Safi mkuu kwa Kutumia Fursa
Naona umetupia mfumowa Mwimba na Mjazo.
Nilipiga sana biashara hiyo hapa Zanzibar,hela nzuri sana,nikapeleka kidogo Comoro nako ilikuwa inalipa kweli,ila baadae usafiri ikawa sheeda kwa Comoro.
Kwa mwenye kujua ni shuka nzuri sana na Ngum,maana kama sikosei Plain shuka zake zinatoka Bujumbura,ila nasikia kariakoo wanaleta kwa sasa.Na zinapendeza sana ukutandika.
Hii ni kwa wale wamaridadi wa ndani,sio wale wa kuukabia huku vyumbani kwao aibu.
Ila Ushauri:
Kama ni mfanyabiashara,basi kwanza jua quality ya uzi unaotumika na Plain shukaz.
Nakuambia kwakuwa nimeifanya hiyo biashara kwa 7 yrs miaka ya kuanzia 1995na shemeji yako anazifuma kwa matumizi ya nyumbani,wakati huo nilikuwa nanunua Kigoma na Burundi kwa Tsh:12,000 mie nauza 25,000 mpaka 30,000
Kuna baadhi ya vitambaa vinakuwa sio vizuri ila inabidi uwe makini sana kuvijua,na lazima upate mzoefu akupe njia ya kujua,maana wafumaji wao pia wanaangalia faida,na wanaweza kukuchomekea kimeo,uzi sio tatizo,ila kitambaa chake ndio wengine huchomekea badala ya Genuine wanakupa vile mpwero,ambapo baada ya muda vinapoza nyuzi
Komaa mkuu,biashara nzuri,na jaribu kutanua soko,na unajua hadi mtu atumie ndio atajua raha ya shuka hizi.Zinapendeza mno Kitandania,kuna kipindi nilimpelekea Rafiri yangu Italy,basi alishangaa kuona kwamba zinafumwa kwa mkono.Ukipata mwanya kwa mtu anaeenda Comoro,jaribu kumpa shuka moja kali sana au mawili,ili kuangalia soko lipoje
Maana Comoro wanalipa kwa USDollars,sasa kwa rate yetu ya madafu,inakuwa imesimama vizuri.
All the best,achana na wanaoponda,na ndio hao hao wanaolalamika maisha magum
We si umesikia kwamba Watanzania hasa wa Dar wanatumia asilimia 1% tu ya akili kufikiria.