Masharti ya kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM)

Mahesabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2008
Posts
6,759
Reaction score
6,851
Kuwa mtu anayeheshimu watu. Kuwa mtu anyefanya juhudi ya kuielewa, kuieleza, kuitetea, na kuitekeleza itikadi na siasa ya CCM. Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha utu, na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo.
  • .
  • Kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake. Kuwa mbu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya umma, kulingana na miongozo ya CCM.
    .
  • Kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake, kuwa mwaminifu, na kutokuwa mlevi au mzururaji. Kuwa ama mkulima, mfanyakazi au mwenye shughuli nyingine yoyote halali ya kujitegema.
    .
  • Mtu atakayetaka kuwa mwanachama atajaza karatazi maalum ya maombi na kuipeleka kwa Katibu wa Tawi anapoishi Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi itafikiria na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya uanachama.
    .
  • CCM kitakuwa na mpango wa kutoa mafunzo kwa wanachama wake juu ya imani, malengo na madhumuni ya siasa ya CCM kwa jumla.
    .
  • Mtu akikubaliwa kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo: Atatao kiingilio cha Uanachama atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda kulipa ada ya waka mzima mara moja.
    .
  • Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmasharui Kuu ya Taifa.
    .
  • Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa ama:- Kujiuzulu mwenyewe; Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba Kutotimiza mashari ya uanachama; au Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
    .
  • Mwanachama ambaye uanachama wake unakiwsha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa. Itabidi arudishe Kadi ya Uanachama wa CCM.
    .
  • Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama akitaka tena kuingia katika CCM itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya wilaya au kikao kilichomwachisha au kumfukuza Uanachama.
    .
  • Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba Uanahcama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

SORCE:Chama Cha Mapinduzi - CCM
 
Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kujikuta navutiwa nacho.
..nina imani nitaweza kulijenga taifa langu kwa umakini zaidi nikiwa kama mwanachama wa CCM .
..kama kuna kiongozi yeyote wa CCM naomba anisaidie namna ya kujiunga na chama na kupata kadi ya uanachama.
Cc Simiyu Yetu FaizaFoxy MSALANI na wanaCCM wote.
 
Last edited by a moderator:

karibu mkuu tena sana wenye akili timamu woote wanajiunga na ccm chama makini.
 
Last edited by a moderator:
nenda kwenye chama cha wajinga wenzako cccm chama chakavu buku saba za kila siku viroba zitawauwa ccm imeshakufa
 
Kumbe wewe ni KILAZA....nlikua nakuona mmu nkafikiri mwerevu...kumbe empty head kabisa
 
Nadhani ni utashi wake, tuheshimu uamuzi wake!
 
Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kujikuta navutiwa nacho.
..nina imani nitaweza kulijenga taifa langu kwa umakini zaidi nikiwa kama mwanachama wa CCM .
..kama kuna kiongozi yeyote wa CCM naomba anisaidie namna ya kujiunga na chama na kupata kadi ya uanachama.
Cc Simiyu Yetu FaizaFoxy MSALANI na wanaCCM wote.

Karibu sana kwenye chama kilichothubutu, kikaweza na sasa kinajenga nchi kupitia ilani yake ya uchaguzi 2010.

CCM hatufanyi mambo ya kisiasa theoretically bali tunafanya practically.

Tembelea kwenye shina lolote la wakereketwa, Balozi wa nyumba kumi au ofisi ya CCM tawi/kijiji na huko watakupa maelezo ya taratibu za kuwa mwanachama.
 
Hongera sana... Lakini mbona hauweki Qualifications zako? au ndio another BLOOD SUCKER ?

Sidhani kujiunga na CCM unahitaji MATANGAZO... Iko kila kona JUST WALK IN...
 
Oooh nadhani hapa nitapata mwongozo sahihi zaidi,huku nilipo sijawahi kuona ofisi za CCM.
Hongera sana... Lakini mbona hauweki Qualifications zako? au ndio another BLOOD SUCKER ?

Sidhani kujiunga na CCM unahitaji MATANGAZO... Iko kila kona JUST WALK IN...
 
Shukurani zangu zikufikie,nitazitafuta ofisi mpaka nizipate.naipenda sana CCM.
Karibu sana kwenye chama kilichothubutu, kikaweza na sasa kinajenga nchi kupitia ilani yake ya uchaguzi 2010.

CCM hatufanyi mambo ya kisiasa theoretically bali tunafanya practically.

Tembelea kwenye shina lolote la wakereketwa, Balozi wa nyumba kumi au ofisi ya CCM tawi/kijiji na huko watakupa maelezo ya taratibu za kuwa mwanachama.
 
Unatamani niwaze uwazacho wewe?nipende upendacho wewe?nifanye ufanyacho wewe?
Nipo kwenye nchi ya kidemocrasia yenye mfumo wa vyama vingi,nina uhuru wa chama gani nisimame nacho.
Kumbe wewe ni KILAZA....nlikua nakuona mmu nkafikiri mwerevu...kumbe empty head kabisa
 
Hongera sana mkuu Jawilat kwa kufanya maamuzi sahihi.

Karibu sana CCM.
 
Last edited by a moderator:
Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kujikuta navutiwa nacho.
..nina imani nitaweza kulijenga taifa langu kwa umakini zaidi nikiwa kama mwanachama wa CCM .
..kama kuna kiongozi yeyote wa CCM naomba anisaidie namna ya kujiunga na chama na kupata kadi ya uanachama.
Cc Simiyu Yetu FaizaFoxy MSALANI na wanaCCM wote.

utakuwa mzigo kama c mchawi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom