dm2000inter
Member
- Oct 27, 2010
- 29
- 10
Maskini mji wa Moshi,
Hadhi ya Mji wa Moshi inaporomoka kwa kasi kutokana na barabara zake za lami kukithiri mashimo makubwa bila kufanyiwa ukarabati kwa muda mrefu. Leo barabara ya kwenda KCMC ni hatari kwa wagonjwa wanaokimbizwa kuokoa maisha yao kutokana na mashimo barabarani.
Uzuri ule wa barabara za mji wetu unatoweka mithili ya moto wa kifuu huku menejiment wakiwa wamelala usingizi fofofo hadi wananchi sasa wanamkumbuka Mama Bernadeta Kinabo kwa umahiri wake hadi mji wa Moshi ukashika nafasi ya kwanza kitaifa kwa usafi kwa miaka sita mfululizo. Lakini leo tumeshikwa mashati na Iringa na kuporomoka hadi nafasi ya pili. Unafikiri nini chanzo cha hali hii na suluhisho lake ni nini? Tujadili pamoja
Moshi unakua vizuri tu nilipita majuzi nyumba za juu (ghorofa) zinachipuka kwa kasi ya kuridhisha. Usafi bado ni mzuri sana kila sehemu. Hizo barabara zenye mashimo zitengewe bajeti mara moja kwa sababu sioni mantiki ya kuweka lami barabara zinazotoka nje ya mji tunaacha za ndani ya mji. Manispaa amkeni!
Wanachokijua Ni Mbwembwe Za Kujengea Tu Makaburi Kifahari Na Kuishi Ki Dili Dili Na Kimagumashi Humu Mijini Mwetu.
Wanachokijua Ni Mbwembwe Za Kujengea Tu Makaburi Kifahari Na Kuishi Ki Dili Dili Na Kimagumashi Humu Mijini Mwetu.
Mkuu upo Moshi muda huu au uko kwenye mikoa ya watuHakuna sehemu nzuri ya kuishi hapa bongo kama moshi,kuanzia usalama hadi hali ya hewa.
Unajua sasa hivi joto la Moshi ni nyuzi ngapi za centrigrade? au umeamua tu kunogesha jukwaanaipenda sana moshi cheki hiyo picha ilivyokaa uzuri hali ya hewa ni safi mno
ile barabara ya kuingia nyumbani kwako ushamaliza kujenga kiwango cha lami...aiseeeee sawa basi tutaenda wka wenyewe si lazima chadema wala ccm okey
ile barabara ya kuingia nyumbani kwako ushamaliza kujenga kiwango cha lami...
Hapo ndo moshi mjini au?