Masikini MICHAEL WAMBURA!

Masikini MICHAEL WAMBURA!

Msimtetee huyu jamaa kwani aliharibu yeye mwenyewe kwa kwenda kuishtaki simba mahakamani kitu ambacho ni kinyume na katiba ya TFF.Tamaa zake za kuongoza ndio zimemponza hivyo msitafute mchawi. BTW hivi hana shughuli nyingine ya kufanya ukiondoa kufukuzia uongozi ktk soka?

aliishitaki simba sawa inamaana hicho kitu alichokifanya hakina mwisho na kama hukumu ilishatolewa kwa maana hiyo hakuna kesi halafu angalia ujinga waliofanya kipengele kimoja kina sababu zaidi ya moja ulishaona wapi na hakuna a wala b mi naona hao kina lyato wanayao ila sio kusema watu hawana ufahamu na ninachoona ni fifa kuingilia kati na hao mende wote wanaoichafua tff wapigwe chini zaidi ya hapo tutaendeleza ushuzi uliopo..
 
nayeye si akimbilie kwenye siasa kama rage kama uongozi wa TFF na CLUB ya simba vimegoma?
 
minaona ambao hamtaki wambura ni wale wanaogopa kuumbuliwa kama yeye walivyo muumbua na chengine kwa nini wasitoe hukumu na sababu za msingi ili hata akiwa na mawazo hayo ashindwe lakufanya kuliko kujitia kafanya madudu wakati waliopo sasa tofauti yao na fat ni jina tu..
 
nayeye si akimbilie kwenye siasa kama rage kama uongozi wa TFF na CLUB ya simba vimegoma?

hata akienda huko watamwambia hana vigezo huyu inatakiwa akawafunge wabaya wake wote zaidi ya hapo ataishia kuambia anakosa la kushtaki mwajiri wake waovu wenzake ndio wanaombania..
 
hata akienda huko watamwambia hana vigezo huyu inatakiwa akawafunge wabaya wake wote zaidi ya hapo ataishia kuambia anakosa la kushtaki mwajiri wake waovu wenzake ndio wanaombania..

hata Rage alifungwa kabisa jela, na kwenye siasa alipigwa zenngwe kali.ila baadaye akawa mbunge na kiongozi wa simba.Tatizo la wambura ni king'ang'nizi hataki kurudi nyuma kidogo ili akajipange upya.kidonda cha wabaya wake bado kibichi yeye anazidi kung'ang'ana,ndio maana wabayawake nao wanagongelea hapohapo kwenye jeraha.
 
Mkuu huna haja ya kupoteza muda wako mwingi kumtetea huyu fisadi... kama vp mtafutieni kibarua sehemu nyingine lkn sio TFF. hivi ni mazuri gani aliyoyafanya alipokuwa katibu mkuu wa FAT mpaka leo hii mtoe mapovu kwa ajili ya kumtetea? Hivi unajua kuwa mpaka sasa hajakabidhi ofisi baada ya kuchaguliwa katibu mkuu mwingine pale FAT?

Huwezi kuzungumzia TFF bila wambura.Wambura ndiye anamchango mkubwa wa kuanzishwa TFF.Kwani yeye ndiye alipambana na akina Rage na Ndolanga wakati ule wakiifanya FAT kama ndio yao.lakini nakumbuka huyu jamaa alipambana na Ndolanga bila kuchoka hadi walipoondolewa wote.na ndio hapo akina Tenga walipata mwanya wa kuchukua madaraka.Ieleweke wazi hakunamtu wakati ule alikua anaweza kupambana na Ndolanga,alikua kama Mungu mtu.
Leo hii binafsi yangu naamini wambura ni kiongozi mzuri,kwa viongozi wa TFF wa leo.ni mtu mwenye msimamo.Kilichofanyika ni kuwa ameonewa tu.TFF ni chanzo cha kufeli mpira wa Tanzia, ukichanganya na Simba na Yanga.
 
Hana kingine cha kufanya zaidi ya soka?Si fundi cherehani huyu?
 
Dah! jamaa king'ang'aniz sana huyu cjapata kuona!!!
 
