepo vyama vya upinzani vyenye nia ya dhati ya kuing'oa CCM mdarakani bali yamekuwa magenge ya wezi wanaotawala milele kama waflme. sasa mwanga wanauona ACT-wazalendo tegemea watu makini kuikimbia CCM karibuni na kujiunga ACT-wazalendo.
3.kwa sababu vyombo vingine visivyompa upendeleo mzalendo ZITTO vinamilikiwa kama sio wachaga basi viongozi wa vyama vya upinzani alikotoka.
4. kwa sababu alikuwa hapangiwi ratiba za kufanya hivyo na chadema ila leo hii ACT-wazalendo wanampangia ratiba. huko ratiba
5.wafadhili
6.hatuongelei CCM tunajenga hoja za kuikomboa nchi, hatupambani na CCM wala UKAWA, acha ushamba, ACT-wazalendo haipo kusema vibaya vyama kama mlivyozoea kutukanana, ipo kujenga hoja zenye mashiko juu ya maisha ya watanzania.
7.kama enzi za nyerere vile kiongozi lazima aaminiwe na wenzake na jamii, leo hii macho ya watz yapo kwa ZITTO kuona anatuvushaje.
8.huu ni utambulisho na hatuna bajeti ya kutosha, lazima tupite nchi nzima then maswala unayotaka wanachama watamalizana na viongozi wa chama ngazi ya mkoa, hilo lisikupe hofu.
9. lakuambiwa changanya na zako, hatujawahi tukana Chadema bali kuikosoa, kama hampendi ukweli kwenu ni matusi tunawapa pole na kwa hilo mtatusamehe.
10. Kumbuka roho ya KABWE ni ya kizalendo kupita kiasi na kama unaishi porini habari ya mjini ZITTO katangaza kutochukua mafao, yakawasidie wanyonge. tayari alishaiandikia ofisi ya spika.
11.kumbuka TANZANIA DAIMA ni gazeti la mwenyekiti wa kudumu Mbowe, usipende sana kulisoma na kuamini siku utaabika mbele ya mama yako, kisa umesoma gazeti hili la kikanjanja.
12.wamegundua uozo uliopo chadema sasa wamejiunga na ukombozi wa mtanzania.
13.kwa bahati nzuri hakuna mtanzania hadi sasa anamimliki kitalu cha gesi, najua unapenda sana kusoma gazeti la TANZANIA DAIMA ndo matokeo yake haya.
14. ask serious questions.
15.refer answer no: 15 hatujibu porojo hapa na fact basi.
16.walijua utendaji wa ZITTO ndo maana umeona matokeo makubwa yalioangusha majoka yenye makengeza na werema wao.
17. ushasema Rais so sioni ajabu kuambatana na kiongozi yeyotea awe wa kisiasa , kidini au taasisi yeyote ile.
18. nadhani kilichowaondoa wale wezi ni ripoti ya PAC mwenyekiti akiwa ZITTO, ndo maana watu wanampenda kwamba ukimpa uongozi atawasaidiwa wasaidizi wake mpaka hatua ya mwisho, taifa linahitaji watu kama hawa, kumbuka hata Mwl.Nyerere hakufanya peke yake ila anakumbukwa kuliko wote wapigania uhuru kutokana na nafasi yake ya uongozi.
19. hana matatizo au uhusiano mbaya na wanachama wa chama chochote, ila tofauti unazoziona ni mitizamo juu ya mstakabali wa nchi hii, mkiendana mko pamoja ukikengeuka miiko ya nchi anakushughulikia, haijalishi upo CCM au UKAWA.
20.bado kijana hivyo kuwa na subira.
21.hatuna uadui na chama chochote, serikali wala taasis, so jifunzeni kwetu au karibu ujiunge na wazalendo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…