Mashine Za EFD Kwenye Mapenzi

Mashine Za EFD Kwenye Mapenzi

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,309
Hasa eneo la Mahari, Sherehe na uuzaji wa Ngono.

Kutokana na biashara ya mapenzi kushamiri na makahaba kudai watambuliwe na kuheshimiwa sasa TRA tunaomba muwatambua na katika awamu ya Tatu ya ugawaji wa mashine za EFD lazima iwapitie.

Katika eneo la MAHARI itawalazimu wale wanaooana kupata stakabadhi za TRA ili kulipa kwani Sherehe nyingi huanzia kiwango cha 10,000,000/- hivo taifa litapata mapato yaliyotukuka.

Ushauri. Kwa wanandoa kuepuka gharama za EFD Tuepuke michepuko ukishindwa dai risiti.

Mgomo wa Eneo hili ni Mtamu sana.
 
Back
Top Bottom