Kama mnavojua timu ya Taifa ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17 inashiriki michuano ya kutafuta bingwa wa afrika .Tanzania ni mwenyejeji wa mashindano husika.Hata hivyo pamoja na kuwa mwenyeji ,timu yetu ni kama imeshatolewa kwani imeshafungwa mechi mbili kati ya tatu inazotakiwa kucheza.Pamoja na kutolewa huko si vibaya tukampa pongezi Mwenyekiti wetu wa uhamisishaji ushindi ambae ni mkuu wa mkoa Mheshimiwa Paul Makondo kwa kujitolea kusimamia jukumu hili kubwa .