Hivi huyu Wambura hawezi kufanya kazi nyingine isipokuwa uongozi wa mpira tu!!!!!!????????. Jamaa ana roho ngumu aisee
 
SHAFFIH DAUDA NA WAMBURA KWA KWAMA KWENYE CHUJIO LA TFF,WALIOPENYA HAWA HAPA


UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
NA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD)
04/02/2013​


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wananchi wote kwamba baada ya kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF na Tanzania Premier League Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi yafuatayo:

1. TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD​


(a) Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:


[TABLE="width: 516"]
[TR]
[TD]NAFASI INAYOGOMBEWA[/TD]
[TD]S/N0.[/TD]
[TD]JINA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MWENYEKITI WA TPL BOARD[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Hamad Yahya Juma[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Yusufali Manji[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MAKAMU MWENYEKITI WA TPL BOARD[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Said Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MJUMBE –KAMATI YA UENDESHAJI (Management Committee)[/TD]
[TD]
1.[/TD]
[TD]
Kazimoto Miraji Muzo[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]2.[/TD]
[TD]Omary Khatibu Mwindadi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


(b) Mwombaji uongozi Ndg. Christopher Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board Ibara ya 28(2) kwa kuwa cheti chake cha Elimu ya Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imemwondoa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya uendeshaji (Management Committee) ya TPL Board.

2. SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)​


(a) Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF.Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:


[TABLE="width: 552"]
[TR]
[TD]NAFASI[/TD]
[TD]
S/No.​
[/TD]
[TD]
JINA​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]RAIS WA TFF[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Athumani Jumanne Nyamlani[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Jamal Emily Malinzi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
MAKAMU WA RAIS WA TFF[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Ramadhan Omar Nassib [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]Wallace Karia[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MJUMBE WA KAMATI YA
UTENDAJI –
Kanda ya 1 (Kagera, Geita)[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.[/TD]
[TD]Kalilo Samson[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Salum Hamis Umande Chama[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 2 (Mwanza, Mara)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Jumbe Oddessa Magati[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Mugisha Galibona[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]Samwel Nyalla[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4.[/TD]
[TD]Vedastus F.K Lufano[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 3 (Shinyanga, Simiyu)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Epaphra Swai[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Kanda ya 4 (Arusha, Manyara)[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.[/TD]
[TD]Elley Simon Mbise[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Omar Walii Ali [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 5 (Tabora, Kigoma)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Ahmed Idd Mgoyi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Yusuf Hamis Kitumbo[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 6 (Rukwa, Katavi)[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.[/TD]
[TD]Blassy Mghube Kiondo[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Seleman Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 7 (Iringa, Mbeya)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]David Samson Lugenge[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]John Exavery M. Kiteve[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]Lusekelo E. Mwanjala[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 8 (Ruvuma, Njombe)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]James Patrick Mhagama[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Stanley W. D Lugenge[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 9 (Mtwara, Lindi)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Athuman Kingome Kambi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Francis Kumba Ndulane[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]Zafarani Mzee Damoder[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 10 (Dodoma, Singida)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Hussein Zuberi Mwamba[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Stewart Ernest Masima[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 11 (Morogoro, Pwani)[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.[/TD]
[TD]Riziki Juma Majala[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Twahil Twaha Njoki[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Davis Elisa Mosha[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Khalid Abdallah Mohamed[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]Kusianga Mohamed Kiata[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kanda ya 13 (Dar es salaam)[/TD]
[TD]1.[/TD]
[TD]Alex Crispine Kamuzelya[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Juma Abbas Pinto[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]Muhsin Said Balhabou [/TD]
[/TR]
[/TABLE]




(b) Waombaji uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:


(i) Ndg. Omary Mussa Nkwarulo anayeonba kugombea nafasi ya Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.


(ii) Ndg. Michael Richard Wambura anayeonba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura alifungua kesi ya madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba. Kwa kufanya hivyo, Ndg. Michael Wambura alivunja Katiba ya Klabu ya Simba, alikiuka Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA.


(iii) Pia Kamati inaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu uchaguzi mwaka 2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyofikiwa na Kamati hiyo ya Rufaa. Maamuzi hayo yanaweza tu kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).


(iv) Ndg. Abdallah Hussein Musa anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 1 (Kagera, Geita) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.


(v) Ndg. Mbasha Matutu anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 3 (Shinyanga, Simiyu) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa aliingilia mchakato wa Uchaguzi kwa kushirikiana na waweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake.


(vi) Ndg. Charles Mugondo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 4 (Arusha, Manyara) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF kwa kuwa vyeti vyake vya Elimu ya Sekondari na cheti cha Ualimu vina utata.


