Mkuu kwanza karibu sana humu JF kwa sababu naona umejiunga leo hii!
Pili kuhusu Kuondolewa kwa Michael Wambura tambua kwamba mpira wa Tanzania sio mpira hivi sasa,mpira unaendeshwa kisiasa zaidi,na ukitaka kuthibitisha hilo,jaribu kurudi nyuma kidogo tangu mchakato wa uchaguzi ulipoanza mwaka jana,kamati ya uchaguzi ya TFF inayoongozwa na mtu mmoja anayeitwa Deogratius Lyato kutoka huko wilayani ukerewe Mkoani Mwanza imeharibu uchaguzi na mpira wa Tanzania kwa ujumla.
Kiufupi kilichpofanyika safari hii kamati ya Lyato ilikuwa ikijaribu kuangalia namna ya kuhakikisha kwamba viongozi wanaopita kwenye vyama vya michezo vya mikoa hawapiti kwa lengo la kukuza mpira katika maeneo husika,bali ni kuhakikisha kwamba wanaopita huko mikoani wanakuja hapa Dar kwa ajili ya kupiga kura kuwachagua viongozi w TFF na hasa wale watu wanaowahitaji kwa ajili ya kulinda maslahi yao.
Deo Lyato na kundi lake wamejitahidi sana kuhakikisha kwamba mgombea wa nafasi ya Urais Athumani Nyamlani anapita kwenye uchaguzi utakaofanyika Februari 24 mwaka huu,hili liko wazi kwa sababu kampeni kubwa zimefanyika kwenye chaguzi za mikoa ambapo mkoa wowote ambao wagombea wake walikuwa hawauingi mkono upande wao walikuwa wakifanyiwa vituko vya kila aina.
Kwa mfano kuna mikoa ambayo ilifikia hatua ya uchaguzi kuahirishwa wapigakura tayari wakiwa ndani ya ukumbieti sabau ikiwa ni wagombea kutokuwa na vigezo,hivi kama watu wamejadiliwa na kupitishwa na kamati za uchaguzi za maeneo yao na kisha TFF yenyewe chini ya Lyato kuwapitisha na kuruhusu uchaguzi ufanyike hao mambo ya hana sifa yanatoka wapi tena,mfano Mkoa wa Tabora,Ruvuma na mingine.
Hiio ni aibu kwa Lyato na kundi lake,lakini nisema tu kwamba hawa watu siku zao za kula pesa za watanzania huko TFF zinazotolewa na FIFA kisi za zaidi ya shilingi milioni 800 kila mwaka zimefikia ukingoni,kwa sababu hao wanaowategemea watapigwa chini siku ya uchaguzi.
Nikirudi kwa Wambura ameonewa vya kutosha na kama kweli yeye ni mwanaume anayetokea mkoa wa mara ambaye najua alitahiriwa alafajiri ya saa 10 akitokea ndani ya maji tena kwa kisu,aende tu mahakamani akauzuie uchaguzi,kwa sababu hakuna atakachokikosa,si hawamtaki!!!!!!!!!!!.
Hivi kama kamati ya uchaguzi ilishindwa kumshughulikia Wambura kwenye pingamizi alilowekewa,leo hii wanatoa wapi jeuri ya kumuondoa kwa sababu nyepesi kabisa kwamba aliwahi kuondolewa kwenye uchaguzi uliopita?!,hii kitu haingii akilini hata kidogo,inaumiza jamani,najua kwamba Lyato na kundi lake walishindwa kumuondoa wambura kupitia Pingamizi na kuamua kuyatupilia mbali mapingamizi yote kwa sababu tu kuna watu wao akiwemo Nyamlani walikuw wakiguswa kwenye pingamizi walizowekewa,lakini kuna siku inakuja ambapo mbivu na mbichi zitajulikana.
Ntaka niseme ninapozungumzia Kamati ya Lyato naweza kujaza zaidi ya kurasa 200 ya madufu ya TFF,hili halikubaliki,na hawa watu nadhani walikwishalaniwa kwa sababu maamuzi yao ni ya kipuuzi sana......bana hebu ngoja niishie hapa kwa sababu napata hasira tu.....