#COVID19 Massabo: Serikali Iwekeze Kwenye Elimu ya Chanjo Dhidi ya UVIKO—19

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Taarifa ya Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo juu ya Umuhimu wa Chanjo katika Mapambano dhidi ya Covid 19

Tangu dunia ilipokumbwa na janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid19, mwezi Machi 2020, jitihada kubwa zimechukuliwa katika mataifa mbalimbali katika kutafuta chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona. Ni jambo lenye kutia faraja kwamba chanjo imeweza kupatikana katika kipindi cha muda mfupi na mataifa yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi, sayansi na teknolojia yameongoza kupatia wananchi wao chanjo.

Hata hivyo, kwa muda sasa kumejitokeza maneno yasiyokuwa na ithibati za kisayansi kutoka kwa baadhi ya watu hapa nchini kupinga matumizi ya chanjo kwa watanzania kwa madai kuwa chanjo hizo si salama. Maneno hayo yanatolewa hadharani na kwenye mitandao ya kijamii.

Sisi Ngome ya Vijana ACT Wazalendo tunaitazama hali hii kuwa yenye kuleta mtanziko na inayorudisha nyuma mapambano dhidi ya janga la Covid19. Wananchi wanayumbishwa na maneno ya watu wasio na utaalamu wa afya na kwa kuwa jamii yetu kwa kiasi kikubwa haina elimu ya kutosha juu ya masuala haya, inajikuta ikijazwa hofu na upotofu kwa na hivyo kuweka vikwazo katika kupamabana na maradhi haya badala ya kutoa ushirikiano.

Sisi tunaamini kuwa, chanjo iliyoletwa nchini ni salama na ina ufanisi kwani imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Ni kwa msingi huo, tunayachukulia maneno yanayotolewa na baadhi ya watu kuwa chanjo hizi si salama na kwamba zina malengo ya kuangamiza vizazi vyetu, kuwa ni uzushi na propaganda zisizo na msingi. Uzushi na maneno hayo ni hatari kwani yanapokelewa na jamii na kuaminiwa.

Tunapenda kutoa rai na ushauri ufuatao kwa serikali katika kushughulikia na suala la chanjo ya virusi vya Corona;-

i). Serikali iwekeze vya kutosha katika utoaji wa elimu ya Chanjo. Watanzania wanapotoshwa kwa sababu hawajaelezwa chanjo ni kitu gani, inafanya kazi gani, inafanyaje kazi, ina manufaa gani, na na changamoto gani. Ukosefu wa kampeni na mkakati mahsusi wa elimu kwa umma utasababisha malengo ya Wizara ya Afya kutokomeza janga la Corona kutofikiwa kwa wakati


iii)Serikali ije na mkakati mahsusi wa kuhakikisha upatikanaji wa chanjo ya kutosha kwa wananchi kwenye Vituo vya Afya na Zahanati nchini. Chanjo iliyowasili bado ni kidogo ikilinganishwa na idadi ya watu nchini. Ili kudhiti janga hili, ni vizuri kila mmoja akapatiwa chanjo ili kujilinda dhidi ya maambukizi.

iv). Serikali kwa kushirikiana na nchi zenye ujuzi na utalaamu wa juu wa matibabu ya binadamu iwekeze vya kutosha katika utafiti wa chanjo hapa nchini ili nchi yetu ijitengenezee uwezo wa kuwahudumia watanzania bila kutegemea hisani ya mataifa mengine.

v). Watanzania tujijengee utamaduni wa kusoma na kujifunza masuala mbalimbali yenye umuhimu kuepuka kuyumbishwa na kupotoshwa na watu wenye malengo yasiyoeleweka. Wananchi wengi bado hawana uelewa wa masuala kama haya ya chanjo kwa sababu jamii yetu haiwekezi muda wao katika kujisomea na kujifunza mambo ya msingi.

Hitimisho;
Janga la Virusi vya Corona ni changamoto ya dunia nzima. Si tatizo lililoletwa Africa na wazungu kama ambavyo baadhi ya watu wanatapakaza maneno. Dunia nzima inahangaika kupambana kudhibiti maambukizi ya vurusi hivi na hatimaye kuutokomeza ugonjwa huu. Wajibu wetu ni kuwasukiliza wataalamu wa afya na kuzingatia maelekezo yao. Ngome ya Vijana ACT Wazalendo tutaendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii katika mapambano dhidi ya janga hili kuhakikisha tunaokoa maisha na nguvu kazi ya watanzania isiendelee kuteketea.


Imetolewa na:

Julius Masabo
Katibu wa Habari, Uenwzi na Mahusiano na Umma
Ngome ya Vijana,
ACT Wazalendo.
28 Julai, 2021.
IMG-20210728-WA0008.jpg
 
Yasiyo na ithibati ya sayansi!?😂,are you joking,,kaangalieni database ya VAERS.
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Back
Top Bottom