MASWALI 10 ya papo kwa papo kwa Nape na wana CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MASWALI 10 ya papo kwa papo kwa Nape na wana CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dik, Feb 17, 2012.

 1. D

  Dik JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nashukuru sana kaka nape kwamba uko humu jf na unachangia.naomba unijibu maswali haya ili niweze kurudisha iman kwa ccm na kuendelea kuitaman tz
  1.ni kwa namna gani ccm haihusiani na ufisadi?
  2.kama siyo chama cha mafisadi mbona mafisadi wengi ni ccm?
  3.je ccm inastahili kuendelea kuaminiwa na wananchi?kwa muda wote hadi nchi ikafika hapa ccm haikuwepo?
  4.ccm inahusika vp na maisha magumu ya watz?
  5.ccm inaongozwa na viongozi wengi wasiokuwa na elimu ya kutosha mf kept.komba,w. Lukuvi,pr.majimarefu et al.ndo maana wanaiyumbisha tz hivi.unalionaje hili?
  6.nikisema ccm(serikali)inaongozwa na chdm nitakosea?ref.mchakato wa katiba mpya,ishu ya ufisadi
  7.viongozi wa ccm(serikali)hawako makini kiutendaji!ref kupishana kwa taarifa juu ya posho za wabunge(kashilila vs makinda,ikulu vs pinda et al),pinda kutoa order ya kuwafukuza madaktari hatimaye kufail etc.
  8.nyienyie ccm na mawaziri kutumia magari ya serikali kwenye shughuli za chama hamuoni kama kuhujumu uchumi?
  9.unaipenda ccm kutoka moyoni?malengo yako hayawezi kutimia ukiwa nje ya ccm?huoni kama unahujumiwa na kudumazwa akili ndani ya ccm?
  10.unanishauri kuwa mwanachama wa chama gan kat y ccm na chdm?
  11.ile taarifa kuhusiana na machinga complex iliysomwa kwa jk pale mwanza kweny madhmisho ya miaka 35 ya ccm ikitaarifu juu ya wamachinga kurudi ccm aliiandaa nani?hela zilizotumika kuwalipa wale jamaa walioandaa alizitoa nani?ni kwa nini unamdanganya hata mh.jk?je ile taarifa ni ya kweli?
  SAMAHANI KWA MASWALI MAREFU!NAJUA YATANIFANYA NIKUFAHAMU VYEMA NA KUONGEZA UELEWA WANGU JUU YA CCM.KAMA KUNA MWANA CCM ANAWEZA CHANGIA PIA
  NB:MOD P/SE USIIFUTE HII THREAD NA JAZBA ZIEPUKWE TOKA KWA WACHANGIAJI!
  Nitashukuru sana kwa majibu yako(yenu)
  0716689250
   
 2. H

  Honey K JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakubwa,
  Nipo na kwakweli natafuta muda ntajibu swali moja baada ya jingine... Mlioanza kwa kejeli nadhani mmekosea njia kuingia kwenye forum ya GREAT THINKERS
   
 3. H

  Honey K JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanza CCM kama chama cha siasa kinachoongozwa na binadamu ni lazima knamapungufu hakiwezi kuwa asilimia mia moja sahihi... Hili nalikiri na kwa mapungufu yeyote ya kibinadamu NAOMBA RADHI KWA NIABA YA CHAMA CHANGU
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mbona maswali yako yanafanana na yale mia moja yaliyoelekezwa kwa JK.... Ok kwa kuwa NAPE ameahidi kujibu, ngoja nisubiri.
   
 5. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Kaka Nape, nafurahi umekiri mapungufu. Hivi serikali inayoundwa na chama chako, utendaji wao unauzungumziaje? Mapungufu ni makubwa na kibaya kuliko hakuna uwajibishwaji.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,879
  Trophy Points: 280
  eti??
  umeomba radhi then?
  unajua kitu alichofanya rais wa ujerumani leo? aliomba radhi then aka step down...wewe unatuletea mazingaumbwe hapa Nape.
   
 7. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  HAya kweli mazingaumbwe, jamaa anakiri makosa na kuomba radhi, ingekuwa Ni mahakamani hapa Ni jela hadi ibomoke. But kaa ukielewa hawa ccm hawana utamaduni wa ku-step down, bila kushurutishwa hakuna atayeweza kuachia ngazi.....c unajua wako zaidi kwa personal interest. Mfano mzuri umeona sakata la madaktari.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kuna thred kule hoja mchanganyiko kuhusu kiongozi wa cdm kubaka,wana jf wanasema haipaswi kuchanganya makosa ya mtu na chama,mbona huku tofauti hakuna kwa nini???????

  me nadhani Nape kwa upeo wako hupaswi sana kuahirisha kutoa majibu sasa kwani time is money....na kitu ukikifanya kikiwa cha moto inapendeza.
   
 9. mamaWILLE

  mamaWILLE Senior Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  swali la nyongeza. Siku 90 ulizokuwa umewapa mafisadi watoke ndani ccm ina semekana ulitumwa na mwenyekiti wako hasa uwakikishe unamdhibiti lowasa. Je ni kweli
   
 10. W

  Wangama guy Senior Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Swali 11: Naomba kujua kama kuna kiapo kingine cha siri cha viongozi wote wa ccm (serikali) kwamba hata kama wakifanya makosa au kushindwa kutimiza wajibu wao kung`atuka kwenye nafasi zao ni MWIKO?
  12. ccm upo kwa ajili ya kutimiza majukum yako tu ili ufikiemalengo yako au unaipenda ccm kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote?
   
 11. chitulanghov

  chitulanghov Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tunakosea sana na hii sio sawa! tumeanza kushambulia hata hajajibi swali la pili tayari yameshakua maswali kumi na tatu! siamini kama nape atakaa tena tutaishia na hilo moja tu. tuache unazi bana!
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  swali la sita kuhusu katiba jamaa anapotosha umma kweli kweli.kwa hiyo kitendo cha rais kukubali kuongea na vyama pamoja na wadau mbalimbali kuhusu katiba ndio imekuwa ya chadema??????????

  hii ni kejeli na ni sifa za kijinga.tuwe firm ktk mambo ya msingi.

  sasa na wengine wakisema cdm walienda pale kunywa juice utasemaje
   
 13. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Nape anawasiliana na JK ili ampe majibu mujarab.
   
 14. A

  AMKA Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hata mimi nasubiria majibu NAPE pliz
   
 15. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape kaahidi kujibu swali moja baada ya jingine mi nadhani ni busara kuwa na subira ili kumtendea baki muulizaji nashangaa wengine wanaendelea kujaza
  swali juu ya maswali mtachanganya watu humu ndani waungwana tujifunze kutoshibia uji wa matanga kama wengine mko na maswali ni vyema mkayaandaa muulize baadae kuliko kuchanganyana humu.

  Halafu la pili katika majibi yake Nape kuna pahala kaomba radhi kwamba ni kweli Chama kina mapungufu yake anakiri hilo na kuomba radhi vile vile ila nimestaajabu jinsi watu walivyoreact as if kuomba radhi huko ni kosa kubwa sana lakini waungwana tukumbuke kuwa ni humu humu ndani tumekuwa tukitumia mfano wa Marehemu Regia jinsi alivyoomba radhi kwa kauli yake kwa wafugaji kule Kilombero na mmekuwa mkimpongeza kwa hatua yake hiyo sasa NINACHOSHANGAA ni jinsi anavyoshambuliwa Nape kwa mifano ya Rais wa Ujerumani!

  Its unfair bana yeye si Raisi tujitahidi kuwa realistic pale mtu anapoonesha ushirikiano manake ni kama vile si moto wala baridi
   
 16. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mtoa mada karuhusu mwachama yeyote kujibu hoja

  Ninachojua serikali yetu inafuta utawala wa sheria je sheria zinanyamaza kimya kwa mafisadi walio kwenye chama. Haya masuala ni makubwa siyo ya kuombana misamaha kirahisi namna hiyo ili isssue ziishe na tuasameheane kuna dhambi hata Mungu huwa hasamehi hata kidogo

  Suala la ufisadi si la bahati mbaya hata tukaombana misamaha kirahisi namna hii Mkuu angalia impact za ufisadi kwa jamii yetu hadi sasa
   
