Masikini hana rafiki...

Kwanza umaskini unaletwa na nini? Je ni ukosefu wa elimu ikiwamo kukimbia umande, uvivu na kutojishughulisha, kuridhika na maisha uliyonayo, kukata tamaa, kutegemea ndugu jamaa na marafiki, etc.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masikini haaminiki, masikini hubadilika haraka cha mwisho masikini lawama nyingi.
 
Tajiri akifirisika au mwenye cheo akibaki hana cheo marafiki humkimbia.

Ndo maana sipendi shobo wala connection isiyoninufaisha ili hata nikifirisika nisipate stress na kutafuta wa kumlaumu eti kanifirisi.
 
Mithali 14:20
[20]Maskini huchukiwa hata na jirani yake;
Bali tajiri ana rafiki wengi.
 
Tajiri akifirisika au mwenye cheo akibaki hana cheo marafiki humkimbia.

Ndo maana sipendi shobo wala connection isiyoninufaisha ili hata nikifirisika nisipate stress na kutafuta wa kumlaumu eti kanifirisi.
Inabidi kuishi mwenyewe mwenyewe tu
 
Inabidi kuishi mwenyewe mwenyewe tu
Kama mtu akiwa rafiki unaapply principle ya wazanaki. Maana ya wazanaki ni umekuja kwangu sasa umeleta nini. Siyo kuniletea tumbo na kunitia njaa kesho nikichoka unicheke.
 
Mkuu,unadhani hii dhana inaweza kubadilika kweli?
Mkuu hizo ni dhana ya kimaskini tu maana hata mm ni maskini inagawa ninishatembea nchi kadhaa Asia na Europe na Nina marafiki matajiri lakini nilivyojiweka wao ndo hunitafuta mm kunisalimia maana washajua mm sijali utajiri wao Bali ni marafiki tu shida inakuja ni pale unapotaka kujifananisha nao na hali yako haikuruhusu kwa iyo tatizo sio umaskini tatizo ni wewe mwenyewe utakavyojiweka tu.
 
Mkuu samahani kwa hiki nachotaka kusema.

Onana na wataalamu wa saikolojia kabla tatizo halijawa kubwa zaidi. Nimekuwa nikifuatilia sana post zako na nyingi unaonekana ukilalamika. Nahisu kuna tatizo linakusumbua ila unatuliza mawazo kwa kupost kinyumenyume.
 
ha ha ha ha relax mkuu, mtandaoni hutakiwi kutumia akili kubwa kufikiri, just for leisure
 
Kuhusu kuwa masikini ni sawa tatizo Sasa hata maono huna mm nitake urafiki na wewe wa kazi gani sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…