Masheikhe mpo wapi, Swalat isstisqa'a ili mvua zije kwa wakati...!!

"Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, wakati ule utakapowatesa;
basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao."


1 Wafalme 8:35-36
 
Waandalizi wamelala usingiziiiii weee...
tukijaribu kwa zindua tutaambiwa !!!!
Tatizo ni sisi wenyewe huyo Mwenyezi Mungu harumtaki,
Hali ya sasa duniani sio shwari tena kila uchao twamuudhi anayeturuzuku,
Ulawiti ndio umekuwa mtindo wa kufanya ngono siku hizi ,kijana akitongoza bint lazima amlawiti na bint nae asipolawitiwa wala hajisikii,
Mashoga wanajitangaza kila siku,
Viongozi wamejigeuza miungu watu,
Zinaa ndio mtindo wa maisha ,concubinage imehalalishwa leo hii,
Kama mtoto wako tu akikosea wamuonya na kumkanya asirudie ,akikosea tena wamzidishia adhabu,basi ni hivyo hivyo kwa tuyatendayo.
"umedhihiri ufisadi baharini na nchi kavu,tuwaonjeshe machungu yaliyotendwa na mikono yao"
 
Mimi nafikiri maombi ya mvua yafanyike kwa pamoja dini zote madhehebu yote.
 
New City , ni kweli lakini bado Mungu anasikia maombi yaetu kama tukiamua kurejea kwake, inaanza na wewe, tumrudie Mungu kwa toba na msamaha wa haya maovu yanayoendelea.

"Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao." (1 Nyakati 7:14)
 
Back
Top Bottom