 17. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  huyu ni mwanasiasa haji tena hapa la msingi kaomba msamaha as if ufisadi ni suala dogo sana na serikali yake hawezi kutekeleza sheria
   
 18. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  HAKIKA. Ni vema tukasubiri ajibu maswli yote then tutauliza maswli mengine kulingana na atakavyjibu maswli ya msingi.Then matumizi ya lugha ya kistaarabu ni ya msing kwni ni ataweza kukata tamaa ya kujibu maswli kwa kudhani anajibu kundi la wahuni flani tu.....Tuvute subira
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ngoja nijaribu kumjibia:


  Jee, baba yako hajawahi kuwa CCM? kama amewahi, na yeye ni fisadi?

  Kwangu mimi hata mtu anaekwepa kulipa kodi ya Serikali ni fisadi, na hilo tulilisoma humu JF kuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa ametuhumiwa na TRA kuwa halipi kodi na (hajakanusha hilo). Ushahidi huu hapa:

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/140835-gazeti-mzalendo-tra-yamwita-dr-slaa-fisadi-halipi-kodi-5.html

  Kama uliipigia kura endelea kuwaamini, kama hujawapigia kura endelea kuto waamini. Tanzania ni nchi huru na inafata mfumo wa demokrasia, hulazimishwi kuiamini au kutoiamini CCM wala CHADEMA wala CUF wala NCCR wala chama kingine au mtu mwingine yeyote yule. Upo huru.

  Maisha magumu yako wapi Tanzania hii? unalinganisha na nchi ipi? Tanzania ni nchi inayokupa fursa ya kujiwekea maisha yako upendavyo, ukifanya kazi kwa bidii na kutumia fursa zilizopo hutayaona maisha kuwa ni magumu, lakini kama husomi kwa bidii, hufanyi kazi kwa bidii, hujitumi kwa bidii, basi katika dunia hakuna utapoishi ukayaona maisha si magumu. Jitume kwa bidii ili uepuke kuyaona maisha kuwa ni magumu.

  Hivi maisha ambayo unayataka wewe ni yepi? ya kukaa JF na kungoja kuletewa kila kitu? Au unataka ukisema "gari" limeshakuja, ukisema "fedha" zimeshajaa mifukoni?

  S.S, Bakhresa mmoja katika matajiri wa Tanzania, mpaka leo anajituma masaa 18 kwa siku mfululizo. Jee, wewe?


  Tuwekee CV zao. Tukuamini vipi bila ushahidi?

  Unakosea sana tena. Kutoa mawazo na ukasikilizwa na kiongozi hakuna maana wewe ndiye unaeongoza. Hivi nyumbani kwa wazee wako kiongozi ni wewe au baba au mama, yeyote katika hao, haruhusu wengine kuwa na mawazo? Isitoshe, swala la katiba mpya sio wa mwanzo chadema kuleta wazo hilo. Hiyo ilikuwa ni sera ya CUF toka ilipoanzishwa na walitengeneza mpaka mapendekezo ya katiba wanayoiona ni sahihi, chadema wamerukia hoja na hata hawajaandika katiba mbadala wanaona iwe vipi. Kuhusu katiba inabidi wapongezwe CUF kwa kuwa waasisi wa kudai katiba mpya.

  Usiseme uongo, Pinda hajatoa order ya kuwafukuza madaktari. Tulimsikia alichokisema Pinda usidanganye, tuwekee ushahidi ni wapi Pinda aliwafukuza madaktari?.

  Hiyo ndio "priority" ya kuwa viongozi wa Serikali.

  Anaedumazwa mawazo ni yule anae ambiwa utanyonya kesho na hiyo kesho haifiki. CCM ndio inaongoza kwa sasa inabidi ujaribu tena kupiga 2015 ili kuwapata ambao hawakudumazi kimawazo. Pole sana.

  Kuwa chadema. CCM hatutaki watu wenye mawazo duni kama yako.

   
 20. M

  Malolella JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamaa anachungulia mnavomsubiri kwa hamu. Atakuja kujibu pindi mkijisahau kama baada ya 1week hivi.
   
Loading...