Wizara ya Afya angalieni hizi saluni za kunyolea nywele na maambukizi ya UKIMWI

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Nimetembelea baadhi ya saluni hapa jijini Dar saluni na kuangalia jinsi wanavyotoa huduma za kukata nywele kwa wanaume na baadhi ya wadada nimeshtuka kidogo.

Nakumbuka huko nyuma wakati wa ufunguaji wa saluni walitakiwa kufuata maelekezo ya hasa namna gani ya kuhakikisha wanawalinda wateja wao na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Lakini nadhani hakuna tena ukaguzi kwa hizo saluni kwa mamlaka husika na kuna watu na uhakika kabisa wanaweza kuwa wanaambukizwa baadhi ya magonjwa ya ngozi hata na damu kupitia mashine za kunyolea nywele na ndevu.

Saluni nilizotembelea hazina kabisa kama mashine kadogo kwa autoclave ambako kanasaidia kuua wadudu baada ya mashine kutumika kwa mtu mmoja.

Sasa niliyoyakuta huko ni kuwa machine inatumika kwa mtu mmoja theni inafutwa na kitambaa then mteja mwingine ananyolewa sijui kama hapo kuna kupona mtu kama yule wa kwanza anaambukizi ya ugonjwa wowote ule wa damu au ngozi.

Nadhani mamlaka husika zipite na kufanya ukaguzi katika hizi saluni kuangalia kinachofanyika otherwise kuna janga la wengi kupata magonjwa ya kuambikizwa bila wao kujua.

Nakumbuka kuna watoto wawili wadogo wa familia moja waliwahi kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa njia ya kunyoa saluni baada ya afya kuanza kuzorota na kuchekiwa wakati wazazi wao hawakuwa na UKIMWI ndipo daktari akauliza kama wanatumia saluni na akasema kuna uwezekano mkubwa wamepata UKIMWI huko saluni.

Ukipitia hapa Africa Health Science ya Makerere Medical School utakutana na baadhi ya wataalam waliofanya study barbeshops n kufikia hitisho hilo hapo chini.

Conclusion
This study has revealed that barbering procedures in Nigeria, particularly in the study area, present the risk for HIV transmission through the use of non-potent disinfectants and improper handling of sharp instruments. The same invasive instruments were used on asymptomatic sero-positive and uninfected individuals. In addition, there were blade-to-scalp contacts in all the sessions.

Therefore, barbers could serve as a potential core group for indirect transmission of HIV in the general population.

This should be of great concern and calls for prompt and target-group oriented interventions. To effectively control HIV/AIDS in Nigeria, a comprehensive approach has to be adopted with the involvement of all relevant sectors and groups. Barbers should not be left out.

It is therefore recommended that enough attention should be given to hygiene practices in barbershops through routine supervision and monitoring by agencies of the government.

In addition, practical-oriented training should be organized for the barbers on equipment decontamination with emphasis on the use of correct procedure and potent decontaminant.

All these can be organized through the barbers' union using peer education' approach.
 
Je hakuna research iliyofanyika juu ya hizi machine za kunyolea kwa kuzingatia mazingira halisia yaani kisafishio ni spirit wakati mwingine ni sponge au kitambaa
Na kama bado wewe umepata wapi hizo takwimu ikiwa ni za kweli kwa nini serekali isishtakiwe kwa kuruhusu usambazaji wa virus coz saloon zinalipiwa kodi inamaana ni biashara halali ya kuambukiza virus
 
Wafanyabiashara hao walishapewa elimu namna ya kufanya lakini si wote wanaozingatia hayo maelekezo....serikali hailaumiwi ila ujinga wako na wa mwingine ndiyo wa kulaumiwa.
 
Wafanyabiashara hao walishapewa elimu namna ya kufanya lakini si wote wanaozingatia hayo maelekezo....serikali hailaumiwi ila ujinga wako na wa mwingine ndiyo wa kulaumiwa.
Ok kama serekali hailaumiwi ulishaona mtu akipiwe TIN number kwa ajili ya biashara ya gongo
Kuna TFDA kuna bibi na bwana afya wanalipwa mshahara kazi yao ni kuhakikisha yote yanatekelezwa je unayajua hayo
Usikurupuke hili ni jambo nyeti ni jukumu lako na mimi pia serekali kwa ujumla kuhakikisha hili lisiwepo
 
Barbershops wako makini sana na kazi zao kiukweli......hapa naongelea jamii kubwa ya watz wnaotumia hizo cutz saluni athari ikoje......?

kwa kweli hyo ndio changamoto sbb wateja wanalipa buku per head hana budi service yake iandane na bei. Imagine atanunua vipi zile neck-covers, sterilizer umeme, after shave, powder. Hapo ndio utakuta unanyoa lile shuka halieleweki, ukifungwa limejaa jasho, poda yenyewe hakuna au iliyopo sio laini vya kutosha, sometimes after shave unapakwa mafuta ya cherehani. Ndio maana hata videvu vinakua vigumu sometimes.
 
Serikali iliwahi kulitolea ufafanuzi hili swala mpaka kwenye vyombo vya habari kwamba mashine ya kunyoa inakata nywele tu uwezekano WA kuambukiza virus ni almost negligible hata hivyo saluni zinapaswa kuwa na sterilizer machine lakini hizo sterilizer nyingi zipo kama bosheni tu na ni mbovu
 
na ikitokea imekata ngozi inakuwaje na hayo yanatokea.
 
Ok kama serekali hailaumiwi ulishaona mtu akipiwe TIN number kwa ajili ya biashara ya gongo
Kuna TFDA kuna bibi na bwana afya wanalipwa mshahara kazi yao ni kuhakikisha yote yanatekelezwa je unayajua hayo
Usikurupuke hili ni jambo nyeti ni jukumu lako na mimi pia serekali kwa ujumla kuhakikisha hili lisiwepo
Tatizo letu ni kila kitu kuilaumu serikali...wakati wewe unaona kabisa mazingira haya utapata ukimwi na wewe unaingia kichwa kichwa halafu unataka kuilaumu serikali.

Kwani hakuna anayejua kuwa gongo ni pombe haramu lakini unaenda kunywa kwa kijificha ukipata madhara unailaumu serikali kama si ujinga wako ni nini.
 
Wafanyabiashara hao walishapewa elimu namna ya kufanya lakini si wote wanaozingatia hayo maelekezo....serikali hailaumiwi ila ujinga wako na wa mwingine ndiyo wa kulaumiwa.
Mbona kwenye kodi watu wanapewa elimu ya kodi na bado usimamizi wa ukusanyaji upo?eti ujinga wako..
 
Mbona kwenye kodi watu wanapewa elimu ya kodi na bado usimamizi wa ukusanyaji upo?eti ujinga wako..
Katika huduma za kiafya nikueleze ujue tu serikali ni ya mwisho kuipa lawama....mambo yote yanaanza na wewe.unakula bila kunawa unailamu serikali na maji yapo.unafanya sex bila condom na mtu usiyemjua bado utailaumu serikali ukipata magonjwa ya ngono na ukimwi,unalala bila chandarua unaumwa mbu na kupata malaria unailau serikali kivipi,mambo mengi ya afya yanaanza na wewe.ujinga wako unaweza kuchangia kupata maradhi.
 
Yote hayo pamoja na lawama kwa watu wenyewe lakini serikali bado ina mzigo wake pia,watu wakifa kwa kipindupindu serikali lazima iulizwe pia,ndio maana Kuna taratibu hata za usafi,ukusanyaji taka,uchimbwaji mitaro n.k,hata ugawaji wa vyandarua kwa eananchi Au vile vile yote hayo inawezekana Ni ukosefu wa elimu kwa hawa watu ambapo serikali inahusika pia,acha ubishi wa kishamba,sikatai watu mmoja mmoja kuwa responsible lakini kwa ujumla wetu macho pia yapo kwa serikali
 
Back
Top Bottom