Kitu kimoja kinachofanyika katika kuwapata wagombea wa CCM kwenye nafasi mbalimbali ndicho cha hatari zaidi kwa sasa.
Kinachofanyika sasa ni kushughulika na kadi za uanachama.Viongozi wamegundua kuwa wakibadilisha mgombea aliyepitishwa na wanachama kumekuwa na malalamiko.Kinachofanyika ni kuuza zile kadi kwa baadhi ya wagombea wanaowataka washinde.Mgombea aliyenunua kadi atafanya utaratibu wa kuwagawia kadi pamoja na pesa wanachama "fake" ili wampigie kura au atapiga yeye mwenyewe na kuzipenyeza kwenye sanduku la kura.Kwa hiyo,wanachama watashangaa mtu wao hakushinda bila kuelewa kilichotokea.