Anna Tibaijuka
Member
- Apr 20, 2013
- 15
- 424
Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?
Profesa shida ya nchi yetu ni kutokutii sheria zilizopo na kutojali mipango tuliyojiwekea. Inasikitisha kuona miji mingi nchini ikikua kwa kasi-holela...kila mtu anajenga anavyotaka na hakuna mamlaka inayojishughulisha kuzuia hali hiyo.
Kama ulivyosema kupanga ni kuchagua. Nyie mliopewa nafasi ya kusimamia miji yetu ndiyo mnapaswa kuhakikisha sheria zilizopo zinafuatwa na kila raia. Pia wizara yako na halmashauri au manispaa zijitahidi kupima, kuuza na kusimamia uuzaji ardhi hasa za mijini kwa wananchi kuliko kuachia kila mtu auze kiholela hali inayopelekea ujenzi holela kuendelea kuwa tatizo kwenye miji yetu.
Mimi nashauri Mjenge makao makuu ya Tanzania inakuwaje nchi haina mji mkuu Mnazidi kujibana Dar??Jengeni Dodoma fumueni miundo mbinu ya CDA anzisheni miundombinu mipya!!Kigamboni nisawa kawa swala la ustawi wa nchi lakini kwa heshima ya nchi Makao makuu yanahitaji kujengwa pia!!
Daha napata wakati mgumu kukujibu kwani hata mimi sijui hatima ya hii kitu kinaitwa makao makuu ya Nchii inamaana kikija chama kingine kinaweza kikaamua makao makuu yawe LINDI!kakakiiza hivi unadhani Dodoma ni makao makuu ya nchi?
Dodoma ni makao makuu ya CCM, hivi unadhani chama kingine kikichukua nchi Dodoma itaendelea kuwa makao makuu?