py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,471
- 4,424
Ubovu wa Gyan kumbe ulisababishwa na imani za kurogwa”-kocha Simba
Kaimu kocha mkuu wa Simba Masoud Djuma amesema, wakati anaingia Simba alikuwa haamini kama Nicholas Gyan ni mchezaji mzuri lakini baada ya kukaa na kuzungumza na mchezaji huyo alimwambia kwamba ameambiwa anarogwa ndio maana anashindwa kufanya vizuri.
Baada ya kocha huyo kukaa, kuzungumza na kumshauri Gyan kuachana na imani hizo za kurogwa, Gyan ameonesha kiwango cha hali ya juu.
Djuma pia amesema, hampangi mchezaji kwa sababu ya jina au undugu ndiyo maana Mavugo licha ya kuwa ni mburundi mwenzake lakini hachezi kwa sababu hayuko fiti, atakapokuwa sawa atapata nafasi ya kucheza.
“Nilivyokuja Simba nilimwambia Gyan wewe kwangu sio mchezaji, alikuwa hawezi kutuliza mpira wala kupiga pasi kwenye mpira kama huwezi kutuliza mpira wala kupiga pasi huwezi kuwa mchezaji.
“Nikajakujua kwamba ana matatizo kichwani aliambiwa amerogwa, nikamwambia kama ametoka Ghana akiwa mchezaji mzuri iweje ashindwe kucheza, nikamwambia aachane na hayo mambo yeye acheze mpira. Siku ya kwanza alipofanya mazoezi mazuri nilimwita nikamwambia tangu nifike Simba leo ndiyo nakuona umefanya mazoezi mazuri”-Masoud Djuma kuhusu Gyan kuamini katika ushirikina.”