Mashirika ya kimataifa yawalaani Magufuli, Makonda

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
WADAU wa habari, mashirika ya haki za binadamu na asasi za kiraia zinazojihusisha na utawala wa kidemokrasia katika nchi mbalimbali duniani, zimetoa kauli ya kulaani vitendo vya ukandamizaji wa uhuru wa habari vinavyoendelea nchini Tanzania.

Tamko lao linakuja kufuatia kikao cha siku mbili kilichoketi juzi na jana mjini Kampala, Uganda ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hali ya uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa katika nchi mbalimbali.

Katika tamko lao lililosainiwa na jumla ya mashirika, taasisi na asasi za kiraia 33 wamesema.

“Tunalaani kwa nguvu zote uvamizi haramu uliofanywa na Mkuu wa Mkoa ili kulazimisha kurushwa kwa kipindi ambao ndiyo umesababisha Waziri wa Habari kufukuzwa baada ya kuingilia na kuunda tume ya uchunguzi dhidi ya suala hilo.”

Itakumbukwa kuwa tarehe 17 Machi, mwaka huu saa nne na dakika 40 usiku, Paul Makonda (Daudi Albert Bashite) aliongoza uvamizi katika kituo cha utangazaji cha Clouds Media akiwa na askari sita wenye silaha, kilazimisha kurushwa kwa video inayohusu mwanamke anayedaiwa kuzaa na Askofu Josephat Gwajima.

Nape Nnauye, waziri wa habari alilaani tukio hilo baada ya kukitembelea kituo hicho na kuunda tume ya uchunguzi iliyoongozwa na Dk. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali. Hata hivyo Nape alifukuzwa kazi siku moja baada ya tume hiyo kukabidhi kwake ripoti iliyomtia hatiani Makonda.

“Vitendo vya mkuu wa mkoa, na kufukuzwa kwa waziri aliyepinga uvamizi katika kituo cha Clouds Media ni kinyume na sheria na Katiba ya Tanzania.

Tunamtaka rais wa nchi hiyo kuzuia uvamizi dhidi ya vyombo vya habari na hata kuvamia mashirika ya watetezi wa haki za binadamu,” imesisitiza taarifa hiyo.

Tamko la asasi za kiraia na wadau wa habari mbalimbali pia limelaani vitisho vya Rais John Magufuli dhidi ya vyombo vya habari visivyoandika kulingana na matakwa ya serikali na kusema kauli za vitisho za kiongozi huyo hazikubaliki.

“Rais Magufuli ameyatisha magazeti na TV zisizoripoti habari za serikali kama serikali inavyotaka. Tangu kuingia kwa utawala mpya, Tanzania imeshuhudia kuminywa kwa uhuru wa kujieleza na kuhatarishwa kwa uhuru wa wanahabari.

“Zaidi ya matukio 40 ya ukamataji na unyanyasaji wa wanahabari yameripotiwa kufanywa na na wakuu wa wilaya kwa kipindi kisichozidi miaka miwili,” imesema taarifa hiyo.

Miongoni mwa mashirika yaliyotoa tamko hilo la pamoja ni Shirikisho la kimataifa la wanahabari la Ubelgiji, taasisi ya vyombo vya habari vya Ghana, Chama cha waandishi wa habari wa Rwanda, chama cha waandishi wa habari wa Cameroon na kituo cha mafunzo ya vyombo vya habari Liberia.

Mengine ni Chama cha wanahabari wa Guinea, chama cha taifa cha wanahabari wa Tunisia, taasisi ya maendeleo ya sekta binafsi na za umma ya Nigeria, Mtandao wa Taifa wa Taasisi za Haki za Binadamu Kenya, taasisi ya haki ya kujua (right to know) ya Afrika Kusini.
 
Sisi wenye akili tulishasema kuwa hapa tuna mtu mwenye vision ndogo, ambae amekosa diplomasia na uwelewa mpana wa ulimwengu ulivyo.
Lkn shida unakuja kwa vikaragosi wake, walamba viatu wanaojali sana tumbo kuliko haki wako ndio wasifiaji makubwa.
 
Bashite ilionekana ni issue ndogo lakini huenda ikamuathiri sana JPM ndani na nje ya chama, nchini na duniani!
 
