Masikini Sitta, Mwakyembe, Kinana, Nape n.k.

Masikini Sitta, Mwakyembe, Kinana, Nape n.k.

Naona team lowasa mnajaribu kutafuta huruma za Jakaya Kikwete.Lowasa anakatwa haendi popote.mwizi mkubwa yule.

Nadhani hukunielewa. JK ndiye CC, ndiye NEC na ndiye Chama. JK ndiye aliyemsafisha la sivyo angekuwa ameshakatwa tayari na hivyo vikao vilivyokutana Dodoma hivi karibuni. Hivyo hakuna tena mwenye uwezo wa kumkata.

Jiandae tu kutawaliwa na ma- trionairs na ma- billionairs: Tr Lowassa, Tr Chenge, Tr Kalamagi, Tr Rostam, Tr Msukuma, Br Tibajuka, Br Kange na kadhalika. Titles za u- Dr na u- Prof sasa mwisho, u- Ndugu ndiyo sahau kabisa.

NB: Tr = trionair, Br = billionair, Mr = millionair
 
kalaghabao!/ wewe ni nape nini?
lakini wakati mwingine imani huponya!

Lowasa rais wa ufisadi na mafisadi na ameanza safari ya kifisadi mwisho wake utakuwa wa machungu yatakayozidi machungu ya kulazimishwa kujiuzulu. Lowasa anatuona Watz hatuna akili na hatujui kitu juu yake. Anajiona Goliathi, DAUDI yuko na Kombeo lake.
 
Utakuwa hujatulia pengine wewe sio mtz ni mkimbizi km unaomba ushahidi wa ujambazi wa lowasa

Ohoo!!! kaa mkimbizi nipeleke kwetu maana utakuwa unapajua ila mie najua ni MNYATURU HALISI NA MTANZANIA 100%.
 
Yeye anaweza kushinda kwa kutumia pesa kununua watanzania, hatukatai. Lkn ukweli ni kwamba tutakuwa tumeamua kwa ridhaa zetu kulipa kundi fulani la kifisadi nchi hii. Hata wanaoshabikia kundi hili wana sifa mbili. Moja; wanafaida za moja kwa moja kwa kupata pesa toka kundi hilo au mbili; wana nia za kifisadi hivyo watafaidika km kundi hili litashika nchi.
 
Ohoo!!! kaa mkimbizi nipeleke kwetu maana utakuwa unapajua ila mie najua ni MNYATURU HALISI NA MTANZANIA 100%.

Sasa km mpaka leo hujui ujambazi wa lowasa basi km sio mkimbizi basi ulikuwa unaishi ughaibuni...
NAKUSHAURI FUATILIA KWA MAKINI MIJADALA MBALIMBALI UTAUJUA UFISADI PAPA NA UJAMBAZI SUGU WA lowasa
 
Siishi ughaibuni japo Kwa Sasa Niko ughaibuni ila nazijua siasa Za Nchi yangu kuliko maelezo.
Wewe unaenekana bado ni kinda sana Kwa siasa Za mbongo .
 
"INNOCENT UNTIL PROVEN GUILTY"
Mahakama gani iliyomuhukumu huyu jamaa?

Kwenye nafasi hii kubwa kuliko zote nchini anayoiomba (Mkuu wa nchi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya nchi), kweli ungalikuwa wewe ungalimpa nafasi hiyo mtu ambaye watu wengi tu wa ngazi mbali mbali, ndani na nje ya chama chake, waweonyesha mashaka dhidi yake? Kwa nini yeye tu ndiye wawe na mashaka kati ya kundi kubwa la waombaji waliojitokeza?

Inawezekana kabisa hana hatia ila tu ni bahati mbaya na ni mkosi tu umempata wa kuhisiwa visivyo! Kwenye nafasi hii nyeti sifa ya kuwa na mkosi wa kuhisiwa visivyo kwa kiwango hicho inatosha kabisa kumnyima kazi hiyo. Huwezi kuwa raisi mikosi, nchi unaweza kuiingiza kwenye mikosi.

Alichokosea ni kuwa alipaswa kuchukua hatua mapema sana dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, pamoja na kuwafikisha mahakamani wote waliokuwa wakimsema visivyo 'for defamation'. Sasa hakufanya hivyo, miaka mingi imepita na 'damage' imeshampata. It is too late; amechelewa.
 
Kwa taratibu za vyama vyetu vingi vya siasa, Mwenyekiti wa chama ndiye alfa na omega. Yeye ndiye chama: msimamo wake hauwezi kupingwa na kikao cho chote cha maamuzi katika chama husika. Vikao kama vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) maamuzi yake shurti yafuate kile ambacho Mwenyekiti anachotaka. Mwenyekiti ndiye CC na ndiye NEC; ndiye Chama!

Haikushangaza kwamba vikao vya CC na NEC vilimsafisha na kumruhusu aendelee na harakati zake za kuusaka umwenyekiti wa chama na uraisi wa nchi kwa utaratibu ule ambao alikuwa alishauanza kitambo uliokuwa umelalamikiwa na wengi, wakiwemo Katibu Mkuu wa Chama, Katibu Mwenezi wa Chama na vigogo wengi tu katika chama.

Kwa utaratibu wake huo aliokwisha jiwekea wa kuusaka uraisi wa nchi na uenyekiti wa chama, wa kutumia nguvu kubwa ya fedha (trions of TShs), sasa hakuna tena kitakachomzuia kupata hizo nyadhifa! Huu ndiyo ukweli. Hakuna kikao cho chote cha chama kitakachokata jina lake na hakuna chama cho chote cha upinzani kitakachomshinda! Usicheze na nguvu ya pesa. Ma- trionairs wa ndani na nje ya Tanzania wamejipanga vizuri nyuma yake kuhakikisha hili linafanikiwa. 'Money can buy anything in this planet except health'

Sana sana kitakachotokea ni kugawanyika kwa hicho chama. Pia Chaguzi kuu zijazo zitakuwa zinatumia mbinu hii. Enzi ya serikali kuwa ya Wanyonge sasa ni jambo lililopita. Tujiandae kisaikolojia, kuna mazuri na machungu tutakayovuna toka kwake.

Mungu ibariki Tanzania.
We si dr akili ni dr asye akili
 
Back
Top Bottom