Dubai Market
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 1,182
- 1,591
1.Jina la mkuu wa wilaya yako. (unapoombea)
Hapa utaulizwa swali hili kukupima na kukuangalia muombaji ni kweli unatoka wilaya husika ama la, inabidi mhusika umjue mkuu wa wilaya yako unapofanya usaili kwa jina ikiwezekana na sura kabisa. Kuna wengine huingilia kupitia mikoa na wilaya tofauti na maeneo ambayo wanaishi kwahiyo hapo mzingatie hili.
2.Jina la mkuu wa mkoa wako. (unapoombea)
Halikadhalika pia hapa wanaangalia weledi wako kama ilivyo katika swali la kwanza.
3.Kirefu cha JKT.
Utaelezea kwa kirefu maana ya JKT kwa kiswahili.
4.Kirefu cha neno JKT kwa kingereza.
Utaelezea kwa kirefu maana ya JKT lakini iwe kwa lugha ya kingereza.
5.Kazi ya JKT ni nini?
Hapa muombaji unatakiwa kutaja kazi angalau mbili au hata moja, usilogwe ukasema "kulinda nchi"
6.Taja jina la mkuu wa JKT.
Muombaji unatakiwa umjue mkuu wako wa sehemu unayotaka kwenda, itapendeza na kukuongezea point kama utataja kwa kuanzia na cheo chake na kufuatia jina kamili.
7.Taja jina la mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.
Hapa utajibu kama nilivyoeleza kwenye namba 6.
8.Taja jina la Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.
Utamtaja amiri jeshi tofautisha amiri jeshi na mkuu wa majeshi kwahiyo uwe makini kwenye kusikiliza swali.
9.Kazi ya amiri jeshi mkuu ni nini?
Utaeleza kazi zake kadri unavyozifahamu.
10.kwanini unataka kujiunga na JKT?
Utaeleza sababu za wewe kutaka kujiunga na jeshi lakini hapa epuka kutamka neno "ajira" yaani usije ukasema unataka kujiunga ili upate ajira weka kipaumbele neno "uzalendo na kujitolea"
N. B.
Maswali haya utakutana nayo kwenye ngazi ya mkoa au wilaya kumbuka kuna ngazi takribani nne;
i/mtaa
ii/kata
iii/wilaya
iv/mkoa
Na sio lazima uulizwe yote haya unaweza ukaulizwa moja kati ya haya au mawili akiingia mwengine pia hivyohivyo.
Usaili huu husimamiwa na mkuu wa mkoa/wilaya chini ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa/wilaya.
Kama ukibahatika kufikia hatua hii basi nakushauri uvae nguo nadhifu sio 'kisharobaro' yaani ikiwezekana vaa angalau kama Dr. Luis itapendeza. Halafu simama kwa kujiamini ukiwatazama 'usiangalie chini" jibu maswali kwa sauti kubwa na ya kinidhamu.
Kama hujui cha kujibu kaa kimya hapa unaweza kubadilishiwa swali, usijibu kitu usichokifahamu. Maswali ni mengi sana lakini hayo ni baadhi tu ambayo ni muhimu kuyafahamu.