Masharti ya mikopo ya kibiashara yapunguzwe

jeff mahugi

Member
Jul 15, 2021
7
16

ILI KUFIKIA MAENDELEO KITAIFA MASHARTI YA MIKOPO YAPUNGUZWE KATIKA TAASIS ZINAZO JIHUSISHA NA MIKOPO​

Habari zenu ndugu na jamaa nikiwa kama kijana ninaye itakia mema nchi yangu napenda kutoa ushauri kwa taasis zinazo jihusisha na mikopo na serikali kwa ujumla. vijana wengi wanao toka katika familia maskini tunashindwa songa mbele kiuchumi kutokana na masharti magumu katika taasis hali ambayo inadidimiza maendeleo kwa taifa. yafuatayo ni baadhi ya masharti na ushauri.

UDHAMINI​

Vijana wengi Tunakosa mikopo kwa kukosa udhamini. taasis za mikopo zinahitaji mkopaji awe na mdhamini na huyo mdhamini awe ni mtumishi,awe na akaunti hai . kwa wale ambao tumekosa udhamini tunashindwa kufanya biashara kwa kukosa mtaji ambao ni mkopo unao hitaji udhamini. ushauri Taasis ziruhusu mtu mmoja mmoja kujidhamini kwa kutumia kitambulisho cha Taifa au cheti cha elimu.

UTUMISHI WA UMMA/MFANYAKAZI
Hiki ni kikwazo kwa wafanyakazi wanaojihusisha na taasis ndogo au wale ambao bado hawajapata kazi. ni wazi kwamba watoa mikopo wanawapa upendeleo sana watumishi wa umma katika fursa hii hali inayo wafanya vijana tusio na kazi pamoja na wahitimu kushindwa kupata mikopo ambayo itatumika kuondoa umaskini kwa jamii na taifa kwa ujumla.

MALI ZISIZO HAMISHIKA/ LESENI YA BIASHARA/ KADI YA GARI
vigezo tajwa hapo juu bado vimeendelea kutunyima fursa sisi tusio kuwa navyo. na washauri waruhusu wazo au blueprint yakile unachotaka kufanya kuwa ni moja ya sifa ya kupata mkopo unaohitaji. yaani mimi naenda benki nawaeleza wazo langu mwanzo mpaka mwisho na namna gani mpango wangu utaleta faida kisha benki wanikopeshe kwa kutokana na mawazo yangu bila kuhitaji vitu visivyo hamishika leseni ya biashara au kadi ya gari.
 
Back
Top Bottom