Masharobaro wagombania penzi la bi mkubwa - Da

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
BI.ROSEMARY OTHUMANI [54] mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, amejikuta akipata aibu ya mwaka kwa watoto na majirani zake baada ya vijana wawili kupigana na kutoana ngeu kwa madai ya kila mmoja akidai ni mpenzi wa mama huyo
Tukio hilo la kusisimua na kwa upande mwingine la kusikitisha lilitokea jana majIra ya saa 1 jioni nyumbani kwa mwanamke huyo

Mtandao huu ulishuhudia nusu mpambano huo na watu wengi wakiwa wamepatwa na bumbuwazi kutokana na tukio hilo

Mmoja wa shuhuda ambaye aliwahi kuona picha kamili aliyejitambulisha kwa jina la Saada [27] ambaye jirani na mama huyo alidai kuwa mama huyo aligonganisha magari na ndio chanzo cha kutokea kwa ugomvi huo

Ameda kuwa, mama huyo mjane miaka mitano iliyopita baada ya kupoteza mume wake kwa maradhi ya kansa amekuwa na tabia ya kujihusisha na mapenzi na vijana wadogo ambao ni saizi ya watoto wake tabia ambayo alishazoeleka nayo mtaani hapo

Amedai, tabia hiyo ambayo watoto wake wa kike walishaipigia makelele bila ya mafanikio na mama yao huyo kudai mapenzi hutua sehemu yoyote na mwishowe watoto walinawa mikono kuhusiana na suala hilo la kumuonya mama yao

Amedai, mama huyo alikuwa akijihusisha kimapenzi na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Beka [30] na watu wengi walifahamu mahusiano yao na baadae baada ya kuzidiwa alimtaka kijana huyo ahamie nyumbani kwake na kudaiwa alihamia

Mpashaji habari hii bi. Saada aliendelea kupasha habari kwenye mtandao huu kuwa, Beka baada ya miezi kadhaa alidaiwa alifunguliwa biashara na mama huyo ambapo ilimladhimu asafiri mara kwa mara kusimamia biashara hizo

Imedaiwa kuwa, wakati mwingine husafiri na huchukua hata mwezi mmoja au mawiki kadhaa katika biashara hizo

Imedaiwa, mama huyo alitumia mwanye wa kusafiri kwa Beka kwa kujihusisha kimapenzi na kijana mwingine kwa kudhani amepata bahati ya mtende kwa kutumia mali za mama huyo bila kujua kama ana mume mwenza

Imedaiwa kuna baadhi ya watu waliokuwa wakimuona na mama huyo walijaribu kumuibia siri lakini kijana huyo alidhani huenda ni kumchukia kulingana na anavyojihusisha kimapenzi na mwanamke aliyemzidi umri

Imeendelea kupashwa kuwa kijana huyo alikuwa akifika nyumbani kwa mama huyo mara chache

Siku ya tukio, ambapo waswahili walisema lisemwalo lipo ama halipo basi liko njiani, Beka alirudi jijini Dar es salaam akitokea mkoani Mwanza kwa ndege ya Precision Air na alitinga jijini humu majira ya saa 10 jioni bila ya kumpa taarifa mama huyo kama anarudi

Ndipo majira ya saa 12 Beka aliwasili nyumbani kwa mama huyo bila ya taarifa kwa kujiamini, huku akimpa mshituko mwenyeji wake kwa kutokutoa taarifa

Mbaya zaidi mama huyo alimpa mwaliko Yule kijana mwingine aje nyumbani kwake kwa siku hiyo ndipo hapo magari yalipogongana na kuleta mshike mshike nguo kuchanika mtaani hapo huku kila mmoja akitunisha misuli yake na kila mmoja akidai kummiki huyo mama

Vijana hao walikutana huku kila mmoja akiwa anamshangaa mwenzake na mama huyo alimtumia ujumbe mfupi wa maneno Yule kijana mwingine kwa kumwambia aondoke kwa muda huo kwani alifikwa na mgeni ujumbe ambao Beka aliushitukia na kudaka simu ya mkononi ya kijana huyo na kugundua kinachoendelea na kuanza kumkunja na hatma yake ugomvi kukua

Hali ilikuwa mbaya kwa mama huyo na kupelekea kuomba msaada kwa walinzi na majirani waje kugombelezea ugomvi huo na hatma yake watoto waliokuwa wakiishi karibu nae walipigiwa simu na majirani na kufika hapo na matokeo askari waliingilia ugomvi huo

Mama huyo alichukuliwa ili kwenda kutoa maelezo kituo cha polisi na kuwaacha watoto na wajukuuu wakiwa na aibu tele mtaani hapo

Imedaiwa mama huyo ni mfanyabiashara ambapo biashara hiyo haijawekwa wazi, na marehemu mume wake aliweza kumuachia mali zikiwemo nyumba mbili na magari mawili ya kutembelelea gari moja ilidaiwa alichukua binti yake mkubwa aliyedaiwa kuwa na umri wa miaka 32

Mama huyo alijaaliwa kuwa na watoto watatu ambapo wawili wa kike na mmoja ni wa kiume mdogo aliyedaiwa kuwa mwaka wa nne UDOM

Masharobaro wagombania penzi la bi mkubwa - Dar
 
mbona ndo life style ya masharobalo wengi tu daslam hii
 
Kila cku nyiny tu ndo m2chue kikongwe miaka 64 na bint wa 20, na sisi zam ye2 jaman, hak sawa mnachoshangaa nini?
 
Back
Top Bottom