Mashetani ndani ya miili ya binadamu

Mashetani ndani ya miili ya binadamu

Kiwalani finest

Senior Member
Joined
Jul 6, 2024
Posts
116
Reaction score
85
MASHETANI HUVAA MIILI YAKAWA KAMA BINAADAMU
HULA VIAPO NA KISHA
HUISHI KINYUME NA VIAPO YAKIWA MAKALI
KINYUME NA MAELEKEZO YA MWENYEZI MUNGU KUHUSU UTII NA UNYENYEKEVU
HAYO NDIYO MASHETANI

Nakumbuka Tarehe 01/06/2021
Dkt Josephat Mathias Gwajima
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima
Na Mbunge wa Jimbo la Kawe
Alisema
Roho yeyote inaweza kugeuza umbo ikawa chochote inachokitaka iwe.
Chochote ambacho ni roho kinaweza ( kujibadilisha) kikawa na umbo lolote kinachotaka chenyewe.
Kwa mfano
Malaika walikwenda kwa ( Nabii ) Ibrahim.
Ni Malaika
( Ila) wakaamuwa ( kujibadilisha) kuwa ( Kama ) watu.
Binaadamu
Wakala Chakula
Wakaoga na Maji
Lakini ( walikuwa ) ni Roho .
Unaona Malaika wakiingia Sodoma na Gomora wakaamuwa ( kujibadilisha) kuwa watu .
Utaona Mahali fulani kwenye Biblia ,
Malaika Hawa hawa ( wamejibadilisha) wamekuwa askari.
Ni Malaika lakini ni askari .
Ana buti
Ana Bunduki
Lakini ( muonekano wa Malaika ) ni Askari.
( Hapa) tunajifunza
Malaika wanaweza kugeuka kuwa Chochote wanacho taka kwa ajili ya kutimiza makusudio Yao .
Mwisho wa kunukuu
Professor Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania
Akitoa Darsa Tarehe 26 /03/2025
Alisema
Hawashuki Malaika ( bila ya kuwa na miili ya Kibinaadamu) ila katika sura za Kibinaadamu.
Kama Wakati wa Mtume alikuwa akishuka Jibril katika sura ya mtu Mmoja akiitwa DihiyatulKaldy.
Mitume nao walikuwa wakishukiwa na Malaika kwa sura nzuri ( za Kibinaadamu )
Mwisho wa kunukuu
Ni wazi na Mashetani kwa kuwa ni Roho chafu nayo hushuka yakiwa na miili ya Kibinaadamu
Ndiyo maana
Unaweza kumshangaa mtu
Amesoma saana ila
Kashindwa tu kuelewa sentensi fupi ya Mwenyezi Mungu isemayo wapende wenzio Kama vile uipendavyo nafsi yako
Hapa unakuwa ni migogoro japo Mali si zake ila ana choyo mpaka anahisi maumivu ya moyo huku akijitamkisha neno Mwenyezi Mungu Kama zuga kwa Mafukara na Watumishi wa Umma
Hayo ndiyo Mashetani yaliyovaa miili ya Kibinaadamu.
Ukiona mtu anakula Milo mitatu
Ana maisha Mazuri
Ana magari
Ana majumba
Anang'ang'ania vyeo huku Akiwa na roho mbaya isiyo na huruma kwa Mafukara na Watumishi wa Umma huku akijitamkisha neno Mwenyezi Mungu ujuwe huyo ndiyo Shetani mwenyewe aliyevaa mwili .
Hana Utii kwa Mwenyezi Mungu Wala utii kwa mitume ya Mwenyezi Mungu
Ndiyo maana hapendi kukosolewa na kurudishwa kwenye njia iliyo sahihi kwa ule Ushetani wake ulijificha kwenye kujitamkisha neno Mwenyezi Mungu
Professor Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania
Nakumbuka Tarehe 27/03/2025
Alisema
Mitume yote ni ndugu .
Na Mitume yote imekuja kwa ajili ya Jambo moja ( nalo ni ) kumpwekesha Mwenyezi Mungu Subhahanahu Wataalla.
Katika Uislam ukimkanusha Mtume Mmoja tu( ujuwe wewe ) unakuwa kafiri
Mwisho wa kunukuu
Yesu kristo ametuagiza kuwapenda na kuwajali wengine Kama tuzipendavyo nafsi zetu.
Mtume Mohammad SAW naye anatutaka tuwapende wenzetu Kama vile tuzipendavyo nafsi zetu
Mitume yote inatukataza Uongo ila Nyakati tulizomo Uongo umekuwa ndiyo habari ya mjini
Ukiwa Mkweli unatengwa .
Na Cha kushangaza hata Baadhi ya Viongozi wanashabikia Mambo yenye Uongo huku wakikwepa kutimiza Wajibu waliomuapia Mwenyezi Mungu kuutendea haki.
Tunapowabaini watu wa namna hiyo tunagundua ndiyo Mashetani wenyewe waliovaa miili ya Kibinaadamu na Kisha kutumia michawa kuihadaa Jamii kuwa ni wema huku wakiwa ni Mashetani yapendayo hila na janja janja kuliko haki .
