Masikini CCM!!!!! Viongozi wa unadi Chanel 10

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,516
1,865
Kumbe Mswaada ulio rudishwa kwa wananchi,baada ya kupingwa na idadi ya watu na wabunge, ambao ulijaa pumba jana niliona waziri Hawa Ghasia na naibu waziri wa sheria na katiba wakiunadi/kuutetea! Eti tusijadili jinsi ya kuandika katiba kwa kujadili nguvu za Rais ni zipi, tume ya uchaguzi kwamba iko imara, na Muungano ujadiliwe kwa kutoguswa muundo wake!!!!!!!!!!!!!! KUMBE WALIKUWA SERIOUS! (it is a sad situation).
Mwenye Mswaa huo auweke hapa

Kabla ya hapo nilimsikia katibu mkuu wa chama cha magamba akifoka kuwa ccm inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, nikaamua kuzima TV na kwenda kulala huku nikijiuliza, watanzania tulikuwa wapi kuweka madarakani watu wasio jua mambo! Hii hali ya kuendelea kuongozwa na watu wasio kuwa na fikra inabidi ianze sasa.
 
Pole sana mkuu. Hawa watu hawajaelewa kwa nini muswada unakataliwa. Walichofanya ni kumtwisha spika mzigo usio wake nae kwa kutojua akakubali.
Muswada ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharura; hivyo spika kuurudisha kwenye kamati ya bunge hakuondoi ule udharura wake. Kimsingi spika na kamati ni kitu kimoja. Spika alipaswa aurudishe kwa aliyeuleta kwa hati ya dharura ili aulete bila hati ya dharura, ambaye ni serikali. Kwa hiyo kinachofanyika hivi sasa ni batili. Aliyeuleta muswada kwa hati ya dharura bado anategemea ushughulikiwe kidharura.
Pili wananchi wameukataa muswada, na kama kweli bunge na kamati zake wanawakilisha wananchi, wanapaswa waukatae; hivyo kukaa nao hadi Juni hakusaidii chochote maana hawana mamlaka ya kuubadilisha.
Tatu, kinacholeta shida ni kwamba serikali imeshindwa bungeni na kama ni hivyo madhira yake ni makubwa sana, yaani iwapo bunge halikubaliani na serikali basi kuna maswala ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya. Haya ndiyo wanajaribu kuyaficha. kimsingi muswada ule haurekebishiki, ni wa kuufuta kwa ujumla wake na kuandika upya. Wananchi tuelewe, huwa kuna marekebisho ya kawaida katika muswada ambayo hushauriwa na wabunge na serikali kukubali kufanya marekebisho hayo kwa kufuata matakwa ya wabunge; hii ni tofauti sana na kilichotokea kwa muswada huu; huu umekataliwa kwa ujumla - na hii ndiyo inaashiria serikali kushindwa bungeni.
 
Eti tusijadili jinsi ya kuandika katiba kwa kujadili nguvu za Rais ni zipi, tume ya uchaguzi kwamba iko imara, na Muungano ujadiliwe kwa kutoguswa muundo wake!!!!!!!!!!!!!! KUMBE WALIKUWA SERIOUS! (it is a sad situation).
.
Muswada ule wameukoroga wenyewe. Lengo ni kuunda tume, lakini ndani yake wakaweka mambo ya kutojadiliwa! Huu ulikuwa upuuzi; kama walitaka hivyo wangevisema katika hatua ya wananchi kujadili katiba mpya wanayoihitaji. Sasa wao walitaka wayaweke halafu tusiyazungumzie?
Hilo changa la macho tumeliona.
Ndugu yangu, nenda katika threads za Katiba mpya utakuta muswada umebandikwa huko
 
