Masharti mapya ya kozi za afya yatazamwe upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masharti mapya ya kozi za afya yatazamwe upya

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BGG, Apr 8, 2012.

 1. B

  BGG Senior Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi karibuni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeangaza vigezo na masharti mapya ya kujiunga na kozi mbalimbali za afya gazi ya cheti na stashahada. Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupita tovuti yake, waombaji wa mafunzo ya afya kwa mwaka wa masomo 2012/2013· Ngazi ya cheti ni lazima ufaulu wao uwe wa kiwango kisichopungua (minimum) pointi 28 na alama ‘D’ (kidato cha nne) kwa masomo ya biologia, kemia na fizikia. Ufaulu wa kiingereza na hisabati ni kigezo cha ziada. · Ngazi ya stashahada : ufaulu wa ‘C’ mbili katika masomo ya biologia na kemia, na alama ‘D’ kwa somo la fizikia (kidato cha nne) au ufaulu wa alama ‘E’ (kidato cha sita) katika fizikia, biologia na kemia. Ufaulu wa kiingereza na hisabati ni kigezo cha ziada. Kwanza kabisa, tunapenda kuipongeza Wizara ya afya na ustawi wa jamii na hasa kitengo cha maendeleo ya rasilimali watu kwa sekta ya afya na wadau wote waliohusika kubadili vigezo vilivyokuwepo awali vya udahili. Ambavyo vilitoa nafasi kwa kozi za afya ngazi ya cheti na stashahada kwa wale tu, waliofaulu masomo yote ya msingi (kemia, biolojia na fizikia) katika kikao kimoja cha baraza la mitihani. Pia vigezo vya awali havikuzingatia masomo mengine ya ziada kama vile hisabati na kiingereza. Masharti(vigezo) vipya vya udahili tafsiri yake ni kwamba, wanafunzi waliofeli kidato cha nne somo la fizikia na wamefaulu biolojia, kemia na masomo ya ziada, hawawezi kupata fursa ya kusoma kozi za afya hata kama wamemaliza na kufaulu kidato cha sita katika michepuo ya kemia, biolojia na lishe (CBN), kemia, biolojia na jografia (CBG) au kemia, biologia na elimu (CB-Ed) wanakosa fursa ya kusoma kozi za afya kwa sababu tu wamekosa kigezo cha fizikia. Hata hivyo uamuzi huo wa wizara umepokewa kwa hisia tofauti na wadau mbalimbali wa sekta ya afya nchini kwa madai kuwa haukuzingatia mazingira na hali halisi ya vijijini na sekondari za kata.
  Mmoja wa walimu wa chuo cha maafisa tabibu cha Mtwara Clinical Officers Training Collage, Dr. Raphael Mwita anaona kuwa kuweka ulazima wa kufaulu somo la fizikia ni kupingana na malengo makuu ya mafunzo ya maafisa tabibu (Clinical officers).Dr. Mwita anayataja malengo ya mafunzo ya maafisa tabibu kuwa ni pamoja na kufanikisha mpango wa serikali wa kuboresha huduma za afya vijijini hivyo kuwa na ulazima wa kupata wanafunzi wanaotoka maeneo hayo ambao ni rahisi kurudi kutoa huduma katika maeneo yao. “Kuna uhaba mkubwa wa walimu wa somo la fizikia katika sekondari za kata hasa zile za vijijini. Kule shule nyingi hazina walimu wa fizikia, hivyo serikali ingeona busara ya kubakiza masomo ya msingi kuwa kemia na biolojia. Fizikia kubaki katika masomo ya ziada pamoja na hesabu, kiingereza na kiswahili kama ilivyo kwa wezentu wa jumuiya ya afrika mashariki (kenya na Uganda). Anasema kuwa ni rahisi kumpeleka mtu aliyezoea mazingira ya kijijini kufanya kazi huko kuliko waliozoea maisha ya mijini ambao wengi hulalamikia mazingira magumu na kuishia kuripoti tu na kurudi mijini.Naye Mkurugenzi wa shirika la Tandabui Health Access Tanzania (THAT)/Afya Radio
  ambaye pia ni daktari kitaaluma, Dr. Joseph Kavit anasema kuwa maamuzi ya wizara yanapaswa kuangaliwa upya ili kuwatendea haki watanzania.
  Dr. Kavit anatoa mfano wa mpango uliokuwa ukitumika zamani kwa waganga wasaidizi vijijini (RMA) ambao wengi wao walikuwa darasa la saba au kidato cha nne na hawakusoma masomo ya sayansi au kufaulu fizikia, lakini walipoendelezwa wakawa na ufanisi mkubwa katika kazi zao.“Wanganga hawa wa RMA wengi wao walijiendeleza hadi kufikia kuwa madaktari bingwa. Mifano ipo, hivyo tunaiomba serikali isipoteze fursa hizo bali iangalie uwezekano wa kupanua wigo ili kuwe na uwiano mzuri kati wataalamu wa sekta hiyo na wateja wanaopaswa kuwahudumia” Anasema Dr. Kavit. Pia aliongeza kwa kusema “ndio maana, hata jopo la wataalamu wa wizara ya afya, NACTE na wengine walipokaa kutengeneza mitaala ya kozi za utabibu ngazi ya cheti (NTA level 4: 2009 version) na ngazi ya stashahada (NTA Level 6: 2009 version) waliliona hili. Nakuweaka ufaulu wa msingi kuwa katika somo la biolojia na kigezo cha ziada kuwa somo la kiingereza”.
  Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo zinasema kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokana na ufaulu wa wanafunzi kuwa mkubwa sana ukilinganisha na nafasi zilizopo katika vyuo vya afya na hivyo kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuweka kigezo cha fizikia kama la lazima ili kuweza kujiunga na kozi za afya. Aidha, wananchi wanahoji ni kwavipi sharti hili liwepo kwetu na hasa katika kipindi ambacho Tanzania inashika nafasi ya mwisho kati ya nchi 52 za kiafrika kwa kuwa na uwiano wa madaktari wawili kwa wagonjwa 100,000 sawa na Malawi. “Serikali haikupaswa kuweka masharti yanayolenga kuwanyima wanafunzi fursa ya kujiunga na mafunzo ya afya kutokana na uhaba wa nafasi za vyuo , bali iweke utaratibu mzuri wa kuwadahili kupitia chaguo la kwanza, chaguo la pili na la tatu” Anasema Katongole Danstan mkazi wa Isamilo mjini Mwanza.Pia iendelee kuimarisha na kuendeleza kasi ya utekelezaji ya mkakati wake wakuongeza vyuo vya sekta ya afya vyenye ubora stahiki.
  Hata hivyo, utafiti uliofanywa na mwandishi wa makala haya umebaini kuwa vyuo vingi vya taasisi za kidini vinavyotoa mafunzo ya afya katika mikoa ya Kanda ya Ziwa vina idadi kubwa ya wanafunzi kutoka nchi jirani ya Kenya. Hivyo kupingana na hisia za wizara kuwa wanafunzi ni wengi kuliko uwezo wa vyuo vyake.

