Mashindano ya draft kutafuta bingwa wa mkoa Tanga, Mtaleban apewa ushindi wa mezani

ilala yetu

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
1,237
1,919
Wakuu nipo mkoani Tanga nilikuja kwa shughuli maalum ya kushuhudia pambano Kali la kutafuta bingwa wa draft mkoa tanga fainali siku ya Jana jion ilitakiwa kupigwa Kati ya bwana Mtaleban dhidi ya dogo yassin.

Duru zote zilikua zinaonyesha kua bwana Mtaleban angeenda kuutema ubingwa wake wa mkoa kwa kijana anaechipukia kwa Kasi ya ajabu kwenye ma draft dogo Yassin.

Kilichotokea jana wengi wamekihusisha na imani za kishirikina Kwan dogo yassin alishindwa kabisa kuwasili ndani ya muda na refa na makamisaa kuamua kumpa ushindi wa mezani bwana Mtaleban na kulamba kitita Cha shiling laki1.

Hakika ni mechi iliyovuta hisia za watu wengi Sana jijini tanga na mikoa ya jirani.

Fainali hiyo ilitakiwa kufanyika mabanda papa round about ya mjini.. maeneo hayo ya Mabanda Papa palifurika vyakutosha wat waliokua na shauku kubwa ya kushuhudia pambano Hilo la kihistoria kabisa hivyo kitendo Cha mchezo kuvunjwa kiliwanyong'onyesha sana wapenzi wa mchezo huo.

Katika hatua nyingine bwana Hussein bingwa morogoro Kama mualikwa kwenye mashindano hayo alifanikiwa kutwa nafasi ya mshindi wa tatu baada kumfunga ndugu kitojo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom