Mashine za bakery zinauzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine za bakery zinauzwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by TZ biashara, Aug 27, 2012.

 1. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  12 (1).JPG 12 (4).JPG 12 (2).JPG P1000030.JPG 95160.jpg !BfqWho!!Wk~$(KGrHqEH-DMErc6Ln_HIBLCSCeeTVQ~~_12.jpg !Blbnn+Q!2k~$(KGrHqUH-EUEtt50vHjjBLbtF5GSPg~~_12.jpg P1030444.JPG $T2eC16ZHJG8E9nyfoUByBQM7)JR,zw~~60_12.jpg 8da1_12.jpg Nauza mashine za bakery ambazo nilinunua uingereza zilizotumika.Mashine hizi nilinunua kwa ajili ya kuzifanyia kazi lakini sikufanikiwa kufungua kutokana na sababu zisizo zuilika na matokeo yake kupata hasara.Hivo naziuza zote kwa jumla ili kukamilisha bakery nzima na tayari kwa kuanzia kazi.Zinahitaji usafi kiasi na labda servise ili ziwe na uhakika zaidi kwa matumizi.Mashine hizi nimenunua katika hali yakuwa zinafanya kazi kutokana na kufungwa kwa bakery lakini sijawahi kuziwasha kwa muda wa miaka miwili kutokana na kutoelewana mtu ambae alitaka tufanye nae kazi.Na hivo kushindwa kuendelea na ndoto yangu.Tatizo kubwa ni picha sijaweza kuziweka lakini kama hajatokea mtu bado nita lirudisha tangazo hili na pengine nitafanikiwa kuziweka baadhi ya picha kutokana na sehemu zilipo sio rahisi kuzipiga picha.Kusema ukweli ni biashara nzuri sana hasa sehemu za mipakani kama Tunduma Mbeya ambapo ndipo nilikua ndoto yangu kufanyia na ushauri nilioupata kwa wenye uzoefu wa biashara.Mashine nilizonazo ni...

  -OVEN kubwa mbili zenye deki 4 na ni pana zenye kutumika kiwandani

  -MIXER mashine kubwa 2 za kukandia unga ambazo zina ukubwa tofauti na nitaweka vipimo baadae

  -MOULDER mashine moja ya kutengenezea au kukata na kupima kama sikosei scones( Record 30 piece automatic bun divider moulder)

  - MASHINE moja ya kukatia mikate

  -FRENCH BREAD MACHINE moja (kutengeneza mikate mirefu) au Turni Pinner Finger Moulder

  -MOULDER mashine moja ya kutumia mkono ya kuweka mezani

  -PROOVER mashine au kama chumba cha kuumulia unga yenye ukubwa wa fidge au kuizidi kidogo kwa urefu

  -Plastic za kuwekea mikate kama sikosei 20 au 25

  -TREYS za kupikia mikate ambayo idadi yake nimeisahau na nimeshindwa kuingia stoo kutokana na nafasi ndogo

  Hivi vitu vyote thamani yake ni kubwa kuliko bei ninayoiuza kwasababu ya hasara nahitaji milioni 35.Tatizo lingine ni OVEN moja lipo Dodoma na vitu vingine vipo DAR.Naomba kwa mwenye kuhitaji vifaa hivi anitumie ujumbe kupitia PM kutokana na kutokuwepo nchini na baadae nitaweza kumpa contact ya uhakika.
   
 2. R

  Richard Nguma Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba email yako please
   
 3. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Weka picha pls!
  Na hiyo machine iko wapi?
   
 4. C

  Chaka Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  tupe bei pls
   
 5. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Bei mbona kaweka hapo juu mkuu?
  Ok ni 35m!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Naomba usiuze ili miye nichukue nafasi ya huyo mtu........ni PM Terms of References
   
 7. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Samahani mkuu kuhusu picha nitajaribu kuweka kwasababu sijapata picha iliyo nzuri kutokana na nafasi ktk stoo ni ndogo mno na sijaweza kupata picha nzuri,ila natafuta picha kama nilibahatika kuwa nayo kabla hazijaingizwa stoo.Picha moja ninayo ambayo nimeipiga kwakuwa ipo Dodoma.

  Vitu hivi vipo Dar na Oven moja lipo Dodoma.
   
 8. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimebahatika kupata picha hizi
   
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,500
  Trophy Points: 280
  Pole kwa kuuvaa mkenge sisi waswahili porojo nyingi matokea tunaingizana hasara bila kutarajia.Haya mambo ya biashara kubwa yanahitaji mwenyewe usimamie,la sivyo mkenge lazima uuvae,watu hupenda easy money hawajui myu ulivyojipinda
   
Loading...