  Hivyo badala ya kuweka nguvu katika vigezo vya kupunguza idadi ya watanzania wanaopenda kujiunga na tasnia ya utabibu, ni bora mkazo huo ukawekwa katika kusimamia upanuzi, ujenzi na ubora wa vyuo vilivyopo ili kuweza kukidhi matakwa ya Mpango Mkakati wa Taifa wa Kuongeza Rasilimali Watu na Kuboresha viwango vya huduma katika Sekta ya Afya kama ulivyobuniwa mwaka 2008 na Mpango wa Maendeleo wa Afya Msingi (MMAM, 2007-2017).
  Mipango na mikakati hiyo mizuri ya serikali, inategemea kwa kiasi kikubwa utashi wa wizara husika ikishirikiana na NACTE ambayo kimsingi haipaswi kuwa kikwazo kwa kuweka masharti magumu yanayolenga kuongeza uhaba wa wataalamu hata wa kiwango cha stashahada na cheti badala yake kutakiwa kubuni njia mbadala ya kuwapa fursa wenye wito wa kuwahudumia watanzania wenzao pasipo kutanguliza maslahi binafsi.Pia, Wizara inapaswa kutambua kuwa taifa linapokuwa na uhaba wa watoa huduma za muhimu kama matibabu, huzaliwa tatizo la rushwa na kuzorota kwa huduma kwani unapokuwa na uwiano mkubwa wa wagonjwa wanaong'ang'ania kupewa huduma na mtaalamu mmoja, kanuni ya Uchumi ya ‘ugavi na mahitaji’ huchukuwa nafasi yake, ambapo mwenye pesa huweka dau ili apewe huduma kwa upendeleo. Mungu ibariki Tanzania!