Haovwaliotoa hayo ni op wa hizo nchi, je rwanda kuna nn kuhusu hbr? Kagame mshikahi wa mkulu wala hana mda na mambo yao kama hayo, ni mishe zinazochezwa na op party ili kufikisha ujumbe waache uoga waendelee kupambana kama kweli wanamaanisha kuliko kutumia watu wa nchi zingine
 
WADAU wa habari, mashirika ya haki za binadamu na asasi za kiraia zinazojihusisha na utawala wa kidemokrasia katika nchi mbalimbali duniani, zimetoa kauli ya kulaani vitendo vya ukandamizaji wa uhuru wa habari vinavyoendelea nchini Tanzania.

Tamko lao linakuja kufuatia kikao cha siku mbili kilichoketi juzi na jana mjini Kampala, Uganda ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hali ya uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa katika nchi mbalimbali.

Katika tamko lao lililosainiwa na jumla ya mashirika, taasisi na asasi za kiraia 33 wamesema.

“Tunalaani kwa nguvu zote uvamizi haramu uliofanywa na Mkuu wa Mkoa ili kulazimisha kurushwa kwa kipindi ambao ndiyo umesababisha Waziri wa Habari kufukuzwa baada ya kuingilia na kuunda tume ya uchunguzi dhidi ya suala hilo.”

Itakumbukwa kuwa tarehe 17 Machi, mwaka huu saa nne na dakika 40 usiku, Paul Makonda (Daudi Albert Bashite) aliongoza uvamizi katika kituo cha utangazaji cha Clouds Media akiwa na askari sita wenye silaha, kilazimisha kurushwa kwa video inayohusu mwanamke anayedaiwa kuzaa na Askofu Josephat Gwajima.

Nape Nnauye, waziri wa habari alilaani tukio hilo baada ya kukitembelea kituo hicho na kuunda tume ya uchunguzi iliyoongozwa na Dk. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali. Hata hivyo Nape alifukuzwa kazi siku moja baada ya tume hiyo kukabidhi kwake ripoti iliyomtia hatiani Makonda.

“Vitendo vya mkuu wa mkoa, na kufukuzwa kwa waziri aliyepinga uvamizi katika kituo cha Clouds Media ni kinyume na sheria na Katiba ya Tanzania.

Tunamtaka rais wa nchi hiyo kuzuia uvamizi dhidi ya vyombo vya habari na hata kuvamia mashirika ya watetezi wa haki za binadamu,” imesisitiza taarifa hiyo.

Tamko la asasi za kiraia na wadau wa habari mbalimbali pia limelaani vitisho vya Rais John Magufuli dhidi ya vyombo vya habari visivyoandika kulingana na matakwa ya serikali na kusema kauli za vitisho za kiongozi huyo hazikubaliki.

“Rais Magufuli ameyatisha magazeti na TV zisizoripoti habari za serikali kama serikali inavyotaka. Tangu kuingia kwa utawala mpya, Tanzania imeshuhudia kuminywa kwa uhuru wa kujieleza na kuhatarishwa kwa uhuru wa wanahabari.

“Zaidi ya matukio 40 ya ukamataji na unyanyasaji wa wanahabari yameripotiwa kufanywa na na wakuu wa wilaya kwa kipindi kisichozidi miaka miwili,” imesema taarifa hiyo.

Miongoni mwa mashirika yaliyotoa tamko hilo la pamoja ni Shirikisho la kimataifa la wanahabari la Ubelgiji, taasisi ya vyombo vya habari vya Ghana, Chama cha waandishi wa habari wa Rwanda, chama cha waandishi wa habari wa Cameroon na kituo cha mafunzo ya vyombo vya habari Liberia.

Mengine ni Chama cha wanahabari wa Guinea, chama cha taifa cha wanahabari wa Tunisia, taasisi ya maendeleo ya sekta binafsi na za umma ya Nigeria, Mtandao wa Taifa wa Taasisi za Haki za Binadamu Kenya, taasisi ya haki ya kujua (right to know) ya Afrika Kusini.
Watu wanatafuta mkate wa kila siku siyo kupayuka na kuropoka mitandaoni!!
 
Hivi hawaoni aibu kusemwa semwa kuwa wahovyo ndani ya mwaka mmoja?
Au wanasikia raha kwa vile wapo mazombie anaoshangilia kila kiachofaywa?
Mie nadhani siku hawa watu wakipita pale Mirembe na wale waliopo mle wakisjangilia jembejembe! Wataona wao ni babu kubwa tuu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huu ni uzushi. Taarifa ya ikulu haikusema kosa la nape. wamapta wapi hizo taarifa
 
Acha propaganda na uzushi,we mkubwa na unategemewa na familia yako ujue? Sasa unapoleta utoto wa namna hii ni hatari sana
 
Back
Top Bottom