Maskendo yake .........nisaidieni jamani. Nifanyeje?

Maskendo yake .........nisaidieni jamani. Nifanyeje?

Siamini kama ni kweli unahitaji tukushauri kwa hili..!!
 
endelea nae anakupenda sana maana sijui unataka kushauliwa nini hapo
 
unasema unampenda pamoja na yote hayo? nashindwa kukupa ushauri wangu wa moja kwa moja kwasababu utakuumiza.
 
. Acha ujinga wewe

Huyo mwanamke anakudanganya

Na wewe umeeidhia kudanganywa kwa kisingizio cha kumpenda sana

Ungekuwa wa maana kwake ulivyoenda angetoka

 
Bila shaka wewe ni tegemezi kwa huyo mwanamke kwenye mambo ya kifedha. Huna mapenzi ya kweli kwa huyo mwanamke kama unavyotaka kutuaminisha, la sivyo una udhaifu fulani.
Endelea kumtegemea mpaka pale utakapopata majibu juu ya afya yako kwamba ni muda muafaka uanze kutumia dozi.
 
Are you mwanamume kweli ama mwanamuke? Skia huyo mdada hana uchaguzi na inavyoelekea anataka kuwa na nyote wawili either mmoja awe mlezi wa mtoto wake mwingne awe mlezi wa yeye mwenyewe na umeshaonywa na bwanae kuwa uachane na mkewe so unauliza nini tena? Had utolewe meno ndo uelewe au? Achana na huyo mwanamke wewe unampenda kitu gani bana wanawake wamejaa tele we muombe mungu wako upate asiye na vkwazo umwoe kabsa ,achana naye huyo HAKUFAI KABISAAA!
 
Jamani wanaJF nakuja kwenu na bonge la tatizo. Kwa kuwa hapa ni kigoda cha fikara naamini nitapata ushauri mzuri.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32. Nina mtoto 1 ambaye nilimpata nikiwa napita ktk kipindi cha balehe.Sina mke hadi sasa. Kwa muda wa miezi 12 nimekuwa ktk mahusiano yenye malengo ya ndoa na dada ambaye naye ana mtoto wa miaka 2. Dada huyu alinihakikishia kuwa mzazi mwenzie hayuko naye tena. Dada huyu pia amewahi kutembea na rafiki yangu wa karibu wa sasa kabla ya kuwa na mtoto. Hili limekuwa likinipa shida hata kumtambulisha demu huyu.
Mbali na hilo miezi 6 iliyopita nilipgiwa simu na jamaa aliyezaa naye akinisihi niachane na mkewe. Mimi nilianza kumkwepa yule dada kwa kuwa hakuwa mkweli maana alisema hana mtui. Baada ya wiki 1 yule dada alinifuata akiwa na marafiki zake 2 akadai yule mzazi mwenzie kesha achana naye na hana mpango wowote isipokuwa anamharibia tu. Mimi nikarudiana naye na nikazama vilivyo ndani ya moyo wake. Ikawa tunakula raha za kila aina za kimwili.
Wiki iliopita nilikwenda kwake bila taarifa mida ya saa 2 usiku. Nilipofika niligonga mlango mara tatu sikupata majibu. Kwa kuwa taa za sebuleni zilikuwa zinawaka nilijipa moyo kuwa huenda yupo chumbani kajilaza kitandani na amepitiwa na usingizi. Nilizunguka nyuma ya nyumba ili nimuite chumbani kwa kupitia dirishani. Niliita mara 2 bila majibu. Mara ya 3 nilikaribishwa na mwanaume aliyekuwa nyuma yangu akitokea ndani ya nyumba ninayogonga. Tulipoingia ndani yule mwanaume alimwita mara 3 yule dada kwa jina aje pale sebuleni ampokee mgeni wake ambaye ni mimi. Dada hakutoka. Ndipo yule jamaa akaniuliza `kwani wewe nani na ni nani yake?` Nikamwambia mm ni mpnz wake na nilipotaja jina langu akaniuliza unakumbuka kuna siku nimekupigia simu kukuonya uachane na mke wangu? Nikampa full story. Akaingia chumbani na kuanza kushusha kichapo kwa yule dada bila huruma, nami nikasepa faster. Leo hii ninavyoandika thread hii yule dada kamtuma rafiki yake aje kumuombea msamaha na kuahidi kumuacha kikweli kweli yule jamaa yake kwani hana malengo mazuri na yule dada kama niliyo nayo mm.
Nimkubalie ama nimkatalie? Maana dada nampenda mno. Naombeni msaada wa kimawazo, niko njia panda.

