Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 13,244
- 26,521
My people,
Huyu ni mwandishi wa habari na mwanaharakati wa Iran ambaye naye kama alivyo Kimambi anaishi MarekaniAkihojiwa na NBC News anasema familia nyingi za viongozi wakubwa wa Iran wanaishi Marekani,anahoji kama wanawatendea ubaya wananchi wa nchi hiyo basi na familia zao nao zirudi Iran ili wote wateseke
Anasema serikali ya kiislamu ya Iran ni kama Kansa ambayo inaitafuna dunia nzima,anaendelea kusema kwamba wananchi wa Iran sio kwamba tu wanajikomboa wenyewe bali wanaikomboa dunia nzima
Anafurahishwa sana na kauli ya Trump kwamba kama Iran itawaua wananchi wake basi Marekani haitasita kuchukua maamuzi magumu na kuichukulia hatua kali nchi hiyo
Kwa upande wa pili mwandishi wa makala haya Ertugrul bey naye anayakusema:
Pamoja na kwamba siungi mkono harakati nyingi zinavyofanywa na Serikali ya Iran,lakini je Marekani ina mapenzi makubwa na raia wa Iran?
Jibu hapana bali ni kile ambacho wamekuwa wakikipigania miaka yote kwamba Iran inatishia usalama wa mashariki ya Kati
Tena naona sasa ndio wamepata sababu ya uungwaji mkubwa wa wananchi wa Iran,watajifanya wanajali sana hali za wananchi wa Iran lakini behind the curtain wana ajenda yao
Swali ninalo jiuliza je,haya yakitokea hayawezi kuwa kama yaliyotokea Libya?
Hofu yangu huenda yakatokea machafuko makubwa sana na nchi inaweza isitawalike,ukichukulia kwamba bado kutakuwa na watu wenye kutaka IRAN iendelee kuwa na mlengo wa kidini na kuna ambao watataka kuwa nje ya mfumo wa dini au sheria za dini ya kiislamu na kuwa free zaidi
Kiukweli kabisa naona mbeleni huko Iran ambayo itakuwa haina utulivu na iliyojawa na vurugu tele,hapo ndipo wananchi wa Iran watatamani walau wangebakia na Iran yao waliyo izoea pamoja na mbanga zake
Mungu ibariki Mashariki ya Kati na Mungu ibariki Iran
Ni hayo tu!