Mashangingi ya CHADEMA!!

Mashangingi ya CHADEMA!!

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,238
CHADEMA ilitoa hoja za msingi sana wakati wa Kampeni za Mwaka 2010 na zikakubalika na wananchi wa Tanzania.

Mgombea Urais wakati huo MH: Willbroad Peter Slaa na wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge walikuwa wanatoa tuhuma kwamba serikali iliyopo madarakani inafuja fedha za wananchi kwa kununua magari ya kifahari aina ya Land Cruiser VX na V8 wakati fedha hizo zingetumika vizuri zingeleta maendeleo kwa wananchi. Katika kukoleza hoja hiyo ikaaminishwa kwamba kama CHADEMA ikishika madaraka basi magari hayo ya kifahari yatauzwa na madala yake yatanunuliwa magari madogo ya bei rahisi.

Slaa alikuwa anasema aina ya magari yanayotumiwa na Wakuu wa Wilaya na Mikoa thamani yake ni sawa sawa na gari moja kujenga Zahanati Nne vijijini. Wanachi waliambiwa kwamba magari hayo yatauzwa na fedha itakayopatikana itatumika kuwekeza kwenye Elimu.

Baada ya uchaguzi wa Mwaka 2010 viongozi wa CHADEMA hawatumii VX au V8 kwa matumizi ya kichama na yao binafsi, au thamani ya magari hayo imeshuka baada ya wao kuanza kuyatumia?

UKIKEREKA SEMA UPENDAVYO!!
 
Acha kufikiria kwa kutumia ma***** huko vijijini utaenda na Corolla au GX 100?
 
Hujaeleweka mkuu, kama hawatumii vx na v8 sasa tabu ipo wapi??
 
Nazungumzia "consistency" ya chama kwenye mambo wanayoyapigania wakati wa Kampeni. Kusema akili yangu mbovu hakuondoi ukweli kwamba hata hayo mashangingi ya CHADEMA yananunuliwa na kwa kodi za wananchi. Wewe hujui kuna baadhi ya wabunge kabla ya kuwa wabunge hata Baiskeli walikuwa hawana uwezo wa kununua.

Unajisahaulisha kwamba wabunge wote walipewa mkopo wa shilingi Milioni 90 na ofisi ya Bunge kwa ajili ya kununulia magari yao?
 
MBOWE anatumia gari la kiongozi wa upinzani bungeni (KU) aina ya Land cruser V8 alilotangaza kurudisha bungeni na kweli alirudisha lakini kalichukua kimya kimya bila kutuambia ameamua kulichukua......siasa bana.


Dk. Slaa anadaiwa kulipwa mshahara zadi ya milioni 7 kwa mwezi ambao unazidi mshahara wa mbunge.


Tukipata maelezo yao dhidi ya tuhuma hizi itapendeza.
 
MBOWE anatumia gari la kiongozi wa upinzani bungeni (KU) aina ya Land cruser V8 alilotangaza kurudisha bungeni na kweli alirudisha lakini kalichukua kimya kimya bila kutuambia ameamua kulichukua......siasa bana.


Dk. Slaa anadaiwa kulipwa mshahara zadi ya milioni 7 kwa mwezi ambao unazidi mshahara wa mbunge.


Tukipata maelezo yao dhidi ya tuhuma hizi itapendeza.

hizi tuhuma porojo,jifunze maana ya tuhuma huenda matumizi yake huyajui.
 
kwa hiyo ya chadema yamenunuliwa kwa kodi za wakenya au?

kabla ya kurukia mada fanya utafiti ujue kama CDM wana hayo mashingingi sio mtu kachoka ku-masaburi ana rusha uzi hapa na wewe unarukia bila kujua ukweli wake.CHOKA KUFANYA KAZI USICHOKE KUFIKIRIA.
 
si utumie lugha inayoeleweka,
utachanwa bure hapa kisa husomeki.
 
nazungumzia "consistency" ya chama kwenye mambo wanayoyapigania wakati wa kampeni. Kusema akili yangu mbovu hakuondoi ukweli kwamba hata hayo mashangingi ya chadema yananunuliwa na kwa kodi za wananchi. wewe hujui kuna baadhi ya wabunge kabla ya kuwa wabunge hata baiskeli walikuwa hawana uwezo wa kununua.

Unajisahaulisha kwamba wabunge wote walipewa mkopo wa shilingi milioni 90 na ofisi ya bunge kwa ajili ya kununulia magari yao?

Sijui watu huwa mnapasi vipi mtihani kama kujieleza kwenyewe ndio huku. Hata maana ya mkopo hamuielewi?
 
ila ni ukwel kwamba kabla ya kuwa wabunge baadh ya wabunge wa cdm walikuwa na escudo na sasa wana mashangingi ! as long as wamenunua kwa pesa yao , hamna shida!
 
Mbunge wangu wa CHADEMA alikua anatembelea Nissan Terrano. mwezi mmoja baada ya kuapishwa kavuta VX. Nadhani wangeanza kutuonyesha wao kwa vitendo ili tuweze kuwaamini wanayoyasema pindi watakapochukua nchi. kama wao tu ndani ya chama wameanza kuonyesha matabaka hali kadhalika wakichukua nchi itakua hivyo hivyo. wenyeviti wa matawi hawana hata baiskeli ye kufanyia shughuli za chama wao wameongeza matumizi kwa kujinunulia magari ya gharama. hii ndio siasa ya Bongo
 
Issue si vx v8 bali issue ni strata nani apewe lipi ni aibu la waziri mkuu linapofanana na mkuu wa wilaya. Kuna alternatives nyingine za suvs kama land rover,vw audi mercs bmw land cruiser lx hardtop.
Lets say waziri mkuu apate vx v8 , mawaziri kawaida vx plain, naibi waziri say vw toareg wakuu wa mikoa landrover puma wakuu wa wilaya suzuki grand vitara na kadhalika.
Shida ni kwamba hakuna daraja nani apate lipi.
As well govt iki diversify pool ya magari itaweza kutathmini magari gani ni reliable running costs durability na vitu kama hivyo. Naona hiyo ndio hoja ya msingi hatuwezi condemn bila kuwa na suggestion kwa hao procurement officers wavivu wa kufikiri.
 
Nakumbuka Slaa alitaja zaidi ya mara moja kuwa bei ya gari moja (hayo unayoyapigia kelele) ni zaidi ya shilingi milioni 200, je, kuna gari lolote CDM imelinunua kwa bei hiyo, ili hoja yako ipate uhalali wa kujadilika?
 
mkuu Kigalama , ccm nailinganisha na Nabii Kibwetele wa Uganda na wewe ni muumini wake,subiri kuchomwa moto maana sumu manazolishana bado hushituki kicha cha mwenda wazim kajisemea mzee Rukusa.
 
Back
Top Bottom