Mashoga wa China Kutafuta Mrembo Wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashoga wa China Kutafuta Mrembo Wao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">Mashoga wa China Kutafuta Mrembo Wao</td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Hawa si mamiss bali ni mashoga toka nchini mbali mbali duniani walioshiriki mashindano ya mwaka jana kumtafuta mrembo kati yao.</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Friday, December 11, 2009 1:53 AM
  Kwa mara ya kwanza mashoga wa China wanatafuta mrembo kati yao atakayeiwakilisha China kwenye mashindano ya urembo ya dunia ya mashoga.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Mashindano hayo ya urembo yanayokwenda kwa jina la " Mr Gay China" yatafanyika tarehe 15 mwezi wa kwanza mwakani katika mji wa Beijing ili kupata mwakilishi wa China katika mashindano ya urembo ya dunia ya mashoga yatakayofanyika mwezi februari nchini Norway.

  "Kutakuwa na mavazi ya michezo na ya kuogelea na pia kutakuwa na maswali na majibu ambapo mshindi atachaguliwa na majaji maalumu wa mashindano hayo", alisema Ben Zhang, mwanzilishi wa chombo cha habari za mashoga nchini China.

  Washiriki wa mashindano hayo ni mashoga wote wanaoishi nchini China wakiwemo raia wa kigeni.

  Hata hivyo mashindano hayo yanafanyika huku bado wachina wakiendelea kuwabagua mashoga katika kila nyanja.

  Hadi mwaka 2001 ushoga ulikuwa ukitambulika kisheria nchini China kama ugonjwa wa akili.

  Zhang alisema kuwa baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wameweka masharti ya kutopigwa picha kwa kuhofia jamii itakavyowachukulia vibaya baada ya mashindano hayo. Kutokana na hatua hiyo, vyombo vikuu vya habari vya China havitaalikwa kwenye mashindano hayo.

  Kwa kawaida mashoga na wasagaji nchini China huogopa kuzitambulisha tabia zao kwa familia zao.

  Hali hiyo inatokana na sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu ya nchini China ambapo kama mtoto atazaliwa halafu akageuka kuwa shoga au msagaji basi wanafamilia huona ukoo wao ndio unafia hapo na hautaendelea kukua tena.

  Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2005 zilizotolewa na gazeti la China Daily, katika watu bilioni 1.3 wa nchini China, kuna jumla ya mashoga na wasagaji milioni 30.

  Hata hivyo vyombo vya serikali vimekuwa vikikanusha idadi hiyo na kusema kuwa idadi sahihi ya mashoga nchini China ni milioni 15.

  Chini ni linki ya Picha za mashindano ya urembo ya dunia ya mashoga yaliyofanyika mwaka jana nchini Thailand.pichazaidi bonyeza hapa http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3722970&&Cat=2
  </td></tr></tbody></table>
   
Loading...