Maswa:Kiongozi anayeingilia majukumu ya Walipafedha ni adui wa Maendeleo.

Maswa:Kiongozi anayeingilia majukumu ya Walipafedha ni adui wa Maendeleo.

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
130
Reaction score
118
Katika nchi inayohitaji maendeleo ya haraka kama Tanzania, kila sekunde ya ufanisi ni hazina, na kila senti ya umma ni dhamana ya kizazi kijacho.

Walipafedha wa taasisi za serikali wamewekwa kwa dhima ya kuhakikisha rasilimali hizi zinasimamiwa kwa weledi, kwa mujibu wa sheria.

Lakini leo, tunashuhudia jinamizi linalonyemelea mfumo huu katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu yupo Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Athuman Kalaghe amekuwa anapoka wazi wazi majukumu ya walipafedha hao kwa maslahi yake binafsi.

Katika taasisi hizo kiongozi huyo amekuwa anadiriki kuamuru apewe malipo yote ya posho za wajumbe na madereva pamoja na shughuli nyingine hususani katika ziara zinazoratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Badala ya walipapesa wa taasisi kutekeleza majukumu yao amekuwa akiyafanya yeye mwenyewe kujigeuza kufanya shughuli isiyo yake kabisa.

Athari zinazojitokeza kufuatia kadhia hiyo ni pamoja na baadhi ya walengwa kutopata stahiki zao kabisa,wengine huzipata zikiwa na upungufu,wengine hucheleweshwa kwa makusudi kupatiwa kwa kuzungushwa kwa maelezo hazijatoka kumbe tayari alishachukua na kufanyia mambo yake binafsi.

Hali hii imezua malalamiko mengi na suala hili limewafikia hata wakuu wa taasisi na wengi wao hawezi kumhoji wakiogopa ndiye Mkuu wa watumishi wa serikali katika wilaya hiyo hivyo kuiingiza hasara taasisi za serikali kufanya malipo mara mbili ili kuwalipa walengwa ambao hawakupata malipo yao licha ya kutoka na kukabidhiwa yeye.

Amekuwa akilazimisha kuomba pesa katika taasisi za serikali tena bila woga kwa kuandika barua matharani kuchangia ugeni wa kiongozi wa kitaifa wa serikali au chama tawala lakini sehemu ya fedha hizo anazitumia kwa maslahi yake binafsi jambo hili lipo na linalalamikiwa mara kwa mara lakini vyombo husika vimekaa kimya na mambo yamekuwa yakijirudiarudia.

Tunapaswa kusema wazi katika ziara ambayo mheshimiwa Rais ataifanya hivi karibuni mkoani Simiyu na wilayani Maswa kuwa Kiongozi anayeingilia majukumu ya walipafedha ni hatari zaidi kuliko adui anayeonekana. Kwa sababu huyu anaharibu kutoka ndani kwa kutumia mamlaka aliyokabidhiwa na serikali.

Tusikubali kufumbia macho!
Walipafedha wapewe heshima yao, mamlaka yao yaheshimiwe, na madaraka ya kiongozi huyo yadhibitiwe kwa kufuata sheria.

Hakuna maendeleo ya kweli katika mazingira ambapo wenye mamlaka wanavuruga taratibu kwa faida zao binafsi.
Wito kwa wananchi na taasisi za serikali.
  • Toeni taarifa za uingiliaji huu kwa vyombo husika kama TAKUKURU, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), na hata vyombo vya habari.
  • Kataa kushiriki katika unyang'anyi huu wa maendeleo.
  • Simama kidete kulinda kila senti ya umma — maana ni kodi yako inayochezewa!
Maendeleo ya taifa hili hayapaswi kuwa mateka wa tamaa ya wachache. Lazima tuwakatae hadharani na kisheria, viongozi wanaothubutu kupora majukumu ya walipafedha na kutumia fedha za umma kama hazina yao binafsi.
Tusikubali. Tunastahili zaidi.
 
Back
Top Bottom