   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kuweni makini jamani. Kuna kizazi kitatokea hakijui kabisa hesabu humu nchini. Uganda huwezi kwenda form five kombi yoyote kama una D ya hesabu. Ni afadhali fizikia hiyo hata mi naweza kusapoti lakini hesabu NO! Tuachane na kugawa dozi kwa mazoea ya fulani alimpa mls kadhaa,lazima tukokotoe dozi! Leo hii ukiingia sehemu nyingi watu wana mifagio ya hesabu na ndo wanahusika na mipango ya maendele ya taifa hili aafu tunajiuliza kwa nini hatuchomoki! Leo hii ukienda vyuo vingi vya watu wanaosoma arts ukawapa mtihani wa kuvmia common mathematics unakula vichwa kibao. Tumekosa sera ya kuendesha elimu yetu. Yes kuna manesi kibao wana majembe ya hesabu lakini lazima tubadilike,tusitumie uzoefu. Ndo maana mpaka leo watu kwenye kampeni wanazungumzia mambo ya maji! Ni aibu!..50 years bado tunazungumzia mambo ya RMA? Wenzetu wanazungumzia specialists sie tunazidi kurudi nyuma.! Nina fomu ya admission hapa nimeona bado rma ipo, i was shocke!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Imbombo ngafu
   
 4. m

  msafi Senior Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tatizo si hizo admission requirement bali ni uhaba wa vyuo vya serikali na kutokuwa na sera madhubuti. Serikali inaongelea kuwa na zahanati kila kijiji, kituo cha afya kila kata n.k n.k. Kwa nchi makini, ukiongelea kuongezeka kwa vituo vya afya lazima uwekeze katika vyuo na kufungua vingi zaidi ili kuongeza rasilimali watu, lakini kwa Tanzania hapana. Sasa ukweli ni kuwa idadi ya vijana wanayoomba kujiunga hasa vyuo vya serikali ni kubwa kuliko idadi ya vyuo, mfano pale muhimbili, kila mwaka kati ya vijana 500-600 wanaomba kozi ya fundi dawa sanifu (diploma in pharmaceutical sciences), idadi inayotakiwa ni 20-30 tu, sasa utaachagua vipi hapo kama si kuongeza viwango vya ufaulu???? Haya, angalia bajeti zinazopelekwa kwenye hivyo vyuo vya serikali, haikidhi mahitaji halisi, na vyuo vingine havina walimu wa kutosha, bado tunaimba zahanati kila kijiji!!!! Na vyuo vingi vya binafsi gharama ziko juu ndio maana wakenya na watu to nje ya nchi ndo wanamudu.Hatuna vipaumbele nchii hiii.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  baada ya kuvuruga elimu sasa ni zamu ya afya.
  Eti matabibu kujifunza kwa njia ya mtandao!
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hilo swala huwa najiuliza siku nyingi sana kuna uhusiano gani kati ya fizikia na afya?
   
 7. m

  msafi Senior Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Na hili wamelishupalia kweli hasa CMO aliyepita, unajiuliza wapi na wapi utabibu ukasomwa kwa njia ya posta au mtandao??? badala ya kuongeza vyuo na kuviboresha ati ndo wanaishauri serikali katika hili.......hopeless
   
 8. m

  msafi Senior Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kiukweli hakuna uhusiano isipokuwa kinachogomba hapo ni idadi ya waombaji Vs idadi chuo inataka, zamani ili usome shahada ya Pharmacy makerere university au Nairobi university, ulitakiwa kuwa na ufaulu wa A katika fizikia, kemia na biologia, tatizo lilikuwa idadi wayotaka ni ndogo sana. vivyo vivyo kwa kozi zingine za afya, lakini vyuo vinapopanuka na kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi, masharti hupungua, mfano sas hivi unaweza kusoma medicine ukiwa na fizikia D kemia C na biology C.
   
 9. B

  BGG Senior Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mhe. hamisi kigangwalla Mbunge wa Nzega nimeona thread yako katika jukwaa hili la elimu ukizungumzia upatikanaji wa ajira kwa vijana.wewe ni mjumbe wa kamati ya bunge ya afya, elimu na huduma za jamii unasemaje juu ya hii fizikia? Na unasemaje juu ya mkakati wa kuongeza vyio?
   