SISI EM HAINA nia ya dhati kwa MUSTAKALI wa Taifa letu. Hili linaweza kuthibitishwa na jinsi wamekuwa vigeugeu katika maswala nyeti ya nchi. Uliona Jinsi walivyokuwa wakishabikia DOWANS ilipwe. Si mliona??? Mliona jinsi kwenye kampeni walipinga katiba MPYA si mlionaaaa???
Hawa ni vigeugeu. hawafai kuongoza nchi......Nyie ngojeni Mtakuja Kusikia wakisema swala la katiba mpya ni wao WAMELIANZISHA...si Mtaonaaaa. Wasubiri nguvu ya UMMA. 2015 Hawachomoki......Wananchi washawasoma si mmeona wananchi,wanaharakati,CDM etc walivyoshikia bango huu mswada feki wakaukataa muswada, Ni vizuri pia bunge na kamati zake wanawakilisha wananchi, kwa wao pia kuukataa mpaka mwisho. Mpaka uendane na maslahi ya wananchi.Vinginevyo wanapaswa waukatae. ETI WANAVUA GAMBA....HIVI NYOKA AKIVUA HAMBA ANAKUWA JONGOOOO??????????? NAULIZA WADAU....ANAKUA JONGOO AU ANABAKIA NI NYOKA....HIVI NDO WALIVYO!!!!!!
WAMEVAA NGOZI ZA KONDOO KUMBE NDANI NI MBWA MWITU WAKALI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Muswada ule wameukoroga wenyewe. Lengo ni kuunda tume, lakini ndani yake wakaweka mambo ya kutojadiliwa! Huu ulikuwa upuuzi; kama walitaka hivyo wangevisema katika hatua ya wananchi kujadili katiba mpya wanayoihitaji. Sasa wao walitaka wayaweke halafu tusiyazungumzie?
Hilo changa la macho tumeliona.
Ndugu yangu, nenda katika threads za Katiba mpya utakuta muswada umebandikwa huko

Kwa hili,wananchi na wadau wote wa katiba wamenifurahisha kwa kuhakikisha haipiti ki-yes man.
 
kuna wakati nawapenda sana wale wanaharakati
na lile chama kwa kuhamasisha wanainchi kukomaa

yule mama anatia kichefuchefu sana na litamshuka shuu

kitaeleweka tu
 
Pole sana mkuu. Hawa watu hawajaelewa kwa nini muswada unakataliwa. Walichofanya ni kumtwisha spika mzigo usio wake nae kwa kutojua akakubali.
Muswada ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharura; hivyo spika kuurudisha kwenye kamati ya bunge hakuondoi ule udharura wake. Kimsingi spika na kamati ni kitu kimoja. Spika alipaswa aurudishe kwa aliyeuleta kwa hati ya dharura ili aulete bila hati ya dharura, ambaye ni serikali. Kwa hiyo kinachofanyika hivi sasa ni batili. Aliyeuleta muswada kwa hati ya dharura bado anategemea ushughulikiwe kidharura.
Pili wananchi wameukataa muswada, na kama kweli bunge na kamati zake wanawakilisha wananchi, wanapaswa waukatae; hivyo kukaa nao hadi Juni hakusaidii chochote maana hawana mamlaka ya kuubadilisha.
Tatu, kinacholeta shida ni kwamba serikali imeshindwa bungeni na kama ni hivyo madhira yake ni makubwa sana, yaani iwapo bunge halikubaliani na serikali basi kuna maswala ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya. Haya ndiyo wanajaribu kuyaficha. kimsingi muswada ule haurekebishiki, ni wa kuufuta kwa ujumla wake na kuandika upya. Wananchi tuelewe, huwa kuna marekebisho ya kawaida katika muswada ambayo hushauriwa na wabunge na serikali kukubali kufanya marekebisho hayo kwa kufuata matakwa ya wabunge; hii ni tofauti sana na kilichotokea kwa muswada huu; huu umekataliwa kwa ujumla - na hii ndiyo inaashiria serikali kushindwa bungeni.

Hoja yako nzito big up. Ombi langu kwako hoja hii uisambaze pamoja na hapa, na nje ya hapa kwa wasomaji wengi na wananchi hata kwa wabunge kama wanapokea maoni. Najua wa CDM WANAPOKEA MAONI
 
Kwa hili,wananchi na wadau wote wa katiba wamenifurahisha kwa kuhakikisha haipiti ki-yes man.

Nakwambia kwa mara ya kwanza kuna wimbi la uelewa wa wananchi usiotiliwa shaka na wa haraka. Wananchi wanatoa ushirikiano kwa hoja yenye kueleweka. Thanks. CDM hiyo opportunity ya sasa hivi; sisi wengine tunatoa michango yetu hapa kwa mategemeo mtaongoza mabadiriko kwa kuzingatia na kuchambua hii michango yetu.
 
Back
Top Bottom