Elections 2010 Masuala ya uchaguzi

riri88

Member
Jul 20, 2010
5
0
Habari gani?
Mimi ni Irene, natoka Italy, Naples na nasoma kiswahili katika chuo kikuu.

Lazima nisome kwa tasnifu na ningependa kuandika kuhusu maswala ya uchaguzi ujao na kufuata kampeni zima hadi uchaguzi wa Oktoba.
Natafuta magazeti muhimu yenye fikra ya kisiasa tofauti, lakini ningependa kujua pia vijana wote wanavyowaza kuhusu maswala na wagombea..

mnataka kunisaida??
mnaweza kusema mnapendavyo na kuzungumza kuhusu suala muhimu kuliko kwenu... na mkitaka kunipa mashauri mengine kwa somo langu.

asante sana,
na samahani kwa kiswahili changu!:redface:

Mabusu,
Irene
 
Hi Irene,
Asante kwe mabusu..:smile: Kiswahili chako si kibaya kama unavyodhani, binafsi nimefurahia kusikia kwamba unasoma Kiswahili Chuo Kikuu...

Hakuna shaka,tutakupa msaada wowote unaotaka kuhusu lugha yetu tamu ya Kiswahili.

Karibu jamvini....:smile:
 
Nakutakia mradi mwema.
Je Wigo wa huu mradi utakuwa tanzania nzima au unapenda kupata taarifa za dar esalama tu ?

We ukiwa na swali uliza tu hapa JF watakupa mchango.
 
Habari gani?
Mimi ni Irene, natoka Italy, Naples na nasoma kiswahili katika chuo kikuu.

Lazima nisome kwa tasnifu na ningependa kuandika kuhusu maswala ya uchaguzi ujao na kufuata kampeni zima hadi uchaguzi wa Oktoba.
Natafuta magazeti muhimu yenye fikra ya kisiasa tofauti, lakini ningependa kujua pia vijana wote wanavyowaza kuhusu maswala na wagombea..

mnataka kunisaida??
mnaweza kusema mnapendavyo na kuzungumza kuhusu suala muhimu kuliko kwenu... na mkitaka kunipa mashauri mengine kwa somo langu.

asante sana,
na samahani kwa kiswahili changu!:redface:

Mabusu,
Irene

Kwa Niaba ya JF Nzima. Asante kwa Mabusu
 
hakuna mtu anaitwa Irene katika chuo hicho ,uyu ni kibaka mwengine tu anabangaiza ?
 
Kwa niaba ya wanachama wote wa JF, kwa heshima na taadhima, napenda kupokea Mabusu ya dada Irene kwa niaba ya wote humu ndani :)
 
hakuna mtu anaitwa Irene katika chuo hicho ,uyu ni kibaka mwengine tu anabangaiza ?

Wewe una-authority gani ya kutuambia kuwa huyu binti hasomi katika chuo hicho, kwani wewe unasoma huko Italia? Mimi nimegoogle na nimepata jina lake kwenye orodha ya wanafunzi wanaosomea kiswahili huko!! Achana na ushambenga huo.
 
SIna authority yeyote ile ila nina haki ya kutoa maoni yangu vile nionavyo ,sasa wewe lkhali ndio utueleze una cheo gani cha kukataza watu hapa wasiseme au wasiandike vile waonavyo ndivyo ,kumbuka tu sijakataa kukosolewa ,zaidi kama ungedai ushahidi hapo ndio ingekuwa noma ,sasa wewe ulie guguli mbona hujaweka hiyo link ya kuwawezesha wengine kukonfirm kuwa huyo ni msomi katika chuo hicho ? Afu sijui unaelewa maana ya ushambenga au ni kutaka kujipendekeza kana kwamba nawe umo ni wale wale know too much without knowing anything just uvuvuzela !
 
Enheeee yamefika huko? watu hamna uvumilivu! kama bulesi angekuwa karibu na monitor nakwambia ungelamba si kofi tu bali na ngumi.
 
wanapunguza stress za uchaguzi; presha inapanda na kushuka; nami pia ngoja tu nipokee busu la shauni la irene-tetetete
 
Mambo! ningependa kupata mashauri kuhusu magazeti gani ni kuliko muhimu katika tanzania kwa kuelewa maswala gani yameandikwa kwa kampeni ya uchaguzi na habari zote zingeweza kunisaidia kuelewa wagombea wakuu...
asante sana.
 
Samahani Mwiba, lakini sielewi mambo nyingine umeandikwa kwa hyvio sijui sababu hutaki mimi nisome katika chuo hicho...
unataka kujua habari nyingine kuhusu mimi?niulize unachotaka... nipo!:smile:
 
Approach zako Mwiba katika suala hili si la kistaarabu.Nadhani una tatizo ingawa si kubwa sana.Usijali maana si la hospitali,litakwisha taratibu baada ya muda utajikuta unaweza kuuliza kwa kutulia na watu wakakuweka katika kundi la watu wa kawaida.Omba radhi kwa dhati utajikuta huru!
 
Back
Top Bottom