 10. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wanachekesha
   
 11. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mkuu yaani fizikia na afya ni baba na mama. Unaweza ukaangalia umuhimu wa fizikia katika afya ukiangalia vitu vifuatavyo:
  1. Utengenezaji Mashine za Kupimia: Hapa kuna vipimo kama Ultrasound, X-rays, CT Scan, MRI, Mammography, Fluoroscopy n.k
  2. Tiba: Kuna kutibu kansa kwa mionzi, kuna kuurudisha moyo upige kazi kwa utaratibu (Defribillation) na hapa ndipo waona Nuclear Medicine imejikita.
  3. Kuna vipimo vya kifisiologia kama EKG (kupima umeme wa moyo), endoscopy, pulse oximeter, Kupima BP, ultrasound n.k
  4. Kuwa na elimu ya kujiepusha na mionzi, kama kwenye vyumba vya CT Scan, MRI na Xray. n.k.
  Halafu hiyo tabia ya kutaka failures ndio waende kwenye cadres za chini ndani ya afya unatakiwa ufutwe mara moja. Tusichezee maisha ya watu.
   
 12. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Na wale wanao feli Tz wakaenda uganda kusoma V,na math wamefail
   
 13. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mkuu hata mimi nawashangaa kusikia watu hawajui uhusiano wa fizikia na masomo ya afya.

  Halafu ni uzandiki kujidai eti unaijua kemia na biolojia halafu zero kwenye fizikia na hisabati.

  Kuna wahuni wako wizarani wanabadilisha mambo bila kujua watu walivuja jasho kuyaandaa.
   
 14. B

  BGG Senior Member

  #14
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na swala la kwamba fizikia na medicine ni kama baba na mama.Nimejaribu kufuatilia wenzetu wa afrika mashariki (kenya medical training college: hichi ni chuo cha serikali ya kenya) nilichokuta ni kwamba maeneo ya diploma au certificate za medical eng, dental technology, medical imaging, optimetry,orthopaedic technology na neurophysiology somo la fizikia ni lazima ila kozi za clinical medicine, pharmacy,community nursing nk fizikia ni somo la ziada. Walichojaribu hapa ni kuwa more details katika umuhimu wa kila somo kwa kozi fulani ili kupanua uwingo.point yako imekuwa ya msingi mno na hivyo basi kwanini nasisi tusipanue uwigo? Kwani hata waganda:nimeangalia kampala international university, na kenya nimepitia toviti ya MOI university mtindo ni huhu wa kuwa na mchanganuo na si generilization.
   
 15. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  unadhani kinachofanyika kenya na uganda ndio kizuri?
   
 16. B

  BGG Senior Member

  #16
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Swali hili linaweza kujibiwa kama tukiangalia competence ya wataalamu wa Tanzania, je wana uwezo zaidi kuliko wakenya na waganda?
   
 17. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mh. Kigwangala, tafadhali jitokeze utoe msaada wako kwa niaba ya kamati yako suala hili linahitaji political intervation, isije ikawa serikali ina uhaba wa vyuo sasa iongeze vigezo ili kupunguza watu. Vijana wengi wanaotoka shule za kata matokeo yao ndo hayo sasa wabaki mtaani kweli?
   
 18. Nyanda Dindai

  Nyanda Dindai JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 723
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 180
  Mkuu mimi ni mwanafunzi wa cbg kidato cha sita nilipata daraja B katika somo la fizikia o level na daraja c katika somo la hisabati,katika mashart hayo mapya je nnaruhusiwa kusoma medicine,phamacy au nursing iwapo ntafaulu masomo ya biologia na chemia katika mtihani wangu wa mwisho?
   
 19. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  jirani hapa Physics ni very significant
   
 20. B

  BGG Senior Member

  #20
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kwa kutumia cheti chako cha o-level unaweza kujiunga na diploma ya clinical medicine, nursing nk pia kwa sasa mtaala wa advance diploma na degree ya bachelor of science in clinical medicine unatengenezwa hivyo untaweza kuunganisha hadi shahada kwa mfumo unaokuja .ila kwasasa hayo masomo yako ya a-level fizikia ni kigezo cha lazima ilikuweza kuingia shahada.
   
Loading...