(vii) Ndg. Ayubu Nyaulingo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 3 inayotaka awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na pia hakukidhi Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.


(viii) Ndg. Nazarius A.M Kilungeja anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa sehemu ya migogoro ya muda mrefu mkoani Rukwa.


(ix) Ndg. Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu mabadiliko ya Katiba.


(x) Ndg. Farid Nahdi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa maelezo ya umri wake na vyeti vya elimu havikubaliani.


(xi) Ndg. Hassan Othuman Hassan anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(5) kwa kuwa hakuhudhuria usaili.


(xii) Ndg. Omary Isack Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa alikaidi maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.


(xiii) Ndg. Shafii Kajuna Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.


3. Usaili uliofanyika kwa waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa zilizoifikia Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na TPL Board.


4. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi wa TFF utafanyika tarehe 24 Februari 2013 jijini Dar es salaam.
 
aliishitaki simba sawa inamaana hicho kitu alichokifanya hakina mwisho na kama hukumu ilishatolewa kwa maana hiyo hakuna kesi halafu angalia ujinga waliofanya kipengele kimoja kina sababu zaidi ya moja ulishaona wapi na hakuna a wala b mi naona hao kina lyato wanayao ila sio kusema watu hawana ufahamu na ninachoona ni fifa kuingilia kati na hao mende wote wanaoichafua tff wapigwe chini zaidi ya hapo tutaendeleza ushuzi uliopo..

wambura labda akanzishe tff yake ndo aingoze ila sio tff yetu watz,.
Hatuwezi ongozwa na mtu asienauwezo kama wambura,. Si mpendi na watanzania wengi hawampendi na sheria za mpira dunian hazimpeni,.
Anataka airudishe tff kiwe kijiwe cha wahuni kama ilivokua FAT hatutokubali.

Kama mnaona anaonewa anzisheni cha tff yenu mumchague awaongoze
 
Kamati ya uchaguz ya SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU (TFF), limempiga chini mheshimiwa huyu asigombee nafas aliyoiomba kwa madai kwamba hana vigezo!!! Jamani mbona wanamuonea sana huyu jamaa, kuna kitu gani pale TFF mpaka wafikie kumuogopa huyu mtu?


Kwani Wambura hana kitu kingine anachoweza kufanya duniani! lazima afanye kazi TFF?! kuna nini pale TFF kinachomfanya atake kufia pale?! ni takribani miaka 20 hivi Wambura anatafuta kazi kwenye chama cha mpira!!!!!!!!!!!!!

Wambura kashone suti Shanghai china; kuna opportunities nyingi kule Wambura; achana na mipra!!
 
Hana kingine cha kufanya zaidi ya soka?Si fundi cherehani huyu?

Hakuzaliwa ndani ya soka, aliishi muda mwingi nje ya soka na aliishi muda mfupi ndani ya soka. Amekuwa nje ya soka tangu FAT ibadilishwe na kuwa TFF! Yapo maisha mengine nje ya soka mfano kilimo, ufugaji, biashara na hata ufundi cherehani. Waungwana hawamtaki, namshauri aachane na kugombea uongozi ndani ya TFF.
 
kama kweli alikuwa ni fundi cherehani basi sishangai kwanini jamaa amekuwa king'ang'anizi.
 
kama kweli alikuwa ni fundi cherehani basi sishangai kwanini jamaa amekuwa king'ang'anizi.

Mkuu fafanua kidogo, ung'ang'aniz wa fundi cherehan ni upi?, maana naona umeingia kwenye taaluma yetu mafundi.
 
Wambura hafai kabisa kugombea nafasi yoyote hapa Bongo kwasababu ni aina ya watu wasiotaka kusikia wala kuelewa ni ving'ang'anizi kama Ndolanga alivyokuwa. Wambura alionywa zamani wakati wa uchaguzi wa Simba kuwa kesi za michezo huwa hazipelekwi mahakamani ila husuluhishwa na kamati za usuluhishi lakini alikataa na akapeleka kesi mahakamani kinyume na taratibu za FIFA iweje leo agombee wakati yeye alisababisha Tanzania karibu kufungiwa na FIFA??? Anavuna alichopanda muda mrefu !! Ajifunze kuacha undolanga hapaaaaaaaa!!!!! Nyau huyo!
 
Back
Top Bottom