Master plan ya Lowassa ni ipi?

Master plan ya Lowassa ni ipi?

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,302
Habari wanaJF?

Lowassa alikua amepanga kuwa rais wa hii nchi tangia miaka angalau mitatu hivi nadhani hivyo ni mtu ambaye alikua anasoma na kupanga mipango mikubwa jinsi ya kuleta maendeleo kwenye hii nchi tofauti na Magufuli ambaye inaonekana ni kama alishtukizwa tu.

Ila kwenye kampeni zake nikisikiliza na nikitafuta kwenye mitandao mi sijaona akitoa mipango ya jinsi ya kuibadilisha hii nchi ki ukweli ukweli
mi nasikia akitoa ahadi ndogo ndogo tu kama vile kusaidia mama ntilie, bodaboda, wachimbaji wadogowadogo, sijaona namna ambavyo atatatua matatizo makuu kwenye hii nchi kama vile ukosefu wa ajira, shilingi kuporomoka, usimamizi mzuri wa rasilimali zetu kama gesi, bandari , vyanzo vya maji, miji kukua bila mpangilio {foleni}, kilimo duni, ufisadi na rushwa n.k.

Mimi nataka mabadiliko lakini kwa mtu sahihi, naomba mnisaidie hapa..
 
Unataka master plan Kwani unataka kucopy kitu gani mkuu.
Jiulize tumekuwa na master plan ngapi Tangu uhuru. Je Tunasonga ama tunatudi?
Usikute hhata hata master yaafamiliamyako yako.
 
Mpigie simu na uache kutusumbua kwa upuuziwa maswali
 
Mkuu master plan ya nchi imeshaandaliwa na watanzania wenyewe kupitia Rasim ya pili ya katiba Mpya.Kazi ya Lowasa ni kuirudisha na kuipeleka kwa wananchi waipe mamlaka.basi.

Kazi ya pili ni kuwa empower watanzania ili wajenge nchi Yao baada ya serikali kuongozwa na malofa wa akili for 54 years,malofa wanaoamini nchi hii itaendelea kwa kushinda ulaya na marekani kuomba omba
 
1. Atafuta tozo zote kwa mazao ya wakulima na wafugaji. Hawa ni 90% ya watz wote. kufuta tozo ni kuongeza kipato kwa mkulima huko ni kuuchukia umasikini.
2. Elimu bure kwa ngazi zote nchini.
KWA MKAKATI UPI?.
Kupunguza matumuzi ya anasa na kwa kukusanya kodi zote.
 
1. Atafuta tozo zote kwa mazao ya wakulima na wafugaji. Hawa ni 90% ya watz wote. kufuta tozo ni kuongeza kipato kwa mkulima huko ni kuuchukia umasikini.
2. Elimu bure kwa ngazi zote nchini.
KWA MKAKATI UPI?.
Kupunguza matumuzi ya anasa na kwa kukusanya kodi zote.

Endeleeni kulialia muone km watz watawaonea huruma
 
Lowassa amekuwa na vission ya hii nchi kwa zaidi ya miaka 20
 
Unadai umefuatilia ila ulivyoandika inaonyesha kabisa hujafuatilia
 
Lowassa anahaidi uboreshaji na siyo mabadiliko. Nasema uboreshaji kwa kua kila anachoahidi ni kiko kwenye utekelezaji wa CCM au ahadi za CCM na hii Mfano suala la elimu anasema elimu bure badala ya kuahidi Mfano kutumia lugha mama kiswahili hadi chuo au kiingereza toka darasa la kwanza n.k kwa hiyo underpinnings za elimu zibaki vile vile yeye lowassa mabadikiko yake ni ubure hii tunaita cosmetic make up na siyo mabadiliko.

Kwenye suala la Katiba lowassa mwenyewe hajahaidi kama rasimu ya warrioba italetwa kwa wananchi kupigiwa kura ya maoni ndani ya muda let say mwaka au miezi mi3 au Siku 100 za kwanza za utawala wake,kuhusu tatizo ufisadi hajaongea kama ataanzisha mahakama au time ya kujadili na kurudisha rasilimali zikizoibiwa katika kipindi fulani chini ya CCM Mfano wa Buhari kule Nigeria ambapo aliahidi kufanya hivyo kama mojawapo ya ahadi za mabadiliko Nigeria na kuua ufisadi nchini humo na mpaka sasa Nigeria na buhari wanefanikiwa kurudisha kwa umma $50b zikizokwapuliwa na walafi wachache .

Kwa mantiki hii hapa tunaona huyu lLwassa asiyeamini mabadiliko ni mtu mbinafsi anayetaka tu kutimiza ndoto binafsi awe rais wa Tanzania basi.

Mabadiliko uwa hayawi vuguvugu mabadiliko ni moto mabadiliko siyo kuboresha mabadikiko ni kufutilia mbali yaliyopo sasa, mabadiliko uwa na ahadi zinazopimika ndani ya muda unaopimika na siyo ahadi tu zisizopimika, na muhimu mabadiliko hufanywa na wale ambao hawakua mpaka hivi punde tu hawaamini kwenye hayo mabadiliko na walikua ni sehemu kubwa ya tatizo lenyewe in the first place hadi tukatamani hayo mabadiliko.
 
