Mashambulizi ya Virus Yanavyobadilika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashambulizi ya Virus Yanavyobadilika

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Apr 24, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0


  Wengi wetu tumezoea mashambulizi ya virus ni pale inapofanya computa yuko kutokufanya kazi vizuri au kwenda mwendo wa taratibu au kufuta baadhi ya files na vitu vingine vingi tu .

  Siku zinavyokwenda mashambulizi haya yanazidi kuongezeka zaidi kwenda mbali zaidi ya kufanya kompyua kwenda taratibu haswa kwa wale wanaotumia komputa zao kwenye mitandao ndio wahanga wakubwa wa mashambulizi] haya .

  Ni kawaida kutembelea search engine ukatafuta kitu ukapata kiunganishi kwenda kwenye tovuti ambayo antivirus yako haisemi kama ni haramu au la , ni kawaida kukuta wahalifu wakitoa programu za bure huku wakiweka vitu vyao hii iko zaidi kwenye mitandao kama rapidshare au megaupload .

  Na imeonekana watu wengi wanapokuwa kwenda mitandao wanapenda sana kushusha vitu haswa programu ndogo ndogo au vitabu na mengine ambayo wanaweza kutumia kwenye mambo yao haswa wale wanaotumia migahawa.

  Kama uliwahi kutembelea tovuti ya www.pdfonline.com miezi 5 iliyopita kisha ukaja kutembelea siku za karibuni kuna kitu Fulani utakuwa umekiona nacho ni kwenye upande wa kubadili faili toka pdf kwenda word kwa sasa hivi unapobadili na kushusha kwenye komputa yako huwa inaibana ndani ya folder .

  Unaweza kujiuliza kwanini PDF online waliamua kufanya maamuzi haya baada ya mashambulizi dhidi ya faili haswa zilizo kwenye mfumo wa word ambao ni wengi wanatumia ilikuwa ukishusha faili yako baada ya kubadili kama komputa imevamiwa na virus huyo basi utakuta ujumbe mfupi kukufahamisha uharibifu wa faili yako .

  Hilo ni moja tu hata ukitembelea mtandao wa AVAST www.avast.com nenda support kama unataka kushusha update mpya haswa ya toleo la 5.0 utaona nalo jina lake limebadilika kwa sababu update hiyo imekuwa inashambuliwa sana kwa siku za karibuni hii imefanana na jinsi Stinger ilivyokuwa inashambuliwa huko nyuma pamoja na baadhi ya updates za programu ya mcafee 7.0 na kuendelea .

  Kwa siku za karibuni mashambulizi dhidi ya kivinjari haswa internet explorer nao iliongezeka kidogo utaona kwamba wale watu wasiojua wanaweza kudanganyika kwenda anuani za tovuti bandia kama kivinjari chake kimevamiwa bila ya yeye kujua .

  Lakini hili suala la mashambulizi dhidi ya vivinjari limekuwa tete kwa kipindi kirefu kidogo kutokana na antivirus nyingi kutokuwa na uwezo wa kutambua vingi vinavyuoendelea kwenye kivinjari labda mpaka pale mtumiaji mwenyewe atakapoamua kubadilisha baadhi ya settings ili aweze kupata taarifa hizo .

  Wakati ambapo wahalifu wa njia ya mtandao wanabadilisha mashambulizi na kuelekeza kwa vile vitu unavyovishusha toka mtandaoni ni vizuri pia sasa hawa wadau wa teknohama watoe somo kwa wengine zaidi ili waweze kukaa tayari kwa mashambulizi mapya yanayoendelea kwa sasa ndani ya mitandao .

  Kwa wale wenye intenet café wabandike matangazo kwa wateja wao kuhusu mambo yanavyobadilika na kwa wale walio kwenye maofisi ni vizuri kuanza kuwafundisha wafanyakazi wenzao jinsi mashambulizi yanavyobadilika kwa siku za karibuni hii iendane na kubadilisha Miongozo ya TEKNOHAMA kwenye maofisi yao ili kuendana na wakati wa Sasa .

  Weekend Njema
   
Loading...