Masheikh wa uamsho ukweli ukoje?

Sasa kwani tuna Mahakama ya Ugaidi Tanzania?

Imeshajengwa mahakama ya Ufisadi, tusubiri mahakama ya Ugaidi
 
Mara nyingi Hawa watu huwa wanatumika kisiasa na baadhi ya mataifa kutoka middle East huku wakiwa wanajificha katika kivuli Cha dini , watu wengi haelewi hilo wanajikuta wanawaunga mkono tu nakutaka waachiwe .

Nikweli nakubali kwamba serikali ya Tanzania Kuna wakati huwa inafanya uonezi na kuonea baadhi ya watu kwa kuwabambikia kesi , ila kwa watu hawa Hapana aisee wanapaswa kubaki huko huko jela maana walikuwa Wanataka kuvuruga amani ya Nchi
Watu wapi ambao serikali imewaonea kwa kuwabambikia kesi ili tupendekeze waachiwe???
 
Wamuulize hayati Aboud Jumbe kuhusu muungano, rais lakini alifichwa kusikojulikana hadi uzee ulipomkuta, sasa wao ni nani watenganishe watu waliochanganya damu?
 
Angalu ww umeenda sawa na kama comments yangu umeisoma vzr nilisema hawa jamaa walipewa kesi ya ugaidi ambayo ushahidi wa moja kwa moja hamna, ila beyond ya hii kesi ni kuwa jamaa walikuwa wanaamsha wazanzibar dhidi ya nchi yao na kukataa kutumika kisisasa wakidai kuwa wanasiasa wanamslai yao, sasa ilipofikia hatua ya kuanza kushisha bendera za vyama na kuweka bendera zao juu serikali ilingilia kati
Unajua kitu kinachoitwa "infiltration" au kutumia "agents provocateurs" . Ni kitendo cha kuchomeka wahuni kwenye legitimate movement ili kudiscredit movement hiyo.
Jiulize, Je ni masheikh ndiyo walioshusha hizo bendera?
Na je makosa hayo ndo ya kuweka watu ndani miaka nane?
Je makosa ya kushusha bendera za vyama hayana dhamana?
Mbona wamekamatwa masheih tupu na siyo raia wa kawaida ambao supposedly ndiyo waliokuwa front kushusha hizo bendera kama kweli hayo matendo yalifanyika?

Kosa la Masheikh wa uamsho ni kuwaamsha Wazanzibar waukatae Muungano kwa sababu waliona hauna maslahi na Wazanzibar!. Sasa kuukataa Muungano kama ni kosa basi liwekwe kwenye hati ya mashitaka ijulikane moja lakini siyo kuwaonea hao Masheikh
 
Watu hawajui huwa, wanaongea ongea tu ,

Niliwahi kusikia story kuwa hata sababu ya Maalim seif kutangulia kuzimu ime sababishwa na hao hao alipokwenda chato na kukutana na jiwe 1 ya agenda yao kubwa ilikuwa ni kuwaachia hao watu wa uamsho ,na jiwe akawa amekubali hilo , deep state ikaona jamaa wanataka kuvuka mipaka wakaingilia kati
Duuh,hii sasa ndo mpya mkuu

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuna mengi sn juu ya ishu ya hawa jamaa ila sitapenda kuyaandika hapa kwa kuheshimu iman za watu wengine. ila jamaa walikuwa htr mnoo nakumbuka siku waliofanya maadamano mie nilikuwa michenzani natokea darajani, dah walileta noma sn aisee walifunga Barabara na wafuasi walichoma moto matairi.
Unajua nini, uamsho kama uamsho hawakuwa na nia ovu na walikuwa na lengo zuri tu la kuwatoa tongo wazanzibari...ila shida ilikuja baadae baada ya wafuasi wao kuanza hizo fujo, japo hakuna shehe hata mmoja aliyewahi kuwaambia/kuwatamkia wafuasi wao wafanye fujo. Lakini pia fujo zilipoanza kutokea hawakuwakemea wafuasi wao... Na hapa ndipo walipojichongea maana ilifikia hatua baadhi ya wafuasi wao wasiojielewa wakaanza kuchoma moto maskani za ccm na kuziba barabara kwa kuweka vigogo, mapira ya moto n.k
 
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri.

Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka Marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?

Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa ndani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Muungano.

Kama mnakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasema Water is incompressible maana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka
Hivi ukijilipua bomu na kuua halaiki unapata thawabu gn?
 
Kwanza kabisa hawa Masheikh wakati wanakamatwa Marais walikuwa ni Kikwete Muislam na Dkt. Shein muislam. Sasa hadi leo Marais ni Samia muislam na Dkt Hussein Mwinyi Muislam.

Lakini kila siku tunasikia hawa Masheikh 'wanaonewa' Kwa kukaa rumande miaka mingi bila kesi yao kupelekwa mahakamani.

Kuna mtu mwenye 'ukweli halisi' Atusaidie? Nini hasa kinaendelea?
Kwan ni wapi walisema walishikwa kwa kutumia sababu za kidini.....?!
 
Pombe zinakupeleka pabaya sana...
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri.

Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka Marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?

Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa ndani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Muungano.

Kama mnakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasema Water is incompressible maana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka
 
Uamsho walikuwa wanapigania muungano wasanzibar wajitawale wenyewe niliwahi kuona video Za mikutano yao wakiongozwa na sheikh mselem ally pamoja na sheikh farid..wasanzibar walikusanyika kwa wingi kuwasikiliza.
 