Mi nakuelewa sana ni kweli unampenda wewe unafanana na mimi ambaye nikipenda nimependa,kuna Ngoma bwana.hivi Kwa Umri huo hebu fikiria ulipokuwa na say 20 mpaka sana wazuri wangapi wamepita na sasa ulishawasahau? tena sasaivi wengine wanahangaika na mateso sema tu hawajua watatokaje,tena ukifuatilia unaweza kukuta wangekupa matatizo makubwa....,na kama umeandikiwa yeye nda wa kuoa,sasa umemfumania live na uzinzi,je haitakuuma pindi hii kitu ikikuijia kichwani ghafla ukashindwa hata ku ejaculate mjamaa akasinyaa ghafla?
Hebu pata Muda wa ku meditate kama 6months to 1 year kukaa na kutafakari utapata mawazo mapya na ujaribu kumuomba Mungu sana.Sometimes Mungu anazungumza nasi kwa Vitendo,Sometimes Mungu anazungumza nasi kwa Negatives things to happen ili kuzuia matwakwa yetu na baadae ili aweze kutimiza malengo yake Mungu.
Kila la Kheri......
Mungu akubariki sana sana.
Jumapili njema.
 
Leo hii ninavyoandika thread hii yule dada kamtuma rafiki yake aje kumuombea msamaha na kuahidi kumuacha kikweli kweli yule jamaa yake kwani hana malengo mazuri na yule dada kama niliyo nayo mm.
Nimkubalie ama nimkatalie? Maana dada nampenda mno. Naombeni msaada wa kimawazo, niko njia panda.

Well, sasa hivi ameahidi kumuacha Kiukweli kweli huyo Jamaa,
Mwanzoni alikuwa anamuacha kiuongo uongo huyo Jamaa,
Labda akupe sababu ni kwa nini hakutaka kumuacha Kiukweli ukweli hapo kabla?
Akikupa jibu njoo uniambie nitajua cha kukushauri.

Mapendo.
TANMO
 
Utakufa siku si zako. Huyo dada ako muongo malaya na shenzi. Aibu hana? Yeye na marafiki zake mashangingi. Wanakucontrol
 
ushukuru kweli kwa kusalimika siku hiyo.
 
hivi unapoomba ushauri hapa bila kutumabia wewe unafikiria nini una maana? sema msimamo wako kwanza ndio upewe ushauri, kumpenda sana si lazima kuwa nae, ...pambaf
 
Kweli kuna la kuja kuuliza humu?! Eti una miaka 32 umesema?!

Wazazi wako wakijua hili wanakulaani uwe mwehu kabisa!!
 
WanaJF nawashukuruni nyote kwa kunipa ushauri japo ujumbe uliwasilishwa kwa lugha kali. Nakubali na kuupokea ushauri wenu.
Nimeamua kuachana naye. Japo yeye hadi leo ananitumia sms kunisihi nimpe nafasi ya mwisho. Anadai eti kesha enda hadi kwa mjumbe kuchukua barua ya kumstopisha jamaa yake kufika kwake na kumpa formula ya kumuona mwanaye. Hata hivyo sikutaka kupata undani zaidi wa formula yenyewe kwani sikutaka hata kujibu sms zake.
Kwahyo akina dada masingo wote mliopo JF naomba mniPM ili nianzishe penzi jipya. Nikikupenda nang`ang`ania kama ruba.
 
Hata sijui nishauri nini!, ni kama mtu akikuuliza ukipewa chai unaweka sukari au chumvi? Kuepusha utata namwambia kunywa hivyo hivyo.
 
Acha ubwege wewe, madem wameisha? mbona wapo kibao? Upendo gani huo, mpaka unakuta dem live na mwanaume? Niambie unataka wa namna gani nikupe namba.
 
Back
Top Bottom