Mashindano ya urembo sio ajira bali ni wito

Gideerast

Member
Jun 27, 2015
56
3
Tofauti na washiriki na washindi wa mashindano ya urembo katika mataifa mengine duniani, hapa Tanzania iko dhana potofu miongoni wa washiriki,waandaaji na hata mamlaka za usiamizi, kuwa ushiriki wa mashindano au ushindi wa mataji ya urembo ni ajira/

Dahana na imani hiyo potofu,iekuwa ni moja ya sababu kubwa ya kudorora kama sio kufa kupumulia mashine. Bahati mbaya zaidi dhana na imani hiyo potofu imejengwa na waandaaji na malaka za usimamizi,kama moja ya uhalalishaji wa mashindano hayo nchini, na kuwafanya washiriki kushiriki kwa sababu ya zawadi,au matarajio hewa ya utajiri.

Urembo ni wito unao tokana na msukumo nafsi (Platform) juu ya jambo ambalo mhusika anaguswa nalo katika jamii (fano - Ukeketaji,Ndoa za Utotoni,Uwindaji Haramu,Rushwa,Ubaguzi wa Kijinsia,Uharibifu wa mazingira n.k).Ambapo husika hutafuta taji husika la urembo kama jukwaa au hadhi ya kufikisha ujumbe wake kwa jamii,au fursa ya kusaidia jambo analoguswa nalo katika jamii.

Washiriki wa Tanzania ,wameainishwa katika zawadi na vifuta jasho,lakini pia wameainishwa kuwa wakishinda au kushiriki mashindano basi wanakuwa wametajirika na kuyapatia maisha. Kinyume na matarajio yao hujikuta wakiingia katika tabia na mienendo iliyo inyume na maadili.

Ujio mpya wa miss utalii Tanzania,hautoruhusu hali hii kuyakumba mashindano yetu, na kuwa na washiriki ambao fikra zao zinaishie kwenye zawadi.

Haya ni aneno niliyo yapata kutoka kwa oja wa viongozi wa juu wa mashindano ya miss utalii Tanzania,leo hii,abaye hakutaka kutajwa jina.
 

Attachments

  • Welcome To miss Tourism Tv(360p).MP4
    758.3 KB · Views: 42
Aisee, sometimes hayo mashindano ni zengwe, uhuni na maslahi binafsi ya watu
 
Back
Top Bottom