Mkuu, sioni faida ya muungano kwa wazanzibar, ni heri ivunjwe tu. Huu muungano navyo ona una faida kubwa kwa serikali yetu.

Nachoona kwa hawa ndugu zangu wa bara---Hawa viumbe wa bara wanajua fiika zanzibar ikijitenga watapata misaada mingi kutoka nchi za kiarabu na europe, na vile vile zanzibar itageuka kuwa Dubai ndogo na kuwa tishio barani afrika, in short zanzibar itabadilika, maendeleo yatakuwepo na wananchi watafurahia munoo. Mimi ni m-bara lakini niko nyuma yao kuwasapoti hawa ndugu zangu.

Mkuu, sio kwamba waislamu hawapo wanaopinga muungano usivunjike, naamini kabisa wapo wakishirikiana na wanaopinga muungano huo usivunjwe, ila ni wachache sana + Baadhi ya viongozi wetu watu wa maslahi/kushibisha matumbo yao.

WAISLAMU HAWA-HAWA-Wanajua kuwa Tanzania bara haiwatendei haki wazanzibar ilhali wale ni waislamu wenzao, wanajua kuwa Masheikh wamewekwa ndani lakini wanasapoti waendelee kukaa ndani kwa kufuata mkumbo wa viongozi na pia kwa raia wa kawaida wasiowatakia mazuri masheikh hawa.. hii dhulma tokea utawala wa karume kama sikosei, waislamu/Oman wengi kama sikosei walinyanyasika, walidhulumiwa na wengine kuuawa, ukatili huo ulifanyika chini ya utawala wa Abeid karume wakati huo raisi wa zanzibar akijua ataishi milele., akiwemo na okello from uganda, na kiongozi wa wakati huo bara alikua Nyerere. Hatunao tena.

Waislamu acheni kufuata mkumbo kwakuwa unaishi bara na wale wanaishi visiwani ukajiona uko paradise, lakini kumbukeni wale ni ndugu zenu, na dunia isiwahadae ndugu zanguni mkawasahau na kuwakandamiza wazanzibar na masheikh waliowekwa ndani kana kwamba mtaishi milele hapa duniani. Unafiki ni mbaya sana, na Mungu hapendi tuwe wanafiki. Unapoona ndugu yako ananyanyaswa na kudhulumiwa kuwa tayali kumsaidia kwa chochote ili kumnusuru, na sio kuwapa faida wasio waislamu, hawata kusaidieni chochote, bali wanawachekeni na kuwakebehi, na wanafurahia munavyopondana na kuchekana ninyi kwa ninyi.
Yani wewe ndo kabisa mbaguzi aisee,na ni mdini kweli kweli.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Ipo hv mkuu, uzuri nilikuwepo Unguja kipindi sakasaka hili linatokea, masheikh wa miadhara (uhamsho) wao walikuwa na ajenda yao kubwa ya kuamsha wazanzibar waliolala juu ya swala zima la nchi yao, wao kipindi wapo walikua wanawakumbusha wazanzibar kuwa si ccm wala chadema wala CUF itakayowakomboa kutoka kwenye maisha ya dhiki bali ni kufata mwenendo wa quraan na sunna za mtume.

Hawa masheikh hawakuvutiwa na CUF wala chadema wao walikuwa na sera yao kuwa demokrasia ni ukafiri ndio maana kila walipokuta bendera ya CUF au CCM wao walikua wakizishusha na kupandisha zao ambazo zina rangi nyeupe tupu na maandishi meupe kati yaliyosomeka kwa kiarabu hakuna mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na muhammad ni mjumbe wa mwenyezi mungu, wao wao walikuwa wanaamini kuwa kwa umoja wao basi walikua na uwezo wa kuiforce serikali ya CCM kutoka madarakani na wao kuchukua mamlaka kamili, nakumbuka wakati huo mambo mengi yalijitokeza wanawake waliovaaa nusu uchi walipigwa fimbo sn mitaani na vijana wafuasi wa uhamsho, walipinga sana siasa ndani ya Zanzibar maana wao hawakuwa na chama, wakawa wanadamana kudai mamlaka kamili ndiipo serikali iliposhtuka na kuona hawa watu wakiachiwa mambo yataharibika Muda si mrefu ndio ikabidi wakamatwe.

Na ndio wakati huo huo viongozi baadhi wa makundi ya kijihad waliwakebehi uhamsho kwa style yao ya kutaka utawala utolewe na kuuita style za kizamni bimana kwenye uislam hakuna maandamano , hivyo walitakiwa washike silaha na kuutoa udhalimu. Note sina uhakika sn inavyosemekana kukamaktwa kwa wale watu agizo lilitoka marekani na kusema hao watu ni htr sn hvy wakamatwe kwa makosa ya ugaidi wapo wanaodai kuna viongozi wa uhamsho walifanya training kandahar, na wakati huo raia wa kigeni huko zenji kipindi cha uhamsho walikutwa na madhira mengi sana like kumwagiwa tindi kali na kufanyiwa vitendo visivyofaa. hayo ndio yaliyowasibu uhamsho hadi leo America wanatazama kwa jicho la mwewe if watatoka au laa kesi ngumu.

View attachment 1750627
Na waozeeee hukohuko
 
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri.

Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka Marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?

Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa ndani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Muungano.

Kama mnakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasema Water is incompressible maana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka
Hivi Kati ua watu wa Tanganyika na Zanzibar watu wa aina gan ndio wananufaika na muungano?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom