wadau,
naomba kujua tofauti ya hizi kadi za kibenki?? benefits au faida ya kuwa na aina fulani ya kadi kati ya hizo?
shukrani
Kimsingi hazina tofauti kabisa.
Zote zinakubalika sehemu nyingi sana duniani.
Sijawahi kukutana na sehemu ambayo inakubali matumizi ya Visa halafu ikatae matumizi ya MasterCard.
Nishawahi kutumia kadi (Visa na MasterCard) za Bank of America kwenye ATM ya CRDB, Bariadi, Simiyu!
Na zote hizo ni kampuni za Kimarekani.
EMT, remember this debate?
watu wa mabenki na mahesabu mnaposema Debit card mnamaanisha nini au credit card maana yake kwa mimi mtoto wa Tandale Uzuri kwa Bibi Nyau?
Debit card inamaanisha kadi aitumiayo mtu ambapo pesa inatoka moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yake.
Credit card ni kadi aitumiayo mtu ambapo pesa anayoitumia ni mkopo tu ambao unatakiwa ulipwe baadaye kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa.
Mkuu, huu mkopo una sura gani?
Je, "overdraft" nayo ni mkopo?
Maana kuna bank (nchi fulani) zinatoa "debit card" na mteja anavuta "overdraft"!!
[*]Bank of America offers Overdraft Protection which allows a checking account to be linked to another Bank of America account to help provide protection against returned items or overdrafts. During nightly posting, if there are insufficient funds to cover a transaction, funds are automatically transferred from the Available Balance in the linked account.
[*][*]You can receive account Alerts to your mobile phone or email to notify you when your Available Balance falls below a threshold you determine.
Kwa sura unamaanisha nini? Mambo kama ya APR?
Overdraft si mkopo by definition.
Ingawa kwa baadhi ya mabenki uki-overdraw utalimwa overdraft fee(s) na kudaiwa kiasi ulicho-overdraw.
Benki nyingi za majuu nizijuazo mimi huwa zinatoa huduma ya overdraft protection. Mara nyingi hii huduma huwa si ya moja kwa moja (automatic). Ni mpaka uiweke mwenyewe. Ukiwa nayo halafu tuseme utumie kadi yako sehemu kwa kiasi ambacho hakipo kwenye akaunti yako, kadi itagoma.
Ona haya maelezo machache kuhusu overdraft protection ya Bank of America:
[*]
[*]
Nafikiri kuna mtu ameiba ID ya Nyani Ngabu huwa hatoi maelezo yasiyokwenda shule kama haya, pengine kazeeka siku hizi maana ukizeeka na akili inakuwa kama ya Mugabe.
Huh?
Kwa hiyo nilichoandika ni pumba au...?
Hukuandika pumba, hivi ni wewe kweli? Naona maelezo yako dhoofu kidogo mimi sitaki kuingilia... ... .. huku Alaska baridi imeanza bana.
Kimsingi hazina tofauti kabisa.
Zote zinakubalika sehemu nyingi sana duniani.
Sijawahi kukutana na sehemu ambayo inakubali matumizi ya Visa halafu ikatae matumizi ya MasterCard.
Nishawahi kutumia kadi (Visa na MasterCard) za Bank of America kwenye ATM ya CRDB, Bariadi, Simiyu!
Na zote hizo ni kampuni za Kimarekani.
EMT, remember this debate?
mkuu mbona mimi Mara nyingi kuna sehemu huwa wanakataa master card ( credit)?
Nafikiri kuna mtu ameiba ID ya Nyani Ngabu huwa hatoi maelezo yasiyokwenda shule kama haya, pengine kazeeka siku hizi maana ukizeeka na akili inakuwa kama ya Mugabe.