Lowassa anahaidi uboreshaji na siyo mabadiliko. Nasema uboreshaji kwa kua kila anachoahidi ni kiko kwenye utekelezaji wa CCM au ahadi za CCM na hii Mfano suala la elimu anasema elimu bure badala ya kuahidi Mfano kutumia lugha mama kiswahili hadi chuo au kiingereza toka darasa la kwanza n.k kwa hiyo underpinnings za elimu zibaki vile vile yeye lowassa mabadikiko yake ni ubure hii tunaita cosmetic make up na siyo mabadiliko. Kwenye suala la Katiba lowassa mwenyewe hajahaidi kama rasimu ya warrioba italetwa kwa wananchi kupigiwa kura ya maoni ndani ya muda let say mwaka au miezi mi3 au Siku 100 za kwanza za utawala wake,kuhusu tatizo ufisadi hajaongea kama ataanzisha mahakama au time ya kujadili na kurudisha rasilimali zikizoibiwa katika kipindi fulani chini ya CCM Mfano.wa Buhari kule Nigeria ambapo aliahidi kufanya hivyo kama mojawapo ya ahadi za mabadiliko Nigeria na kuua ufisadi nchini humo na mpaka sasa Nigeria na buhari wanefanikiwa kurudisha kwa umma $50b zikizokwapuliwa na walafi wachache
Kwa mantiki hii hapa tunaona huyu lowassa asiyeamini mabadiliko ni mtu mbinafsi anayetaka tu kutimiza ndoto binafsi awe rais wa tz basi.

Mabadiliko uwa hayawi vuguvugu mabadiliko ni moto mabadiliko siyo kuboresha mabadikiko ni kufutilia mbali yaliyopo sasa, mabadiliko uwa na ahadi zinazopimika ndani ya muda unaopimika na siyo ahadi tu zisizopimika, na muhimu mabadiliko hufanywa na wale ambao hawakua mpaka hivi punde tu hawaamini kwenye hayo mabadiliko na walikua ni sehemu kubwa ya tatizo lenyewe in.the first place hadi tukatamani hayo mabadiliko.
mkuu hapa jamii forum kuna watu wenye background tofauti kwa hiyo ni vema ukalizingatia Hilo kabla ya kupost ujinga wako
 
Nafatilia sana hotuba zake za majukwaani wala hatuwezi kusema zile ni hotuba anacho fanya ni kutoa mihitasari tu ya dakika tatu alafu anakaa chini!!

Simsemi vibaya lakini tuna wajibu wa kuwa wakweli - Jamaa huyu hana mkakati wowote thabiti wa kuleta mabadiriko ya kweli katika Taifa letu, kama angekuwa nao basi angejinadi majukwaani wananchi wakamsikiliza na kujiridhisha kwamba jamaa huyu balabala,ninacho shuhudia mimi ni mihemuko ya kisiasa ya kutaka mabadiriko bila ya kujali wasifu wa mshika bendera kama ana uwezo wa kuwavusha rubicon au hana!
Rasm ya pili ya katiba mpya ambayo Lowasa na chadema wana ahidi kuifufua si tu inafanya mabadiriko Bali pia kufagia uchafu wote ulioletwa na ccm ndani ya nchi hii.haya huyaoni kwa Kuwa akili yako ipo likizo.hapa unatumia akili ya magufuli,ulofa,upumbavu na tumbo lako
 
Elimu..Elimu..Elimu..Kilimo..Afya..Mawasiliano..na kama hauna uccm kwa sasa Tanzania tunahitaji vitu kama hivyo..itasaidia vijana kujitambua na kuacha kuongea pumba humu JF ili akapate buku 5 pale Lumumba..
 
mkuu hapa jamii forum kuna watu wenye background tofauti kwa hiyo ni vema ukalizingatia Hilo kabla ya kupost ujinga wako

Kitu gani technical hapa kinachohitaji ufanunuzi mithili ya matibabu toka kwa daktari? Wewe utakua wale wapuuzi wa team lowassa walioazima akili zao kwa kufikiria maslahi Yao binafsi kama huyo mtu atashinda...waafrika tuna safari ndefu sana namna hii
 
mkuu hapa jamii forum kuna watu wenye background tofauti kwa hiyo ni vema ukalizingatia Hilo kabla ya kupost ujinga wako
Na.kama siyo mpuuzi na unakuja jukwaa la siasa na.hujui kinaongelewa nini zaidi ya kutukana nakushauri jifunze kwa kusoma na kuuliza ukishindwa nenda jukwaa la mapenzi, chit chat n.k huko kunafaa akili yako fupi
 
Rasm ya pili ya katiba mpya ambayo Lowasa na chadema wana ahidi kuifufua si tu inafanya mabadiriko Bali pia kufagia uchafu wote ulioletwa na ccm ndani ya nchi hii.haya huyaoni kwa Kuwa akili yako ipo likizo.hapa unatumia akili ya magufuli,ulofa,upumbavu na tumbo lako
Mkuu labda nikukumbushe kitu, jaribu kutumia lugha yenye staha - usifikiri hatuna uwezo wa kutukana/kejeli,we can agree to disagree without offending anyone -don't U 4get that.

Taifa letu ni huru kila raia ana uhuru wa kutoa maoni yake bila ya kubugudhiwa na mtu, sio kila raia ni bendera fuata UPEPO kukimbia mbio mbio kukimbilia mlio kumbe wanako kimbilia kuna kilio! Nimalizie kwa kukupa ushauri wa bure, tukiwa ahi baada ya uchaguzi rudi hapa jamvini tutathimini kama lugha zenu za vijiweni zimewafikisha popote. CHEERS.
 
Back
Top Bottom