Wana Chuki dhidi ya katiba kanuni Miongozo na Taratibu kiasi kwamba hata wakimsikia mtu anawakumbusha hayo wao humfanya Adui Yao Kwa ule Ushetani ulivyowaganda kiasi Cha kuitamka haki kishetani tu huku wakiichukia haki na kulindana wenyewe kwa wenyewe kwenye maovu na kupongezana
Wewe ni Mtumishi wa Umma
Umeapa
Kuhifadhi
Kulinda
Na kutetea katiba na Sheria za Jamhuri
Unakumbushwa ulipoteleza
Badala ya kujutia ulipoteleza wewe unakuwa na hasira
Hapa ndipo tunapokubaini ya kuwa Wewe ni Shetani uliyevaa mwili wa Kibinaadamu.
Professor Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania
Akiwa katika Mashindano ya Qur aan
Nakumbuka Tarehe 23/02/2025
Alisema
Ghadhabu ikimpata mtu saa nyingine akili pia inatoka na busara inaondoka
Mwisho wa kunukuu
Watu walioondokewa na akili wameondokewa na busara pia wamebaki na Ushetani ndiyo maana wakikumbushwa Ilani katiba kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo wanajawa na hasira kwa ule Ushetani ulivyowazidi nguvu .
Padre Dkt Faustine Kamugisha
Paroko wa Parokia ya Minziro Kagera
Nakumbuka Tarehe 06/04/2025
Alisema
Shetani ni Baba wa Uongo
Shetani ni Mshitaki
Mwisho wa kunukuu
Mashetani yaliyovaa miili ya Kibinaadamu
Na Kisha kujichanganya kwenye Taasisi mbalimbali Mara nyingi Mashetani hayo huwa ni vyanzo vya matatizo.
Yanacho kiongea huwa hakina uhalisia kwenye Matendo
Hayo ndiyo Mashetani ambayo hutumia uelewa Duni wa Mafukara Kama kisa Cha kuchukuwa Mali za Mafukara hao ili kuwafanya Mafukara na Watumishi wa Umma wahisi kuwa Wametelekezwa na Mwenyezi Mungu.
Mashetani hayamuamini Mwenyezi Mungu na ukiyatamkia aya za Mwenyezi Mungu kwa ule unafiki uliowajaa hukuchukia Wewe uliyekumbusha aya hizo
Huu ndiyo Unafiki unaoweza kuubaini kwa Mashetani hao
Hupenda Batili kuliko halali na Mashetani yako tayari kuunganisha nguvu kumkabili anayeongelea aya za Mwenyezi Mungu kwani Mashetani hutumia tu aya za Mwenyezi Mungu kinafiki ili kuficha Ushetani wao
Shekhe Mharamu Rashid Mziwanda
Akitoa Darsa
Nakumbuka Tarehe 13/03/2025
Alisema
Imekuja katika Suratul Tawbah
( Watu ) Wanafiki wao kwa wao ni Nani !?!?
Ndiyo ndugu wenyewe hao
Mwisho wa kunukuu
Professor Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania
Nakumbuka Tarehe 19/03/2025
Akitoa Darsa
Alisema
( Watu ) wale ambao itafika siku ya kiama ( zikawa) nyoyo zao hazina Ushirikina
Hazija Mshirikisha Allah Subhahanahu Wataalla na Wala Hawana Unafiki wa namna yeyote ( ile)
Hao ndiyo Waumini wa sawa sawa hao
Mwisho wa kunukuu
Njia Nyepesi ya kuyashinda Mashetani hayo ni kwa kila mtu
Kujipa muda kusoma Maandiko Matakatifu kwa imani yake .
Kisha
Kusoma Ilani katiba kanuni Miongozo na Taratibu
Na Kisha kusikiliza kwa Umakini Viongozi wetu wakuu wa Kitaifa kwa Kauli zao Chanya .
Na Kisha
Kila Mtu aishie Tanzania
Kujipa muda kusoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26(1)(2) ibara 09 a,b,f, na h na kuziishi.
Tusiwaogope watu wawezao kuuwa Mwili ila wasiiuwe roho
Bali tumuogope Mwenyezi Mungu Muumba wa vyote awezaye kuuwa Mwili na Roho.
Dkt Benson Kalikawe Bagonza
Askofu Mkuu wa Dayosis ya KKKT Karagwe
Nakumbuka Tarehe 23/02/2025
Alisema
Tumuombe Mwenyezi Mungu Baba yetu wa Mbinguni
Uliyetukusanya (hapa) kwa wema wako ...
Unayetuita tusikie neno lako
Tunakusihi
Utujaalie neema ya kutulia ( na ) kutafakari neno lako .
Neno lako ni Kweli
Neno lako ni nuru
Neno lako ni uzima wetu
Yesu Kristo Bwana wetu
Amina
Mwisho wa kunukuu
Nikashtuka Ndotoni katika ulimwengu wa kiroho huku nikiwa nasema tuwabaini Mashetani tutumie Maandiko Matakatifu katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo kuufia Ukweli


Kidumu Chama Cha Mapinduzi


Mathias Mugerwa Kahinga
 
Back
Top Bottom