Masikini watoto hawa!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SIMANZI imetawala kwa wazazi na uongozi wa Shule ya Awali iitwayo Nia baada ya kupoteza watoto wanne kufa papohapo baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wakiwa michezoni
Shule hiyo ya awali ‘chekechea’ ipo Kimara Matosa jijini Dar es salaam wilayani Kinondoni inamilikiwa na Jacqueline Sarungi [42] mkazi wa Kimara Matosa.

Juzi majira ya saa 6:30 mchana katika shule hiyo watoto wane walipoteza maisha papohapo na wengine watatu walijeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba uliokuwa karibu na shule hiyo.

Watoto hao walipoteza maisha wakati walipokuwa wakibembea na ghafla waliangukiwa na ukuta wa nyumba iliyo karibu na shule hiyo

Watoto waliopoteza maisha ni Isaack Ndosi [5], Gladness Shimwela (5), Devotha Living (5)na Ludacris Lawrence (3) wote walikuwa wakazi wa Kimara B Matosa.
 
mwenye sshule akamatwe na asekwe jela...huu ni uhaini,a ada zinalipwa lakini majengo hayaboreshwi, hapo hamna cha siasa, sweka jela na damu zao zitamlilia...unakumbuka kule tabora kwenye kumbi flani watoto walikufa siku ya sikukuu......hawajifunza tu...huu ni uzembe sana...!!
 
Kaka una uhakika na mazingira ya ajali yenyewe? Nimesikia kitu kama ukuta wa nyumba ya jirani, hapo mwenye shule anahusika vipi?
 
ok kuna umuhimu wa maeneo ya shule kua mbali na makazi ya watu!
Kaka una uhakika na mazingira ya ajali yenyewe? Nimesikia kitu kama ukuta wa nyumba ya jirani, hapo mwenye shule anahusika vipi?
 
ipo haja ya wanao kagua shule wawe wana fanya proper risk assessment hata ya majirani , au kama shule ina uzio, na pia sisi wenyewe tuwe tunakumbushana kuhusu taadhari ya majalala tunamopita, vyoo, kuta nk nk ambapo mara nyingi watoto wanapita au kucheza. Maana tunatabia ya kudharau vitu au kusema hiki hakinihusu, lakini wewe au mimi tunaweza kupita hapo tukapata hayo madhara.
na Pole kwa wafiwa.
 
SIMANZI imetawala kwa wazazi na uongozi wa Shule ya Awali iitwayo Nia baada ya kupoteza watoto wanne kufa papohapo baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wakiwa michezoni
Shule hiyo ya awali ‘chekechea’ ipo Kimara Matosa jijini Dar es salaam wilayani Kinondoni inamilikiwa na Jacqueline Sarungi [42] mkazi wa Kimara Matosa.

Juzi majira ya saa 6:30 mchana katika shule hiyo watoto wane walipoteza maisha papohapo na wengine watatu walijeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba uliokuwa karibu na shule hiyo.

Watoto hao walipoteza maisha wakati walipokuwa wakibembea na ghafla waliangukiwa na ukuta wa nyumba iliyo karibu na shule hiyo

Watoto waliopoteza maisha ni Isaack Ndosi [5], Gladness Shimwela (5), Devotha Living (5)na Ludacris Lawrence (3) wote walikuwa wakazi wa Kimara B Matosa.

Wakulaumiwa ni Idara ya ustawi wa jamii ya eneo husika kwani shule zote kama hiyo hutakiwa kukaguliwa maeneo na mazingira yake kabla na baada ya kuanzishwa na kuna sheria no 17 ya mwaka 1981 ya uanzishaji wa shule au vituo hivyo.Kama sheria hiyo ingefuatwa kusingekuwa na shule hiyo maeneo hayo na watoto hao wasinge angukiwa na huo ukuta mbovu na hatimae kupoteza maisha.Kwa Dar ni kawaida kukuta vishule hivi vipo ktk mazingira ya ajabu ajabu kwa mfano kapo kamoja maeneo ya Msasani -macho nyuma ya Chines restaurant watoto wanasomea juu ya Canopy na Uangalizi wa watoto ni mdogo na huyo mwalimu hana hata ujuzi wa ualimu wala malezi ya watoto! USTAWI WA JAMI K/NDONI MKO WAPI?
 
Back
Top Bottom