Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,326
Kwa taratibu za vyama vyetu vingi vya siasa, Mwenyekiti wa chama ndiye alfa na omega. Yeye ndiye chama: msimamo wake hauwezi kupingwa na kikao cho chote cha maamuzi katika chama husika. Vikao kama vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) maamuzi yake shurti yafuate kile ambacho Mwenyekiti anachotaka. Mwenyekiti ndiye CC na ndiye NEC; ndiye Chama!
Haikushangaza kwamba vikao vya CC na NEC vilimsafisha na kumruhusu aendelee na harakati zake za kuusaka umwenyekiti wa chama na uraisi wa nchi kwa utaratibu ule ambao alikuwa alishauanza kitambo uliokuwa umelalamikiwa na wengi, wakiwemo Katibu Mkuu wa Chama, Katibu Mwenezi wa Chama na vigogo wengi tu katika chama.
Kwa utaratibu wake huo aliokwisha jiwekea wa kuusaka uraisi wa nchi na uenyekiti wa chama, wa kutumia nguvu kubwa ya fedha (trions of TShs), sasa hakuna tena kitakachomzuia kupata hizo nyadhifa! Huu ndiyo ukweli. Hakuna kikao cho chote cha chama kitakachokata jina lake na hakuna chama cho chote cha upinzani kitakachomshinda! Usicheze na nguvu ya pesa. Ma- trionairs wa ndani na nje ya Tanzania wamejipanga vizuri nyuma yake kuhakikisha hili linafanikiwa. 'Money can buy anything in this planet except health'
Sana sana kitakachotokea ni kugawanyika kwa hicho chama. Pia Chaguzi kuu zijazo zitakuwa zinatumia mbinu hii. Enzi ya serikali kuwa ya Wanyonge sasa ni jambo lililopita. Tujiandae kisaikolojia, kuna mazuri na machungu tutakayovuna toka kwake.
Mungu ibariki Tanzania.