Maswali 11 kwa Baba Askofu Dallu

Kanisa hili limepitwa na wakati. Nashangaa npaka leo watu wanaenda kusali huko.
Shida ya mtu inakiaje ihusishe kanisa zima,kusema kanisa limepitwa na wakati ni kumkashifu KRISTO,ni sawa na kusema KRISTO kapitwa na wakati,
Tuache kuropoka,tuache kukurupuka,tuache chuki,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuuu hapa sasa unaenda mbali hebu jaribu kubaki kwenye hoja yako ya msingi ambayo umeiwasilisha vyema

Watakuja hapa wanao muamini Yesu ambaye ni..... Kama ulivyosema hapata kalika

Umetumia neno kali sana kumfananisha nalo Yesu
 
Duuuuu hapa sasa unaenda mbali hebu jaribu kubaki kwenye hoja yako ya msingi ambayo umeiwasilisha vyema. Watakuja hapa wanao muamini Yesu ambaye ni..... Kama ulivyosema hapata kalika.
Umetumia neno kali sana kumfananisha nalo Yesu
.
Neno hilo kali liko wapi?
Naona mouse yako iliokota text isiyo yangu.
Maneno yangu yote yako shwwari.
Hebu cheki tena uone....
 
Hivi bado unaamini kuna viongozi wa dini siku hizi?,kwasasa ni bora kuwategemea viongozi wa kijadi hawa wa dini ni wachumia tumbo. Kama hawa wakatoliki ndio majanga wanatenda tofauti na wanavyo hubiri, wako kibao wenye wake na watoto huku mitaani ili hali ni kunyume na amri za kanisa, wala siku hizi hawajadili au kukemea maswala ya ukiukwaji wa haki za viumbe vya mungu lakini macho yao ni kodo kwenye sadaka.
 
Tumsamehe Bure Baba Askofu Hajui Alitendalo Maana Ukitazama Vizuri Tunaye Baba Askofu Wa Escrow Wa Jimbo La Rulenge Ngara Tunangoja Kuona Hatua Atakazochukuliwa Hivi Punde
Ha ha ha maana nadhani kwenye maadili yao sidhani kama wanaruhusiwa kupokea mgao kama ule ....but hutasikia kuwa kafukuzwa upadri hata akimpa mtu mimba wala hutasikia kafukuzwa sana sana wataficha ficha wee
Kama nakumbuka 6yrs nyuma kuna.padri alikamatwa usiku mitaa ya chuo udsm akimlawiti mtoto wa kiume kwenye gari...yule mtoto akasema ni kawaida yule padri kumfanyia hvy..but kanisa iilipiga danadana weeee wakaipotezea
Ila kwa magu aah kila kitu twende
Sasa wewe kamuulize padri vipi ukandamizaji wa demokrasia na mtu kushikiliwa hadi siku 7 bila kupelekwa mahakamani kinyume na sheria za nchi...akikupa jibu lazina ukaee chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nashukuru ndugu kwa kunielewesha vizuri sana ndo mana nikataka kujua km kuna sheria ya shule sio ya nchi inayoruhusu mwanafunzi kujihusisha na ngono... Na vipi nasikia neno analotamka rais w nchi linatafsiriwa km ni sheria kamili lina ukweli swala hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Kwa ujumla, mfumo wa sheria una ngazi tano:
  1. Sheria asilia ya maadili
  2. Sheria za nchi/Bunge
  3. Matamko ya watawala.
Hivyo basi, vipaumbele vya utii viko hivi:
  1. Sheria asilia ya maadili ina nguvu kuliko Sheria za nchi
  2. Sheria za nchi/Bunge zina nguvu kuliko Matamko ya watawala
 
Wanaharakati wetu mara nyingi wanashangaza sana! Hivi sasa wanapambana mabinti waliopata mimba waruhusiwe kuendelea na masomo wakati huohuo wanapinga ndoa za utotoni! Sasa vipi kupata mimba nje ya ndoa iwe sawa na binti aonewe huruma na kuruhusiwa kurudi shule ilhali akiolewa iwe tabu?! Leo hii ukioa binti aliyemaliza shule ya msingi hivi karibuni na hakubahatika kuendelea na elimu ya sekondari jamii nzima inakugeukia lakini wale wanaowatandika hawa mabinti nje ya ndoa wanaonekana sawa tu! Wala huwezi kuwasikia wanaharakati wetu wakikemea vitendo vya ukahaba vinavyofanywa na mabinti wadogo kabisa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar. Kwao wao shida ni pale binti anapoolewa lakini anapozini hakuna shida. Tuache unafiki na huu ushetani.
 
Aisee...
Hivi hakuna mtu mwenye uwezo wa kujibu hoja kama hivi, ili amjibu Lissu.
For the first time naona mtu anajibu HOJA na anapinga kwa HOJA ndani ya JF.
Hakuna mihemko wala personal interests.
kula 5 mkuu.
 
Asante Mtumishi wa Mungu Baba Askofu Kazoba kwa kutokua mnafiki, wengi tulitegemea Baraza la Maaskofu Katoliki kutoa tamko la kujitenga na msimamo binafsi wa Askofu Dallu
 
Kanisa hili limepitwa na wakati. Nashangaa npaka leo watu wanaenda kusali huko.
We unaenda wapi mkuu...na hilo unaloenda lita expire lini...halafu utaenda lipi tena....

germve himself
 
aache unafiki mbona maaskofu, walikula hela ya escrow lakini kanisa limewasamehe???

maaskofu na mapadri wazinzi. kanisa limewasamehe waendelee na huduma

cha ajabu ni kipi? kumsamehe Binti aliyedungwa mimba na mizee kama Dallu
 
Mbaya zaidi hizo shule zilijengwa kwa sadaka za waumini masikini ambao uwezo wao hauruhusu kusomesha watoto wao kwenye hizo shule walizozijenga wenyewe.
Ukweli in za ghali yaani wanasoma wenye nazo tuu...ila uache uongo seminary nyingi zimejengwa na wafadhili sio waamini

germve himself
 
Mimi ningemuuliza swali moja tu huyo Askofu, aje hapa atuambie ni kwanini Maelfu ya Mapadri wanaowapa mimba waumini wao Kanisa Katoliki haliwafukuzi lakini linaendelea kuwalea?
Liwafukuze waende wapi...mchungaji au mwanandoa yeyote akimpa mimba mtu ambae sio mchumba au mke wake anafukiziwa wapi

germve himself
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…